Je ulifanya nini baada ya kuhitimu Elimu ya Msingi

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,446
3,202
Baada ya kuhitimu Elimu ya Msingi, hususani miaka ya nyuma ikizingatiwa nafasi za kuendelea na Elimu ya Sendondari zilikuwa finyu, ilikuwa ni mwanzo wa harakati za kuanza maisha.
Je ulifanya nini baada ya kuhitimu (kumaliza) Darasa la Saba?
 
Nakumbuka ilikuwa mwishoni mwaka 1999 nilitoka kijijini nilikozaliwa na kukulia na kwenda Moshi Mjini kuuza duka kwa mshahara wa 15,000/- kwa mwezi.
Nilipanga kufungua duka langu baada ya miaka michache. Bahati nzuri/mbaya nilifaulu kuendelea na Sekondari.
 
Nakumbuka ilikuwa mwishoni mwaka 1999 nilitoka kijijini nilikozaliwa na kukulia na kwenda Moshi Mjini kuuza duka kwa mshahara wa 15,000/- kwa mwezi.
Nilipanga kufungua duka langu baada ya miaka michache. Bahati nzuri/mbaya nilifaulu kuendelea na Sekondari.

aisee mangi shukuru Mungu ulifaulu maana jf ungeisikia tu. Mi nilikuwa hapo hapo moshi nikaambiwa nichague moja kwenda maua seminari maana kuna shangazi yangu alikuwa anatamani sana niwe padri na alishanifanyaia mpango wa kuingia seminari,pili au niende bongo kwa mshua.kusikia bongo akili yooote ilihama,habari za kutumikia kanisani pale kristu mfalme zikaishia hapo hapo.nikaja bongo. Dingi akataka kunifungulia duka niuze koz elimu allishaona haina maana anapoteza hela yeke tuu,na hii ilitokana na ndugu zangu 3 kuharibu f4. da nikaa kwenye baa yake nikawa baamedi,nilikaa kaunta mpaka mwezi wa pili kuingia 3 bro alitoka masomoni akakomaa na mshua mpaka nikapelekwa shule.
 
darasa la saba nilikwenda form one moja kwa moja tena shule hiyo hiyo...nilikua na bahati kati zile shule tatu unazojaza ungependa upatiwe nafasi mi nilipata ile ya kwanza....
 
Nilijiunga na sekondari kwa masomo ya kidato cha kwanza...
 
Back
Top Bottom