Je ugovi wa mume na mke ndani ya nyumba unasababisha kutokutoaa matumizi?

ebu sahihisha heading yako kwanza,,,ilo neno( ugovi ) limebadili kabisa maana ya hicho unachomaanisha.
 
AHAHAHAAAA...UGOVIIIII ..AHAHAAAA...unanikumbusha mbali sanaaaa..ngoja niende toilet nikalichek kama lipo..maana mie ni kati ya endangered spices hapa mjini...kila mtu hiyo kitu hana keshatoa NIMEBAKI MIE TUUU...Natural man
 
Ugomvi watu hugombana mke na mume lakini pesa yachakula haija husu,labda awe mwanamme sio muelewa....
 
Je ugovi wa mume na
avatar71119_1.gif
Yeye mwambie aende hospitali akakate, ila wewe usikeketwe.

 
Ugomvi sio wakutoa matumizi tu ndugu yangu kuna mambo mengi mnaweza kutofautiana kimsimamo na kila mtu akawa anataka msimamo wake ndiyo ukubalike hakuna anayekubali kushindwa hapo tayari ni ugomvi, lakini hauna uhusiano na kununua chakula nyumbani. Kutokuihudumia familia, huwo sio ugomvi ni ushetani unakuwa umeingia kwa kutupiwa pepo au kulogwa na malimbwata ya nyumba ndogo au mpenzi wa nje. Ndugu zangu uchawi upo hata vitabu vyote vya dini vimeandika na kuthibitisha, mtu analishwa dawa anaisahau familia yake hata ndugu zake wa kuzaliwa anawaona kama panya. Familia zinahitaji kumshirikisha Mungu katika kila jambo ili ndoa zidumu bila kuwa na migogoro.
 
kiswahili chako kina utata kama ana govi mshauri aende kwa daktari akalitoe...kama ni ugomvi ndiyo unaomsababisha asitoe matumizi inaonyesha bado ana hasira na siyo mwelewa anataka ujue kwamba yeye ndo kidume...hapo kwake....
 
Lakini kweli! Kama kuna umgomvi mwanamke ananyimia unyumba, basi na mwanaume asitoe matumizi...
Just thinking aloud.
 
Kwakua waume wakigombana na wakeze ndani ya nyumba inakuaje?mume anakua hatoe matumizi
ya ndani ugovi unasababisha tusile?

Nadhani wengine wameshaongelea kichwa cha mada yako na utarekebisha. Wengine ukitaja hiyo kitu mwili unasisimka kukumbukia zoezi gumu la kuiondoa enzi zile za ujima walipokuwa wakiliondoa bila ganzi. Nitajikita kwenye vyanzo vya kugombana. Kwa ufupi viko vingi na wakati mwingine havifanani kabisa toka ndoa moja kwenda nyingine. Hilo la kutokutoa matumizi linaweza kuwa ni dalili tu za chanzo cha ugomvi.
 
Mwanaume anayekataa kutoa matumizi kisa ugomvi hana akili na je anakuwa anataka watoto wake wale kwa nani? Mi huwezi ondoka bila kuacha kodi ya meza hata kama atuongei nitawatuma watoto wakwambie au beki tatu
 
Ugomvi hua unaweza kutokea , Ila ikifikia kwa mume kutotoa matumizi hiyo ni kushindwa kwa mwanaume kuelewa yeye ni nani ktk nyumba husika

Unapokua KICHWA cha familia tunategemea kuona majibu CHANYA sio tu kwenye maendeleo bali hata kwenye matatizo kama haya ya kutoelewanaa na mwenzako ndani
 
Back
Top Bottom