Je UDSM kudisco maana yake nini?

mwasambili

Senior Member
Oct 28, 2013
151
77
Heshima kwenu wanajamvi, mara nyingi humu jukwaani tumesikia udsm wanachukua wanafunzi wenye viwango vizuri vya ufauru kidato cha sita lakini je inakuwaje hao hao wanafunzi wanadisco?

HIZI NI SABAU ZANGU TOA NA WEWE ZA KWAKO
1.inawezekana walichukua vilaza walio faulu (najua hapa itakuwa kazi kueleweka nina maana kwamba walifauru kwa njia zisizo halali au pengine ni alifaulu kwa bahati mbaya(alibahatisha kidato cha sita).

2.inawezekana wanapewa mitihani si kwa ajili ya kupima uwezo ila ni kwa ajili ya kukomoana (wakizani wanafunzi wengi kufeli sana ndio umakini wa chuo).

3.Hila za waalimu (kutokana na ugomvi unaoweza kutokea baina ya waalimu na wanafunzi)

4.inawezekana hawafundishwi vizuri na hivyo kusababisha kufeli(maprofesa wengi ni wazee hivyo wanachoka)

5.wameathiri wanafunzi kisaikolojia hivyo kuona elimu yao ni ngumu na kusoma ni mateso hivyo kuongeza hofu na kuwa na hamu ya kufaulu na sio kuelewa somo hivyo inawalazimu muda mwingine kukariri

6.wanafunzi wameendekeza mambo yasiyo ya muhimu chuoni..mfano starehe

7.wanazani ili mwalimu aonekane mahiri basi lazima akamate wanafunzi wengi

MY TAKE
chuo cha udsm sio chuo kizuri kusoma kwa sasa hasa kwa madogo wanaotegemea kujiunga mwakani kwa sababu
*hiki chuo kinaweza kukupotezea muda yaani unaweza ukasoma mpaka mwaka wa tatu alafu ukarudishwa nyumbani bila hata cheti na hivyo kukukatisha tamaa zaidi ya kuendelea kielimu
*Nawashauri wabadilishe hii kanuni ya kuanza upya masomo unapodisco badala yake iwe ni kupumzika nyumbani mwaka mmoja na akirudi mwanafunzi aendelee pale alipoishia(HII INATUMIKA ST JOSEPH UNIVERSITY IN TANZANIA)
*wanafunzi jengeni mahusiano mazuri na waalimu wenu maana inaonekana hatima yenu haiko uwezo wenu darasani bali ni mahusiano mazuri kati ya mwalimu na mwananafunzi
 
Hujawahi kusikia au kuona mtu anafaulu O, level vizuri sana ila anakuja kufail A, level
 
Andika vizuri,,,my take UDSM bado ni chuo kizuri ila most us we think that university is a place of kula bata that's why guys wanadisco
 
ukiweza kuvumilia mauzi jinsi ya mwezako asiyekupendeza utakuwa ni msomi uliyeelimika,,,hata kama nimekosea uhandishi naamini hoja imeeleweka
 
yote aliyoyasema yamekuwa yakizungumzwa sana na wana ud. Elimu haipimwi kwa ugumu bali output.

Inakatisha tamaa mtoto wa maskini ana disco afu wengine wanachekelea kwa ku fail kwake. Nchi za wenzetu hawapendi mtu a fail tofauti na sisi tunaona ufahari. Na sio kila anaye shindwa mtihani ni kilaza huwa kuna sababu nyingiiii nyingine zimetengenezwa na mwanafunzi mwenyewe na nyengine mazingira hata watu wengine pia wamechangia.

Tunapaswa kubadisha mitazamo yetu. Elimu si ugumu hapa taifa lilipo lina wakurugenzi makatibu na watendaji wengi waliohitimu udsm lakini output haifanani na sifa za chuo ni lazima tujiulize julipojikwaa
 
kwa ujumla tanzania hamna chuo cha maana ila ni umaskini tu ndio maana wenye pesa zao wanakwenda huko kwenye vyuo vilivyokamilika, hata huyo anaefundisha utaona anaona ufahari kwa kuelezea alisoma mfano masters yake katika chuo fulani cha maana huko nje, elimu inaanza na mazingila na mazingira ya kusomea je kwa tanzania kuna chuo gani kina mazingira mazuri ya kusomea? lecture maisha magumu mshahara mdogo muda wote anatamani labda akajaribu kugombea ubunge aboreshe maisha yake, mwanafunzi ajapata mkopo na kama kapata hautosherezi, chuo chenyewe hakina facilities mwanafunzi hana mahali pa kulala analala kilometre kumi huko mtaani na usafiri ni wa shida, basi ni kama fujo tu ilimradi tu
 
Starehe na new life styles tamaa zinawabadili hawa wasomi wa form six kutoka dividion one hadi division five
 
njoon tumaini iringa msuli kama o level vile yaan kukomaa mwanzo mwisho wakati huko UDSM 41 ume faulu huku iringa unalamba SUPP nzuri tu tembeen muone sio mnaongea tu
 
Elimu haipimwi kwa ugumu bali output. Inakatisha tamaa mtoto wa maskini ana disco afu wengine wanachekelea kwa ku fail kwake. Nchi za wenzetu hawapendi mtu a fail tofauti na sisi tunaona ufahari.

kukusaidia tu...hapo kwenye red...elimu haipimwi na output bali katika outcome... tuna output nyingi sana lakini perfomance zao ni za ajabu hasa makazini...mfano vilaza wa Mulugo.
 
ina maana wanafunzi wanaodisko huwa ni wanaosoma UDSM peke yake? mbona hata vyuo vingine wanadisko tu km kawaida? tuache lawama jamani, km ni wanafunzi someni kwa bidii, heshimuni kila mtu na mtaona mafanikio yake. Hata mie nimesoma hapo UDSM na sikupata tabu yeyote kwa kuwa nilikuwa najua kilichonipeleka pale ni elimu na sio kula bata km waonavyo wengine. Na mtu usiwe unaponda tu chuo kisa labda UNATAMANI ila HUKUFANIKIWA kwenda kupata elimu yako kupitia chuo Fulani...hapo ndio utakuwa mtu anaishia kuponda chuo husika na kutafitiza sababu...achene hizo bwana...UDSM mie ninakiheshimu sana!
 
HABARI WADAU
Naombeni kujua kuhusu SELFORM (O'LEVEL)

je, kwa hawa wanafunzi WALIOPO NYUMBANI Kwamba wanaweza kujaza wenyewe au lazima warudi tena shuleni walikosoma?

MANAKE WENGI WAKO MBALI MNO KWASASA NA SHULE.
.ASANTE
 
HABARI WADAU
Naombeni kujua kuhusu SELFORM (O'LEVEL)

je, kwa hawa wanafunzi WALIOPO NYUMBANI Kwamba wanaweza kujaza wenyewe au lazima warudi tena shuleni walikosoma?

MANAKE WENGI WAKO MBALI MNO KWASASA NA SHULE.
.ASANTE


SUKAH...
 
Back
Top Bottom