Je ualimu ni fani muhimu kuliko zote?

hilbajojo2009

Member
May 25, 2009
46
1
Siku za karibuni tumeshuhudia matokeo mabovu katika ngazi mbalimbali za elimu, kidato cha nne, sita na kidato cha pili. Pia matokeo ya mtihani wa darasa la saba hayaridhishi. Pia tumeshuhudia vijana wengi wanaohitimu elimu katika ngazi mbalimbali wakikosa ajira. Wahitimu pia wameshindwa kujiajiri. Wasomi waliobahataika kupata ajira katika sekta binafsi au serikali hawajasidia kiasi cha kutosha katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.

wasomi wameshindwa kuleta ugunduzi wa kweli, badala yake wameishia kupata shahada mbalimbali ambazo ugunduzi wake ni wa makaratasi tu.

Je hali hii inasababishwa na uhaba wa walimu nchini? au mfumo mbovu wa elimu. Unafikiri elimu yetu inaweza kuwa bora bila kuwa na walimu bora?

UPE ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa elimu Tanzania. Kuna ulazima serilaki yetu ifutilie mbali waalimu wa UPE na pia iifanya kazi ya ualimu kuwa ni ya maana!
 
Kila fani ni muhimu. Kuna muda hata u-housegirl utauona muhimu, hasa pale utakapokuwa umebanwa wewe na mwenzio, mna watoto na majukumu kibao, halafu housegirl kakimbia...
Wakili (advocate/lawyer) akiamua kuchemsha makusudi unaweza ukaishia lupango hivi hivi. Watu wa sector ya afya nao wakiamua kuchemsha, maisha ya wengi yatapotea. Kila fani ni muhimu. Ila kila mtu anahitajika kuifanya fani/kazi yake kwa moyo na nguvu zake zote ili asisababishe madhara kwa wengine.
 
Siku za karibuni tumeshuhudia matokeo mabovu katika ngazi mbalimbali za elimu, kidato cha nne, sita na kidato cha pili. Pia matokeo ya mtihani wa darasa la saba hayaridhishi. Pia tumeshuhudia vijana wengi wanaohitimu elimu katika ngazi mbalimbali wakikosa ajira. Wahitimu pia wameshindwa kujiajiri. Wasomi waliobahataika kupata ajira katika sekta binafsi au serikali hawajasidia kiasi cha kutosha katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.

wasomi wameshindwa kuleta ugunduzi wa kweli, badala yake wameishia kupata shahada mbalimbali ambazo ugunduzi wake ni wa makaratasi tu.

Je hali hii inasababishwa na uhaba wa walimu nchini? au mfumo mbovu wa elimu. Unafikiri elimu yetu inaweza kuwa bora bila kuwa na walimu bora?
KINACHOSABABISHA.........
1. Madai ya walimu.........malimbikizo ya nyongeza ya mshahara, nauli, kupanda madaraja.

2. shule moja wanafunzi wengi walimu wachache e.g NYANGAMALA PRIMARY SCHOOL IN LINDI REGION..........INA WANAFUNZI 800......WALIMU 3..... NI MIUJIZA TUUU INAHITAJIKA KUFAULISHA ANGALAU MWANAFUNZI MMOJA..............

3. MAZINGIRA YA SHULE.............. unampeleka mwalimu akafundishe shule ya msingi mchoteka kule tunduru halafu mshahara wake akaufuate songea.......... are you serious....??? just mfano......... but we have this situation in this country.

4. MWALIMU ANATUMIA ALMOST NUSU YA MSHAHARA WAKE KUFUATILIA MSHAHARA WA MWEZI UNAOFUATA......WHAT DO YOU EXPECT.............

5. USAFIRI WA KUTOKA KULE LITUMBA KUHAMBA HADI MBINGA NI MASHAKA MATUPU......... MPAKA LIJE GARI LA HOSPITALI KWENYE ZAHANATI YA KIJIJI AU LA PAROKO................. UNATEGEMEA NINI HAPO......????

6. WAZILI WA ELIMU SIJUI KAMA ANAZIJUA SHULE ZOTE ZILIZOPO TZ. .......... HII HAIWAPI MOYO WALIMU.

7. WENGINE MISHAHARA MPAKA TEREHE 39.................

8. WENGINE UTASIKIA MWEZI HUU KOMPYUTA IMEKURUKA.............. HIVYO SUBIRI MWEZI UJAO............. NA IKIKURUKA TENA NDO WAFWA...............

9......ETC
 
Back
Top Bottom