Je, Tunaweza kuwasiliana na wafu?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
JE, TUNAWEZA KUWASILIANA NA WAFU?

Mbona watu huenda huko na kulala?
Mbona watu huenda makaburini kufanya ibada?

Je ulishawahi kujiuliza haya maswali ?
Somo hili ni muhimu kwa sababu kuna tatizo kubwa kubwa sana na la muda mrefu. Tangu enzi za mababu zetu watu wameendelea kutambika na kufanya maombi kwa wafu waliozikwa siku nyingi. Kuna maswali mengi yasiyokuwa na majibu juu ya hiki wanachokifanya:
1. Je, watu hawa wanadhani kuwa huyo aliyezikwa bado angali hai?
2. Je, kama ni roho yake ndiyo ingali hai na inaweza kuwasikia, kwani roho ya mtu huyo iko eneo la kaburi lake? Mbona wanadai kuwa mtu anapokufa roho yake inalazwa mahali pema peponi? inakuwaje sasa waende kuongea nayo au kuiomba kaburini?

Sikiliza nikwambie: Kuna mambo machache ambayo ni muhimu kujua juu ya imani hii.

1. Umizimu: watu huendelea kuishi baada ya kifo
Tangu zamani za kale mababu zetu waliamini kuwa mtu akifa bado anakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa na kuamua mstakabari wa familia yake. Imani hii ndiyo iliyowasukuma kwenda mara kwa mara makaburini kutoa kafara. Familia ilipopata msukosuko wa majanga kama vifo, magonjwa, njaa n.k walikwenda makaburini kuwaomba mababu zao waliokufa wakiamini kuwa watawaondolea majanga hayo. Hiyo ni imani ya umizimu.

Mwandishi maarufu aitwaye J. Arthur Hill katika kitabu chake kiitwacho Spiritism: history, phenomena and doctrine. uk 25; anasema:
“Msingi muhimu wa ibada ya mizimu ni kwamba watu huendelea kuishi baada ya mwili kufa, na kwamba mara kwa mara, katika hali ambayo haijaeleweka, tunaweza kuwasiliana na wale waliotutangalia”

Kimsingi imani hii haitofautiani na imani kuwa mtu akifa roho yake inakwenda peponi! kuwa mtu akifa "ametangulia mbele za haki"! Hawa wote wanaamini fundisho hilo hilo moja, fundisho lile lile lililotolewa katika bustani ya Edeni kuwa “hakika hamtakufa.” Je, ni watu wengi kiasi gani wameanguka katika hili?

2. Kuomba udongo: kuomba wafu na kutambika
Kwa sababu roho haina mifumo ya fahamu, na kwa kuwa mtu akifa mifumo yake yote huoza na kuwa udongo, tunaweza kusema kwa hakika kuwa kwenda makaburini kuomba mtu aliyekufa ili akuombee kwa Mungu na kutambika ni sawa na kuuomba udongo ukuombee au ukusaidie katika matatizo yako! Mtu anaweza akaamini sana lakini kwa hakika udongo huo hautamsaidia kwa lo lote. Hakuna mwongozo kama huu katika maandiko.

3. Mungu: “Marufuku Kuomba Wafu”
Maandiko yanasema kuwa ni jambo baya sana mbele za Mungu kuomba wafu wakuombee. Ni machukizo. Maandiko yanasema dhambi hii ni sawa na dhambi ya uchawi, ni imani za mashetani na Mungu amepiga Marufuku kufanya hivyo.
Katika Kumbukumbu 18:10-12 imeandikwa:
“Asionekane kwako …msihiri, …wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana …” Hebu nikuulize; kwa nini Mungu anajumuisha pamoja kuomba wafu na usihiri na uchawi? Sikiliza nikwambie: Yeye Mungu anajua bayana kuwa kuomba wafu ni imani ya umizimu, na umizimu ni ushetani kama ilivyo uchawi na usihiri. Je, ni wangapi tumeanguka katika dhambi hii??

4. Mizuka: Kutokewa na Wafu
Maandiko yanasema kuwa mtu akifa hawezi kurudi tena akaonekana kwa watu.
Ayubu 7:9: “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa”
Ayubu 16:22: “Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.” Ayubu 14:14: “Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena?”

Kuna visa vingi sana vya watu waliokufa, kwa hali isiyokuwa ya kawaida, walikuja nyumbani mwao baada ya kufa na kuwasemesha ndugu zao na mara kutoweka!! Sikiliza ujue tangu sasa: Biblia inasema mizimu hii inayowatokea watu baada ya kifo ni roho ya mashetani. Haijalishi mtu anatokewa na mzimu katika sura ya mtakatifu gani!! Maandiko yanasema: “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, …” Ufunuo 16:14.
Tena maandiko yanasema: “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru” 2 Wakorintho 11:14

5. MWISHO
Kulingana na maandiko tunaweza kusema pasi na shaka kuwa kuomba na kuombea wafu, kutambika, kutokewa na waliokufa (mizuka) yote msingi wake ni imani kuwa mtu anaendela kuishi baada ya kufa. Kulingana na maandiko haya tuliyoyatafakari imani hii ni ya umizimu na ni chukizo kwa Mungu.
 
Mtu akifa ni mwisho wa kila kitu chake.Kitakachomsaidia ni yale mazuri aliyoyafanya duniani ambayo ameyaacha na yanaendelea kusaidia jamii kwa ujumla.Kumuomba aliyekufa ni wenda wazimu...yeye hata kusimama au kutembea hawezi hapo kweli anaweza kukusaidia...???
 
ni ujinga kumuomba mfu yeyote akusaidie wakati yupo aliyeshinda kifo na mauti Yesu Kristo
 
Kuna wakati mzazi wako anaweza kukutokea kwenye ndoto akakupa maelekezo kwenye jambo zito unalokosa ufumbuzi
 
Ukimshika MUNGU kwa imani ile ya kuhamisha milima,hutaenda kuwaomba wafu makaburini wala kutwa kucha kutafuta watumishi wakuombee.unaweza tiisha kila linalokuhusu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom