Je,tunampenda dr.mwakyembe kweli? Au mafisadi wameturoga?

greenstar

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
390
53
Inasikitisha kuona Jeshi la POLISI linatoa taarifa za uongo makusudi ili kuangalia Watanzania watasema nini,haya masuala ya kuongozwa na mafisadi kuangamiza watu kwa kutumia vyombo vya USALAMA ni hatari sana.Nilitarajia uongo utasukwa kuzima moto wa Mh.SITA ili tuamini ni muongo kama wanavyo jaribu kupindua RICHMOND kuwa ni uongo na kuteka watu wawasafishe kwa gharama yoyote...NCHI imefika pabaya sana,si muda mrefu tutaanza kufanyiwa unyama kama watumwa.Tanzama hata kupanda DALADALA ni ubabe hata kama unapesa zako,vitu vinapanda bei kila siku,Wametengeneza MGOMO wa madaktari na bado wanaanda machafuko zaidi ili kufanya maangamizi kwa watu wanaowapinga...ARUSHA ni mfano tu,MBEYA na MWANZA zipo kwenye TARGET.DSM wanaogopa kwa vile ndipo wanapotegemea kuishi na kuratibu UMAFIA pia wanavitega UCHUMI vingi zaidi.

Narudia tena DR.Mwakyembe walimemtegeshea SUMU na wahusika ni wanausalama....Hivyo basi Siyo RAHISI kwa JESHI la POLISI kujichongea kwa wananchi ili kulinda IMANI juu ya CHOMBO hiki. RAI yangu kwa RAIS, kama ni kweli unampenda DR.MWAKYEMBE na Mh.SITA naomba uingilie kati hili suala haraka sana kabla nchi hajachafuka.I swear to my ALMIGHTY ,hawa watu watafikishwa ICC na tutawafilisi mali zao pindi tukichukua DOLA iwe kwa KURA au MAPINDUZI..........
 
watu wameweka pesa na matumbo mbele..sasa kama hadi dol inanunuliwa wewe unategemea nini....
 
Sisi tunategemea nguvu ya Mungu naamini Mungu hawezi kutuacha tuangamie, wao watatumia nguvu ya pesa sisi tutatumia nguvu ya Mungu, tunakuomba ee Mungu wetu utjalie nguvu ya kupambana mpaka mwisho kama mwanao wa pekee alivyoteswa na kufufuka akashinda mauti naamini na sisi kwa imani ya hii ya bwana wetu Yesu Kristo utuongoze tushinde. Tunakuomba umjalie afya njema Dr mwakyembe na wezake wapone ili afya zao zirudi tuendelee kutukuza utukufu wako. Amen
 
Aliwahujumu mamilioni ya WATANZANIA kwa kuficha ukweli katika ripoti ya RICHMOND ili kuwalinda mafisadi wachache; sasa Mungu huyo huyo mnaemuomba amponye ndio anayemuadhibu kwa unafiki wake!! Mungu mara zote yuko upande wa wengi na ndio maana inasemekana kuwa SAUTI YA WENGI NDIO SAUTI YA MUNGU!!
 
Aliwahujumu mamilioni ya WATANZANIA kwa kuficha ukweli katika ripoti ya RICHMOND ili kuwalinda mafisadi wachache; sasa Mungu huyo huyo mnaemuomba amponye ndio anayemuadhibu kwa unafiki wake!! Mungu mara zote yuko upande wa wengi na ndio maana inasemekana kuwa SAUTI YA WENGI NDIO SAUTI YA MUNGU!!
kWa sasa anapougua si jambo jema kumsemea maneno ya kashfa!
 
Mungu yupo nasi daima,naamini Dr.Mwakyembe atapona na MUNGU atawapiga MAFISADI kwa UPANGA wa MOTO......DCI Manumba ajiuzulu haraka sana kwa vile yeye si mzalendo kwa kuwatumikia MAFISADI...Tunataka TANZANIA mpya izaliwe ili MUNGU azidi kuibariki.
 
Back
Top Bottom