Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Kuna mambo mengi ya msingi na kero nyingi sana za kujadili/kufanyana juu ya taifa hili, sio huo upupu wa vazi la taifa.

Hizo kamati ni kupeana kula tu.
 
ndo maana nimesisitiza kamati izunguke na kutafiti..watakuja na kitu.
Haina haja ya kuwa sceptical,eti uhakika utaalamu wa Wahaya bado upo ama la.. Halafu sikusema litatofautiana kulingana na hadhi ya mtu,someni vyema.. Au kaulize kwa Mnigeria yeyote gharama ya nguo yao ya kitaifa,amu mhindi yeyote muulize Sari hata huko kwao India inauzwaje,kaulize utasikia.. Halafu watu wanadhani ni kama nguo ya kuvaliwa ukienda sokoni au shopping,ni nguo ya heshima sana. Huenda ukaivaa mara moja katika miezi hata sita. Zaidi ni kwamba wataboresha ujuzi watakaojifunza wa njia za asili za kupata vitambaa hivyo.. Na wewe unashauri njia ya ujumbe kupiga kura,sidhani kama ni lazima,labda kama watashindwa kuja na kitambaa ama mshono wa aina moja.

mkuu ata hivyo nimekuelewa..
 
kukubalika kwa vazi la taifa na kwenyewe ni shughuli tofauti na kuchagua! nadhani kwa sasa tukubali uhalisia wa mchakato huu - maana ulikuwa wazi kwa kitambo

uwazi huo unaodai ulikuwepo toka kitambo siuoni ndugu..au umeendeshwa kama ule wa vitambulisho vya taifa..?
 
Unajua bwana naipenda sana nchi yangu manake imekaa kikomed komed hivi huwa inanipa burudani kwa vituko. Haiishi vituko. Yaani nchi ina akili kama za sekondari tena form tu. AAAA Tanzania, Mambo yanayohusisha tuvikao na tukamati we are very good, eti kamati ya vazi la taifa. Kama tunataka kujulikana kuna vitu vingi vya kututangaza tumeviharibu sasa tunaibuka na vituko. Mfano, MICHEZO, TANZANITE, ML.KILIMANJARO, MBUGA ZA WANYAMA, MADINI, NK. Acheni usanii. Huo ni ulaji mwingine.

lakini hizi kamati za kipindi hiki hakuteua mkuu...
 
uwazi huo unaodai ulikuwepo toka kitambo siuoni ndugu..au umeendeshwa kama ule wa vitambulisho vya taifa..?
ulianza toka mwaka juzi kama siokosei, kulikuwa na shindano la wazi la mitindo/mavazi - hakikupatikana kitu kipindi kile. Ndio wanaendelea nadhani
 
1. Swala zima la vazi la taifa kupangwa kwa kamati lina matatizo. Vazi la taifa litatoka kwa watu.

2. Serikali inaweza kuchangia kwa kuweka mazingira ambayo yanaweza kustawisha kuwepo kwa vazi la taifa. Kwa mfano, kwa kufufua sekta ya viwanda vya nguo nchini, na kuacha designers wenyewe washindane, vazi litakalopendwa na wengi kama lina muonekano wa kitaifa automatically litakuwa la taifa. Hatukuwa na kamati ya kupanga wanawake wavae khanga au vitenge, ni vitu vinavyotokea organic tu. Huwezi kupanga mipango miingi ya vazi la taifa wakati huna hata viwanda vidogo vidogo tu vya nguo, achilia mbali textile mills.

ndugu kiranga hadi sasa mchakato umeshaanza na ngumu kuapply huo utaratibu uliousema..kusema kwamba wafungue/ kwanza textile industries ni ngumu au haiwezekani kabisa..usishangae kusikia vazi la taifa ni suti za kiitaliano kwa viongozi wa nchi pamoja na wafanyabiashara mashuhuri na kanga za india kwa akina mama wa uswahilini kama anavyopendekeza dada FAIZAFOXY.
 
mwanzoni walikuja na 'vazi la Taifa' wakashindwa vibaya vibaya. Sasa tena wamekuja na ''vazi la Taifa' ila siku zinavyosogea wanabadili utaratibu. Sasa jana nimesikia wakiwa clouds wanasema wanaandaa mchakato wa kitambaa kitakachokuwa utambulisho wa utaifa wetu. Kwamba mtu atashona staili anayotaka. Sasa nauliza hilo ni vazi au kitambaa cha Taifa?
 
Vazi la Taifa ni National Identity kama ilivyo kwa bendera, sarafu n.k. Ni jambo zuri linalo ainisha utaifa wetu, tafadhali msibeze tu angalia na kwa jicho la tatu.
 
Mimi binafsi sihitaji kwani suruali na shati la mikono mirefu vinanipendeza tu. Mi nahitaji vitu na fedha walivyo tufisadi virudishwe na mikataba feki ivunjwe, hivi vikifanywa utaifa wetu utarudi. Je hilo vazi litafunika umaskini? Tena watakao vaa huko ughaibuni watajitakia aibu ya bure, kwani watakua wanakunyoshea kidole na kusema ombaomba yule amekuja kutembeza bakuli.
 
Vazi la Taifa ni kanzu na kofia kwa wanaume, wanaotaka kulibadili hili wana agenda za siri na kwa kina mama Khanga mbili nje ndani chochote.

Teh teh teh teh teh! Haswa umenena. Wanaotaka kulibadili ni serikali ya CCM na tumestukia ajenda zao za siri. Halafu hapo kwenye "... ndani chochote" mh! Yaani unamaanisha hata yale masarawali magumu ya kimerikani almaarufu kama "jeans" ambayo baadhi ya mashule yameamua kuya-adopt kama mavazi rasmi ya ndani ya mabinti zetu?
 
Ingawa ni kweli kwamba linaweza kuleta utambulisho wa Taifa, lakini tuna mambo mengi magumu kuliko hilo vazi. Kwani kuna Mtanzania anayetembea bila nguo kwa kuwa hakuna vazi la Taifa? Tupambane na gharama za umeme kwanza.
 
vazi la taifa ni utamaduni wa watu, huwezi kulipgia kura kwa kamati kama hii ya walaji. Vazi la taifa hujitokeza lenyewe tu kwa mtu fulani anayewavutia watu wengi hasa kiongozi mkuu akija na vazi la aina yake watu hulipenda na kuanza kuiga na mwisho kila mtu hulipenda.
Mimi naamini vazi la taifa letu litaletwa na kiongozi mzalendo atakayependwa na watanzania na wataamua kuiga mavazi yake na hilo ndo litakuwa Vazi la kitaifa.

Mimi naamini magwandaa ya chadema ndiyo yatakuja kuwa mavazi ya taifa kwa kila mtu kuanza kuyashona kwa mtindo wake.

Chadema wakikaa vizuri na kiongozi wa chadema akaamua kutumia mavazi haya kwa kuyabadilisha kidogo yakawa unique basi tutakuwa na vazi la kitaifa la gwanda. Hatuna sababu ya kukimbilia suti ili hali sisi ni masikini wa kutupwa. Kitambaa cha gwanda la chadema ni nafuu kwa kila mtu ili mradi ukishone kwa manjonjo yako. Tunakumbuka jinsi Halima Mdee alivyotoka bomba bunge lililopita.

Acha ccm watafute vazi lao kwa ulaji lakini cdm wakichukua nchi vzai la CDM ndo litakuwa vazi la taifa maana limetokea tu kama utamaduni wa chadema.
 
Ha2liitaji because ukifuatilia juhusu hii ishu ni uchakachuz mtupu kwa sababu ishu hii ilianza 2004 mpaka leo ni upoevu wahela. Za taifa nthng mre kwanza hamna m2 atalivaa!
 
hivi tunaitaji vazi la taifa na hoja ni kitambaa au vazi la taifa vinafanana? Mods mbona mnakua wavivu kiasi hiki!!??? Hizi ni thread mbili zenye jumbe tofauti..na kuziunganisha ni jambo la ajabu sana,kwanza uelekeo wa mada umepotea ni mambo ya ajabu sana haya mnatufanyia!!!
 
How about some sort of local-made Kilts for men ili tupate na hewa kidogo kuna joto sana..
 
Vazi la Taifa ni National Identity kama ilivyo kwa bendera, sarafu n.k. Ni jambo zuri linalo ainisha utaifa wetu, tafadhali msibeze tu angalia na kwa jicho la tatu.

ILI ITUSAIDIE NINI
HIYO VAZI YA TAIFA?
ukija cheki hesabu ya
huu upumbav utalia
mchozi,

nonsense
 
Back
Top Bottom