Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Source,Habari Leo!!!!
Tanzania yaishukuru Libya kwa Msaada
TANZANIA imeishukuru Libya kwa misaada yake ya kibinadamu ambayo imetoa kwa Tanzania kusaidia watu walioathiriwa na athari za mvua na mafuriko ya hivi karibuni katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.
Shukurani hizo zimetolewa usiku wa kuamkia jana na Rais Jakaya Kikwete katika mazungumzo yake na Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi mjini Sirte, Libya.
Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Sirte kwa mazungumzo na Kanali Gaddafi akiwa njiani kwenda Davos, Uswisi kuhudhuria Mkutano wa 40 wa Taasisi ya Uchumi Duniani ya World Economic Forum unaoanza leo ukishirikisha viongozi kutoka nchi zaidi ya 30 duniani.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete alimwambia Kanali Gaddafi: Nakushukuru sana kwa misaada yako ya kibinadamu ambayo Serikali yako imeipatia nchi yangu kufuatia mafuriko na athari nyingine zilizosababishwa na mvua katika Tanzania. Rais Kikwete alimwambia Kanali Gaddafi kuwa familia zipatazo 26,000 zilikuwa hazina mahali pa kukaa baada ya nyumba zao kubomolewa katika mafuriko hayo na kuwa zilikuwa zinaishi katika kambi za muda.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ni wilaya za Mpwapwa katika Mkoa wa Dodoma na hasa Wilaya ya Kilosa katika Mkoa wa Morogoro, ambayo imebeba athari kubwa zaidi za mafuriko hayo kutokana na mvua zilizonyesha kuanzia wiki ya mwisho ya Desemba, mwaka jana, hadi wiki ya kwanza ya Januari, mwaka huu.
Tunakushukuru kwa mahema, kwa dawa, na kwa misaada mingine ambayo imetoa mchango mkubwa na kuleta tofauti kubwa katika maisha ya watu wetu walioathiriwa na mafuriko hayo.
Tulikuwa na ukame wa miaka miwili mfululizo, na mvua zilipoamua kunyesha zikaja wa hasira kubwa, Rais Kikwete alimwambia kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Rais alisema mafuriko hayo yaliyotokana na mito miwili, ukiwamo Mto Mkondoa kuacha njia za asili na kubomoa kingo, yameharibu mno miundombinu ya barabara na reli kiasi kwamba Serikali ya Tanzania inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 15 (zaidi ya Sh bilioni 15) kukarabati miundombinu hiyo.
Ni hasara kubwa kwetu. Kiasi cha dola za Marekani milioni 15 ni nyingi kwa nchi masikini kama Tanzania lakini tumeamua kuwa ukarabati huo utakuwa umekamilika katika muda mfupi.
Jumatatu wiki hii mjini Dar es Salaam, Rais Kikwete aliitisha mkutano maalumu wa viongozi na wataalamu wa Wizara ya Miundombinu, taasisi na kampuni zilizoko chini ya wizara hiyo, kujadili hali ya uharibifu kwenye miundombinu hiyo, na hatua za haraka kukarabati miundombinu hiyo.
Rais Kikwete alisimama Libya na kushauriana na Kanali Gaddafi kuhusu masuala kadhaa yanayohusu AU na mkutano wa wiki ijayo wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia. Gaddafi ni Mwenyekiti wa AU anayemaliza muda wake baada ya kumpokea uenyekiti Rais Kikwete mwaka jana.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amesema Tanzania haina nia ya kuwania moja ya nafasi mbili za kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), na badala yake, itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki ya Afrika kupata nafasi mbili za kudumu katika Baraza hilo.
Aidha, imesisitiza kuwa iko tayari kuunga mkono nchi nyingine za Afrika zilizoonesha nia ya kuwania nafasi hizo iwapo suala hilo litakubaliwa chini ya mageuzi makubwa yanayojadiliwa ili yafanyike ndani ya Umoja huo.
My take! Ingekua jambo la Busara sana kama Tanzania ingeingia katika kinyang'anyiro cha nafasi ya uwakilishi kwenye baraza la usalama la UN.Tunayo Cv ya kutosha kabisa...Sasa Jk anasema hatuhitaji hiyo nafasi and yet tuli-risk watanzania wenzetu ku-command huko comoro,kukomboa mataifa ya kusini mwa Afrika nk.hatujawahi kupata malipo.Kuna haja ya kujadili hili suala huku nyumbani,ikiwezekana Tanzania iwanie kiti katika UN security Council
Tutaweza kurudisha anagalao kiasi cha gharama zote za kiuchumi,kijamii na kisiasa ambazo Tanzania ilibeba tangu tupate uhuru hadi sasa.
Viongozi wetu kwa kweli wanatia shaka sana degree ya uzalendo wao.