Je, Tanzania bado ni nchi ya Amani?

kwenye dhiki na njaa kunakuwa na nidhamu ya woga. hakuna amani wala mshikamano
 
toa amani ndio utajua hata wale wenye uwezo wa kusaidia nyumbani kutoa mlo tu, sasa wananyaganywa barabarani mikate yao. Usicheze na Amini.

Usililie matatizo ambayo hayaja kukuta, waulize waliopetaza mzazi aliekua akitoa mlo alivyotoka ilikuaje. Waulize wenye njaa tukitoa amani itakuaje.

Sio kila mtu anaamkia mkate na siagi asubuhi, wengine uji miaka yote toka nyerere mpaka leo toafauti ya uongozi amna tofauti ya maendeleo. Sasa msiwapoteze kitu peke wanachokijua kisa we mkate wako umekosa siagi.

Do people really understand our society or just selfish motives guide us.
 
Ndiyo maana watu hawajiandikishi kupiga kura, wamekata tamaa, hivyo kuendelea kuwa Watawaliwa na Wanyonge!
 
Ndiyo maana watu hawajiandikishi kupiga kura, wamekata tamaa, hivyo kuendelea kuwa Watawaliwa na Wanyonge!

Labda cha kujiuliza ni kwa nini watu wengi hawajiandikishi na hawajajiandikisha kwenye daftari??? Je ni ukosefu wa elimu ya uraia, uoga au hali ya kukata tamaa kwamba nikienda kupiga kura against haitaleta tofauti bila kujua kama watu 200 mkiwa na mtazamo huo basi wanampa mtu ushindi kiulaini
 
Penye Dhiki na Njaa; Amani Utulivo na Mshikamano vina manufaa gani?

Penye dhiki na njaa, by definition, hapana amani.

Kwa hiyo hii notion iliyoumba swali la "Penye dhiki na njaa Amani na Utulivu na mshikamano vina manufaa gani?" inabidi iwe re-examined.

Amani na utulivu ni pamoja na kutokuwa na njaa, ukishakuwa na njaa huna amani na utulivu.

Kwa hiyo hizi nyimbo za amani na utulivu tunazoimbiwa si za kweli.Kuna amani gani kwa watu wanaohemea maembe mabichi kwa kukosa chakula?. Unaweza kuniambia kuna complacency au hata debatable contentedness in some cases, lakini si amani.

Kuna amani gani kwa watu wanaokunywa maji ya tope na kupata magonjwa kwa sababu hamna maji safi.

Kwangu mimi amani inajumuisha kutokuwa na njaa na dhiki, bila hivi amani itakuwa ya kuchongwa tu.Tusiilimit amani kwenye sense ya "kutokuwepo kwa mapigano" tu, hii ni narrow thinking, sawa na kuona bombings ndizo terrorism wakati the real terror ya malaria inaua millions of people.
 
Tatizo kubwa kuliko yote ni pale hao walio katika dhiki na njaa hawajui kuwa wako kwenye hali hiyo kwa sababu ya viongozi.Ila wanaamini wako hivyo kwa sababu ya Mungu!

Pili ni pale walio katika hizo calamities wamezoea kama vile ni sehemu ya maisha yao, na kwa namna nyingine mtu kupata chakula ca mchana ni sherehe, kwao akipata milo mitatu kwa siku hata kama hakushiba anaamini serikali imemwezesha!
 
Penye dhiki na njaa, by definition, hapana amani.

Kwa hiyo hii notion iliyoumba swali la "Penye dhiki na njaa Amani na Utulivu na mshikamano vina manufaa gani?" inabidi iwe re-examined.

Amani na utulivu ni pamoja na kutokuwa na njaa, ukishakuwa na njaa huna amani na utulivu.

Kwa hiyo hizi nyimbo za amani na utulivu tunazoimbiwa si za kweli.Kuna amani gani kwa watu wanaohemea maembe mabichi kwa kukosa chakula?. Unaweza kuniambia kuna complacency au hata debatable contentedness in some cases, lakini si amani.

Kuna amani gani kwa watu wanaokunywa maji ya tope na kupata magonjwa kwa sababu hamna maji safi.

Kwangu mimi amani inajumuisha kutokuwa na njaa na dhiki, bila hivi amani itakuwa ya kuchongwa tu.Tusiilimit amani kwenye sense ya "kutokuwepo kwa mapigano" tu, hii ni narrow thinking, sawa na kuona bombings ndizo terrorism wakati the real terror ya malaria inaua millions of people.
Bluray,
Mkuu hoja yako ipo juu ya kiwango cha Ndivyo Tulivyo ktk kufikiri kwa hiyo ni lazima uchukulie hali halisi na jinsi Mdanganyika anavyofikiria. nadhani Rev anahoji zaidi ufinyu wa kufikiria hivyo kwani ndio maisha yetu yalivyo.. tumekubali ktk imani zetu kuwa Amani inayoishia kutokuwepo na mapigano..Ni sifa na mila ama desturi inayokubalik....Je, uzuri wake ni upi haswa!

Ni ukweli kwa mdanganyika yeyote kwamba Amani na utulivu unaishia kutokuwepo na mapigano, hayo ya njaa na afya za watu ni vitu vya kawaida kabisa katika maisha yetu.
Kisha hili neno Amani lina makubwa, Utawala wa Kiafrika ni sawa na mtu anayetafuta ugonvi... ata ku bully iwe shuleni au kazini ili mradi tu anatafuta wewe ufanye kosa la kumjibu vibaya au kutaka ugonvi..sasa hapo kuna mawili yawezekana wananchi hawataki ugonvi pamoja na kwamba wanaonewa lakini hawaoni faida ya kujitetea..Yawezekana pia woga wa kuingia ugonvi wakijua kwamba hawana ubavu wa kupigana kujitetea hivyo bora kukaa kando na kukubali kuonewa.

Ajabu ya mila na desturi ya Kidanganyika.. pengione yawezekana imetokana na mafundisho ya dini kwamba ukipigwa shavu moja geuka la pili akuwashe jingine. ndio imegeuza maonevu haya kuwa ni sifa kubwa! sifa ambayo tumeiona hata hapo JF na ktk familia zetu kwamba yule anayekataa ugonvi na kujibu Ewallah bwana ndiye muungwana na mtu bora kati ya watu hata kama anaungua rohoni.
Kwa kuepuka ugonvi basi huyo atasifika na kutuzwa AMANI na ajabu hata kama watu hao watavunja urafiki na hawataongea tena maishani, bado itasifika kitendo cha kutokuwepo Mapigano!
 
Penye dhiki na njaa, by definition, hapana amani.

Kwa hiyo hii notion iliyoumba swali la "Penye dhiki na njaa Amani na Utulivu na mshikamano vina manufaa gani?" inabidi iwe re-examined.

Amani na utulivu ni pamoja na kutokuwa na njaa, ukishakuwa na njaa huna amani na utulivu.

Kwa hiyo hizi nyimbo za amani na utulivu tunazoimbiwa si za kweli.Kuna amani gani kwa watu wanaohemea maembe mabichi kwa kukosa chakula?. Unaweza kuniambia kuna complacency au hata debatable contentedness in some cases, lakini si amani.

Kuna amani gani kwa watu wanaokunywa maji ya tope na kupata magonjwa kwa sababu hamna maji safi.

Kwangu mimi amani inajumuisha kutokuwa na njaa na dhiki, bila hivi amani itakuwa ya kuchongwa tu.Tusiilimit amani kwenye sense ya "kutokuwepo kwa mapigano" tu, hii ni narrow thinking, sawa na kuona bombings ndizo terrorism wakati the real terror ya malaria inaua millions of people.

tuna matatizo mengi solution ni kuyapunguza na si kuyaongeza poverty is poverty. amna anae-deny ya kwamba umaskini una ambatanisha na other social problems ambazo unazofikiri wewe zinatoa amani kwa watu wenye hali ngumu.

the idea is to tackle these problems one by one (something the government doesnt do), lakini si kuwaongezea watu other difficult circumstances to negotiate with just to provide for their families.
hivyo basi amani yako unayo i-define ni purely poverty lakini usicheze wala usifikiri biashara ya mtutu ni the same mjomba hiyo ni issue nyingine kabisa na ni matatizo makubwa mengine kabisa kwa nchi kama tanzania kujiinua tena kufika hapo tulipo ni miaka mia mingine.
 
Jamani nisaidieni, hivi kipimo cha amani na utulivu duniani au katika nchi fulani ni kitu/vitu gani hasa...????
 
Imeandikwa na Mwandishi Maalum,
Rome, Italia;
Tarehe: 18th November 2009

Habari Leo

RAIS Jakaya Kikwete amerudia kuvionya vyombo vya habari nchini visitumie uhuru wao kuvuruga amani na kuvunja umoja wa kitaifa.

Rais Kikwete amesema, endapo vitafanya hivyo Serikali haiwezi kuviacha,vitashughilikiwa.

Sanjari na onyo hilo, Rais Kikwete amesema, Serikali itaendelea kulea na kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.

Lakini Rais Kikwete amesema,vyombo vya habari lazima vijirekebishe,vitimize wajibu ambao ni sehemu muhimu ya uhuru huo wa habari.

“Kama nilivyowaambia pale Musoma majuzi wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, huu hauwezi kuwa uhuru wa kuvunja taifa, uhuru wa kugawa watu, uhuru wa kuchochea maasi na ugomvi kati ya dini mbalimbali, kati ya makabila, kati ya watu wenye rangi mbalimbali”

Alisema “Baadhi ya vyombo vyetu havina wajibu kabisa. Vinachochea maasi ya kuvunja nchi na kuleta mfarakano kati ya watu wetu. Vinajaribu kugawa watu wetu, kugawa mataifa yetu na kusababisha maafa makubwa. Hatuwezi kuvumilia vyombo vya habari vya namna hiyo vinavyotumia uhuru kuleta balaa kwa watu.”

Lini atamuonya papa fisadi Rostam ili aheshimu ripoti ya kamati ya Bunge na kuacha kuropokaropoka!?
 
Jk yuko Italy anakula kuku.Kama namtembelea rafiki yangu kila mara nyumbani kwake inabidi naye aje kwangu.Sijawahi kusikia PM wa Itally, Silvio anatembelea Tanzania.

Media ya TZ lazima iendelee kuandika kuhusu ufisadi!Sidhani kama waandishi wetu wanaadika kuhusu kupindua nchi!
 
Mimi nadhani hapa JK anakosea kitu kimoja. Watu wa kuwaonya ni viongozi wa serikali ambao kila siku hukimbilia vyombo vya habari kuzungumza ulevi wao kana kwamba pale ni mahala pa kuuzwa mchemsho..
Ni busara kwa JK kuwaonya viongozi wake kwanza kuheshimu wadhifa waliopewa na kutumia maneno ya busara wanapowakilisha hoja laa sivyo vyombo vya habari vitaendelea kuchimba zaidi kutafuta ukweli wa vita baina ya wahusika..ambao kwa bahati mbaya ni viongozi wetu na toka chama kimoja.
 
Anachokisema hapa JK ni kuhusu upotoshaji wa makusudi kwa lengo la kutishia au kuvuruga amani.
Juzi nilienda Pemba, Wapemba wamesusia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura, nilipoingia mitaani na dodoso langu, baadhi wakaniamini, wakasema, hatujiandikishi na tumejipanga uchaguzi haufanyiki pemba, na wako tayari kufa kulinda uhuru wao.
Ningekuwa mwandishi nikaandika Pemba hakuna uchaguzi ni damu kumwagika, hata kama ni kweli, gazeti lingetoa hiyo, breki ya pili ni msalabani. Ndicho anachosema JK
 
Mkuu wangu pengine sikukuelewa lakini kama wewe ni mwandishi wa habari unatakiwa Uandike habari hiyo kwani sii uzushi..Upotoshaji ni pale unapoandika kitu ambacho hakipo kabisaaa, lakini kama kweli Wapemba wamekataa kujiandikisha wao na kuweka madai kwamba uchaguzi hautafanyika, Na wako tayari kufa... huo ndio ukweli tunaotaka kuusikia mapema kuliko kusubiri siku ya mwisho ya kufa kwao pasipo kuelewa haswa sababu ya mauaji hayo.
Damu haiwezi kumwagika ikiwa wananchi wamekataa kujiandikisha na itaeleweka mapema, hivyo utaratibu mwingine unaweza kutumika ikiwa ni pamoja na kutazama sababu zilizowafanya wafikie maamuzi hayo. Pengine yawezekana kabisa muafaka baina ya Maalim Seif na Karume kuwa ndio sababu kubwa. Hivyo, mapema inawezekana kurekebishika au vyama husika kutazama upya muafaka huo..Kwa ujumla makosa huanzia kwa viongozi wenyewe, magazeti ni upepo unaokoleza moto ulokwisha washwa na viongozi wetu.
 
Ndugu ya Mkandara, ukisikia watu wanasema Damu itamwagika Pemba 2010, kwa vile hii ni 2009, utaitwa Mchochezi.

Kwani Mwahalisi alifungiwa kwa kosa gani?, kisa kasema kuna mkakati wa kumtomteua JK kuwa Mgombea wa CCM, 2010. Kikatiba JK mwisho wake ni 2010 mpaka apate tena ridhaa ya chama chake, hata kama wanakajiutaratibu kao, hako ni kautaratibu tuu sio sheria wala kanuni, hivyo Mwanahalisi was just right, kilichomkuta tunakijua, huo ndio uhuru wa vyombo vya habari anaozungumzia JK.

Ila pia nakiri, suala la Mwanahalisi, wapambe wake ndio waliyafanya waliyoyawafa ili kuendelea kujikombakomba komba kwa JK.

Na la Pemba, ni kweli jamaa walijipanga kufanya kitu mbaya, thanks for the secret deal ya Seif na Karume, itaepusha yote, na mengine yatakayokuja na kutuacha bara midomo wazi.
 
Ole wenu wana jf mnaowachanganya akili wapiga kura!...........
 
Back
Top Bottom