Je smz inatekeleza ilani ipi?

Petiro

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
309
45
Kunapokua na muungano kati ya vyama vya kisiasa katika kuunda serikali ya pamoja huzingatia
sera(mrengo), katiba, falsafa,mitizamo na desturi za vyama hivyo katika kuendesha shughuli mbalimbali za kisiasa,
kijamii na kiuchumi.
Kabla ya uchaguzi mkuu vyama shiriki kutengeneza ilani zao za uchaguzi na ndio utakua mwongozo wao pindi
watakapo shinda na kuunda serikali. Na pale panapokua na serikali ya pamoja basi hujadili na kufanya marekebisho
ya ilani zao ili ziweze kuakisi ilani za vyama vyao kwa pamoja.


1. je katika serikali ya umoja ya SMZ wanatekeleza ilani ipi? ile ya CUF au ya CCM?
2. Je kama wanatekeleza ile ilani ya CCM(2010-2015) na ile ya CUF anaitekelezwa nani?
3.je serikali ya umoja inayolazimishwa na katiba ya dola/nchi (kama ile ya SMZ) na ile iliyofikiwa baada
ya mazungumzo ya hiari baina ya vyama husika(kama ile ya serikali ya shirikisho ya Ujerumani) ni ipi bora kwa mtizamo wao? na kwanini?


Mtizamo wangu mabadiliko ya katiba ya ZNZ ya kulazimisha kuundwa serikali ya pamoja ili hali itikati na falsafa za vyama
huweza kutofautiana ilikua wa "kisiasa uchwara". Hauna mashiko yoyote wala busara zaidi ya "funika kombe mwanahatamu apite"
na ulikua kwa manufaa kwa watu wachache zaidi ya waZNZ wote


Pindi ikitokea vyama zaidi ya CCM,CUF kujumuishwa kwenye kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa mujibu wa katiba, hakika
itatokea mgogoro na mivutano isiyopatwa kushuhudiwa ..
 
Hao CUF njaa tupu utafanyaje makubaliano na mpinzani wako ktk siasa wamejiua wenyewe si unaona. Hakuna urafiki kati ya Masikini na Tajiri au Bemki na Maskini
 
Back
Top Bottom