Je siasa za Tanzania zitamuokoa mwananchi wa hali ya chini? Je nini kifanyiike kuinusuru nchi yetu?

Nahory Mwendi

New Member
Mar 11, 2012
1
0
Nimekuwa nikiangalia mwenendo mzima wa siasa za hapa nyumbani, na kulinganisha na siasa za nje, kusema ukweli siasa za hapa nyumbani zinalenga masilahi binafsi na wala si masilahi ya Taifa. Inauma sana unapoona kiongozi mliemchagua huku mkiwa na imani kubwa kuwa atawaondolea kero mlizonazo, mwisho wa siku akipata uongozi hata kurudi kuja kuwashukuru kwa kumuweka madarakani anashindwa. Je hii ni haki kweli? Ni lini wanasiasa watamuokoa mwananchi wa hali ya chini? Nini kifanyike kuinusuru nchi yetu kwani inamegwa kila siku na hao ambao tuliwapa dhamana kutuletea maendeleo?​
 
siasa hizi bongo za akina kikwete hazina ukombozi wa ukweli wowote kwa tanzania ya leo hovyo kabisa. ukombozi huu ni wa akina ridhiwani na wadogo zake wanaomiliki mali nchi nzima. inaonekana baada ya bb yake kukamata nchi aliwaasa kuanza kusaka mali kwani familia yao ilikuwa maskini wengine mlie si lolote si lolote

Back
Top Bottom