Je sheria ya kumfanya Msajili wa Vyama kuwa na uamuzi wa Mwisho ni Halali? na ina nia

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,393
4,056
Wadau naomba tuangalie sheria ya kumrushusu Msajili wa Vyama kuwa ndio msemaji wa Mwisho kuhusu Usajili wa Vyama, kama ilivyo elezwa na Mwanakijiji katika thread ya CCJ yaandika barua kwa Mabalozi.
Sasa kwa uelewa wangu kitu chochote kinacho husu haki na sheria mwamuzi wa mwisho anatakiwa kuwa ni Mahakama ya Rufani.
Pili sheria inatakiwa kuangalia kwamba nia ya sheria ni nzuri au mbaya, yaani ipo pale kukuza ufanisi na demokrasia au ipo katika kudumaza Demokrasia na Ufanisi.
Tatu kitu chochote kile kinacho husu haki na utawala bora kinatakiwa kuwa na mfumo ambao unakuza uangalizi wa utendaji wa haki na ikikiukwa basi mkosa lazima aazibiwe ile asiwe na hisia ya kumtendea mtu kinyume cha sheria. (i.e check and balance) je sheria zetu za uchaguzi na za usajili ya vyama vina kidhi haja hizi au kuelekea huko?
 
Back
Top Bottom