Je sheria inasemaje kuhusu wakati gani madaktari wanaweza kugoma?

Teroburu

Member
Aug 6, 2009
41
3
Sheria ya Tanzania imeweka utaratibu wa kugoma katika Sheria za Kazi za Mwaka 2004.

Sheria za Tanzania pia zimeweka wazi utaratibu wa wafanyakazi wanaotoa huduma muhimu (Essential services) kama madaktari, waongozaji wa ndege wanaotaka kugoma.

Je utaratibu wa madaktari kugoma umefuatwa?

Kwa nini watanzania tumejenga tabia za kutumia siasa na malumbano ili kutatua maswala ambayo ni ya kimikataba wa kazi, kisheria…?

Kila daktari ana mkataba wake binafsi wa kazi. Kila daktari alipoajiriwa alisoma masharti yake ya kazi. Hayo masharti yanasemaje?

Ajabu moja hapa Tanzania tunashabikia migomo bila kuuliza maswali ya msingi:

  1. Je sheria na taratibu zimefuatwa?
  2. Je kila daktari anayegoma amesoma barua yake ya ajira na masharti yake ya kazi aliyoyakubali? Je wanaoshabikia migomo ya madaktari wamesoma masharti yao ya kazi?
  3. Je? Chama Cha Madaktari (MAT) ni chama cha wafanyakazi kinachoweza kutangaza mgogoro wa kazi na kuwahamasisha wanachama wake wasiende kazini?

Wanasheria wa Serikali wanaosimamia sekta ya afya mnawajibu wa kwenda mahakamani kupata kuulizia uhalali wa mgomo husika na kama hauna uhalali hatua za kisheria zichukuliwe.

Katiba mpya haitakuwa na maana yoyote endapo Sheria zilizotungwa na Bunge au kwa idhini ya Bunge hazitumiki kutuongoza.
 
Kwa hiyo unamaanisha kuwa mgomo wa madaktari hautakiwi? Na kama ndo maana yako, unafurahia manyanyaso wanayoyapata madaktari yanayotokana na ufisadi wa CCM, utawala mbovu wa serikali ya CCM? Jaribu kukumbuka kuwa madaktari pia ni watu na wanafanyakazi ktk mazingira magumu!
 
Kugoma wanaruhusiwa kwa masaa kadhaa,then wanafanya kazi,harafu wanagoma tena kwa masaa kadhaa kama sita hivi1 serikali hi ya kifisadi ya CCM iache usanii na usharobalo.
 
Hebu jaribu kuyajibu hayo maswali mwenyewe ili utuweke wazi na msimamo wa hoja yako.
 
JF -wacheni kujadili hoja isiyoisha na haina mshiko. Kwa mujibu wa sheria ya Kazi ya mwaka 2004 Madaktari hawaruhusiwi kugoma. Acheni uvivu nendeni mkaisome sheria. Ulipokuwa unajadiliwa mswada wa uliozaa sheria hiyo Madaktari walikuwa busy kuchukua vijisenti kutoka kwa wagonjwa. Sikuwasikia wakipiga kelele kuipinga. At the end of the day wanavunja sheria. As long as sijaona chama cha wafanyakazi kilicho nyuma ya mgomo huu au kuanzisha mchakato wa kujadiliana na mwajiri wao then huu mgomo it's a non starter na let us wait and see hivi kwanini wasiweke kwenye bango bayana wanachohitaji in bold letters ili if they make sense tuwaunge mkono au tuwapinge? Wangechukua somo kutoka Kenya how they conducted mgomo wao last year na ukazaa matunda?
 
To hell with your laws!who cares about them?the government?mafisadi?siku hizi sheria zinatumika kukidhi matakwa ya mafisadi tu nothing else!
 
unaongelea sheria Tanzania?mbona hamkujadili sheria wakati mafisadi wa EPA wanarudisha hela walizoiba BOT mchana kweupe kwenye mabox ya mbao tena bila riba?hizo si ndo hela za kuwahudumia watanzania walipa kodi?hakuna utawala wa sheria Tanzania hii hata kidogo.Serikali imekataa kukaa meza na madaktari kama wiki mbili zilizopita,katibu wa wizara ya afya na naibu wake wakaishia kuwatukana wawakilishi wao matusi ya nguoni wewe unaongelea sheria,vyovyote na viwe,with or without your crooked laws
 
unaongelea sheria Tanzania?mbona hamkujadili sheria wakati mafisadi wa EPA wanarudisha hela walizoiba BOT mchana kweupe kwenye mabox ya mbao tena bila riba?hizo si ndo hela za kuwahudumia watanzania walipa kodi?hakuna utawala wa sheria Tanzania hii hata kidogo.Serikali imekataa kukaa meza na madaktari kama wiki mbili zilizopita,katibu wa wizara ya afya na naibu wake wakaishia kuwatukana wawakilishi wao matusi ya nguoni wewe unaongelea sheria,vyovyote na viwe,with or without your crooked laws

chano kavu bila chenga kudadadeki!
 
Hebu jaribu kuyajibu hayo maswali mwenyewe ili utuweke wazi na msimamo wa hoja yako.

kwanza mat haijaitisha mgomo, ni kamati maalumu iliyoundwa kufuatilia maslahi ya madactari ndo imeratibu kazi hiyo. Hivi hizo sheria zinafanya kazi kwa watu wachache tu? Mbona watendaji wengi wanakiuka sheria za manunuzi na wapo tu? Mbona kuna watu wanaajiriwa kwa upendeleo tofauti na sheria zinavyesema?
 
habari zenu wanaJF, nimejiunga leo, lakini kwwa miaka miwili nimekuwa nikisoma na kuelimika na jamvi hili. Kwa upande wa hoja ya mgomo wa madaktari ieleweke kuwa chanzo ni kuchelewa kwa posho ya madaktari waliokuwa intern Muhimbili NH. Wakati wa ucheleweshaji huo sheria zetu zilikuwa kabatini, wamhamishwa na wenzao wameamua kuwaunga mkono, wanasiasa waliojazana wizara ya Afya wanakuja na matamko ya ajabu (moja wapo ni kwamba hao si madaktari ni wanfunzi wa mwaka wa 5). Our government should avoid double standard practices. Sheria haina maan kwa mwenye njaa.
 
Back
Top Bottom