Je? serikali kuja na stimulus package nyingine?

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
157
Wana JF, Nimekuwa nikiwaza sana namna wenye viwanda na wafanyabiashara mbalimbali nchini walivyo/wanavyoathirika na mgao unaondelea wa umeme.Mambo yafuatayo ni matokeo ya mgao huu kwa wenye viwanda na wafanyabiashara; 1.Ongezeko la gharama za uzalishaji kutokana na matumizi ya mara kwa mara ya generators hivyo kulazimisha makampuni ku-review/kupitia upya bajeti zao. 2.Kufungwa kwa baadhi ya biashara kutokana na kushindwa kujiendesha kutokana na either kutokuwa na generator au kushindwa kumudu ongezeko la gharama. 3.Watanzania kuwa laid off/kupunguzwa kazi kutokana na kushuka kwa uzalishaji katika viwanda na hivyo kupunguzwa kama sehemu ya kupunguza gharama za uendeshaji. 4.Kupungua kwa kodi ya mapato kutokana na faida kushuka katika viwanda na pia kupotea kwa mapato kutokana na wafanyakazi waliokuwa laid off kwa maana ya PAYE. Swali langu kwa serikali ya JK ni je? Kwa kuwa serikali iliwafaidia wafanyabiashara/wanunuzi wa pamba kutokana na kushuka kwa bei ya pamba katika soko la dunia! Haioni kama ipo kila sababu ya kuwa-compensate/kuwafidia wafanyabiashara na wenye viwanda kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji zilizosababishwa na mgao wa umeme? na swali la pili Je, serikali inaoyojali wananchi wake na ambayo kauli mbiu/slogan yake ni maisha bora kwa kila mtanzania haioni kwamba inapaswa kuwafidia watanzania waliondolewa/waliokosa kazi kutokana na matokeo ya mgao wa umeme? Naomba kuwasilisha. Kinyamana
 
Back
Top Bottom