Je, Saharan Communication ndio inafilisika?!

Elai

Senior Member
May 26, 2011
154
9
Maeneo mengi huku mikoani walikoweka repeater za redio free Africa (RFA) yamekuwa yakikosa matangazo yao kwa ufasaha. Nichukulie mfano Iringa, matangazo ya RFA kwa mwaka 2011 yamepatikana kwa chini ya 50%. Imekuwa iki-scratch sana na kukata kwa muda mrefu na kurudi kwa muda mfupi kabla ya kukata tena, na hakuna marekebisho yoyote yanayofanyika.Ni kero hasa pale unapokuwa na ratiba ya kutaka kusikiliza kipindi fulani. Zamani haikuwa hivi kiasi kwamba imenifanya niamini kuwa wako hoi kifedha. Ninakaribisha maoni.
 
Tatizo la kuwa na wafanyabiashara waliozoea vya kunyonga. Wanakuwa na uwezo wa kufanikisha biashara zao wakiwa ndani ya siasa, maana mfumo unawakingia kifua. Wakikosa madaraka tu, vyeo viayeyuka na biashara zao. Mifano inazidi kuongezeka. Wapi Scandinavia Bus Services?!
 
Ni kweli kabisa, tupo pamoja.
 
star tv ndio kabisa mpk inaikitisha hata mwanza inapatikana kimachale, mbaya zaidi utakuta wkt wa taarifa ya habari saa 2 usiku-- wanarusha habari ya kitaifa lkn picha za matukio ni za habari ya michezo ni full mkanganyiko na inachukua dk nyingi bila wao kunotice hayo makosa, na makosa yanajirudia karibu kila siku. Sauti haina mpangilio inapanda inashuka mara matangazo yanakata ...
 
Back
Top Bottom