Je, ruksa watoto wa kufikia kuoana?

Hmaster

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
346
86
Mume ana mtoto wa kiume na mke ana mtoto wa kike (au kinyume chake), wanaoana. Katika mazingira hayo watoto wakikua na kupendana wanaweza kuruhusiwa kuoana? Kwa hali ya kawaida ni lazima watafundishwa sana kuheshimiana kama kaka na dada lkn wanaweza pia kukiuka. Je waweza kuruhusiwa kuoana?
 
Hawawezi kuoana,,ina maana wazazi wao wageuke kuwa wakwe zao.....hiii hapana kabisa kabisa...hao ni dada na kaka mpaka kufa......

Imekuwaje umeuliza swali kama hili??? Nini nyuma ya pazia ya hili swali???
 
yawezekana keshampenda kaka/dada yake
 
Mume ana mtoto wa kiume na mke ana mtoto wa kike (au kinyume chake), wanaoana. Katika mazingira hayo watoto wakikua na kupendana wanaweza kuruhusiwa kuoana? Kwa hali ya kawaida ni lazima watafundishwa sana kuheshimiana kama kaka na dada lkn wanaweza pia kukiuka. Je waweza kuruhusiwa kuoana?

KiIslaam Ruksa, unless wawe wamenyonya ziwa moja.
 
Mmmhhh
wanaweza
lakini is not acceptable
This is incest..

In my opinion
Ndugu si lazima
Mtoke tumbo moja
Hawa wawili wazazi
Wao wamesha oana
tayari wao ni ndugu
Na kama wanaishi nyumba..
Moja automatic wamesha kuwa kaka na dada
 
Ruksa kabisaa kuoana kwani hawa si ndugu kabisaa, na hata tukilazimisha ukaka na dada itakuwa kwa heshima tu ya nyumba lakini hii haina mushkeli.
Ikiwa kijana wa kiume anaweza kumuoa mtoto wa shangaziye/binamu kwanini hao wasioane,ambao kihalisia hawana unasaba wa karibu.,
ruksa bila pingamizi japo wafuate sheria za kindoa au kimila/kidini wajilie raha zao
 
subhana llah!!!! mi hisia zangu wallah zanipelekea kuamini kwamba dunia ishakwisha bado bahari kupasuka tuu...inshallah heri lakini allah atunusuru kwa kila baya mi sisi na kizazi chetu inshallallah!!!
 
Ndugu zangu mnaosema wanaweza kuoana mna tatizo na tatizo lenu ni kuathiriwa sana na uzungu katika kila maamuzi yenu,,,wazazi wameoana eti na wao waoane ksb hawajanyonya ziwa moja,,,nyieeee angalieni sana madhara na faida ya ushauri wenu kwa kila mnachoshauri......wazazi wao wageuke kuwa wakwe zao hii kweli ni halali??? Au wanatafuta laana hao.
Wanawake na wanaume wooooote waliojazana dunia hii bado mnaruhusu eti dada na kaka yake waliolelewa nyumba moja waoane kweli????.....jamani sisi walimwengu hata sijui tunaelekea wapi??....eeeh mungu naaamini watu sasa tumepungukiwa hekima ,busara,utu, katika maamuzi yetu mengi tunayoamua. Nakuomba mungu utuepushe na hasira yako tujaalie hekima,busara,utu na kikubwa zaidi tutambue uwepo wako mungu katika maisha yetu ya kila siku.
 
Mume ana mtoto wa kiume na mke ana mtoto wa kike (au kinyume chake), wanaoana. Katika mazingira hayo watoto wakikua na kupendana wanaweza kuruhusiwa kuoana? Kwa hali ya kawaida ni lazima watafundishwa sana kuheshimiana kama kaka na dada lkn wanaweza pia kukiuka. Je waweza kuruhusiwa kuoana?

Ruksa kuoana na kuna CASES nyingi tu kama hizo... Hawa siyo ndugu "wa damu"...
 
Mmmhhh
wanaweza
lakini is not acceptable
This is incest..

In my opinion
Ndugu si lazima
Mtoke tumbo moja
Hawa wawili wazazi
Wao wamesha oana
tayari wao ni ndugu
Na kama wanaishi nyumba..
Moja automatic wamesha kuwa kaka na dada

Afrodenzi,

Hawa siyo ndugu hata kidogo - ndugu lazima mtoke kwenye "family tree" moja na siyo kwenye "family branch"...

"Baba/Mama wa kufikia" siyo BABA na Wala Siyo MAMA bali ni MLEZI...
 
Ruksa kuoana na kuna CASES nyingi tu kama hizo... Hawa siyo ndugu "wa damu"...

Wamesha kuwa
ndugu tangu wazazi
wao wafunge pingu za maisha
ndugu si lazima awe wa damu au
tumbo moja.. mama yangu ame adopt watoto
wawili na hao ni wadogo zangu sasa na ni ndugu
zangu..nataka tu kuonyesha si lazima mtoke tumbo moja..
 
Back
Top Bottom