Je rais Kikwete na Dr Slaa ni yupi anafanana na Mwl. Nyerere?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,600
8,741
Je kama Baba wa taifa Mwl. Nyerere angekuwepo leo Je ni sera zipi na ni nani hasa angemuana anafaa kwa nchi yetu. Ni nani mwenye hekima kama zake, mwadilifu, mwenye uchungu na nchi, mwenye kupambana na rushwa, anaye ogopeka kwa ukali, mwenye kipaji cha akili, mwenye kujitoa muhanga kama yeye. Je ni Raisi wa sasa Kikwete au Dr. Slaa. Tusiangalie vyama kwani Chama alicho acha Nyerere sio hiki cha sasa cha CCM kuna mabadiliko mengi sana.
 
Ili mtu afananishwe na nyerere ni lazima ucheki IQ yake kwanza na uwezo wa kujenga hoja, sio kusoma notisi kila saa kama JK. Juzi kasema hataki kura za wafanyakazi leo anawanyenyekea, mbona asiweke msimamo?
Kweli mkwere hafai hata kufananishwa na julius nyerere wala hana chembe.
Silaa akurupuki, anafanya tafiti na kuja na hoja pamoja na data.
 
Je kama Baba wa taifa Mwl. Nyerere angekuwepo leo Je ni sera zipi na ni nani hasa angemuana anafaa kwa nchi yetu. Ni nani mwenye hekima kama zake, mwadilifu, mwenye uchungu na nchi, mwenye kupambana na rushwa, anaye ogopeka kwa ukali, mwenye kipaji cha akili, mwenye kujitoa muhanga kama yeye. Je ni Raisi wa sasa Kikwete au Dr. Slaa. Tusiangalie vyama kwani Chama alicho acha Nyerere sio hiki cha sasa cha CCM kuna mabadiliko mengi sana.
Kwa vyovyote vile angemchagua padre slaa kwa sababu si kwamba tu ni mkatoliki mwenzetu bali pia nikiongizi wake kwenye nyumba ya ibada. Akikataa sianamwambia tu hutauona ufalme wa mungu, sasa wewe unatarajia nyerere angeenda kuungama wapi? nani yupo tayari kuukosa ufalme wa mbingu? unafanya mchezo na ufalme wa mbingu?
 
Nyerere anatukuzwa mno na watanzania.....
Utasema alikuwa hana kasoro.......

Baadhi ya matatizo ya tanzania leo hii yaliletwa na nyerere....

Hasa hili la rais mwenye nguvu kupita kiasi..........
 
Haya mambo ya kufananisha ama sijui Nyerere yamepitwa na wakati

Wakati huu kinachotakiwa ni nani atakaye jenga mustakbali wa watoto wetu. Nyerere alikua Rais takribani miaka 25 lakini alifeli, saa hizi tuangalie ideology nyingine ya kutunasua. Haya mambo ya kufuata siasa zilizo feli ndo zinaturudisha nyuma.

Sijui azimio la arusha, sijui la msoma, sijui la zanzibar yote hayo wakati wake umepita.
 
Nionavyo mimi Rais Kikwete anafaa kuendelea kuongoza nchi na Dr. Slaa anafaa kuwa kiongozi wa chama cha Upinzani ili aendelee kufumua maovu yanayotendeka nchini na kuwapa nafasi wananchi japo kujua ni nini kinaendelea hata kama mabadiliko ni madogo au hayapo. Nchi yangu ilishanikatisha tamaa kitambo kirefu kilichopita. Hata humu JF huwa nasoma maoni au ushauri wa watu ambao unanithibitishia kuwa sikukosea kukata tamaa.
Mambo mengi ya kizembe au yanayoweza kurekebishwa yamekubaliwa na jumuiya kuwa " .. hivi ndivyo mambo yanavyofanyika... ukitaka chochote ni lazima utoe rushwa...au unyenyekee na kuwatukuza hao unaowaomba maana ukiongea kwa namna ambayo mwenye authority haipendelei basi ujue hutapata kitu...."
Angalau Kikwete ana vitu vyake anavyoweza kuvifanya - kawaruhusu wachache wafurahie mali ya Umma wakati walala hoi wana maisha magumu kupindukia. Naogopa kuwa Dr. Slaa kama viongozi wengine akipata Urais, ama anaweza kujaribu kuleta mabadiliko (mazuri) kwa kasi na yakamkuta yale yale ya Marehemu Sokoine au Mrema. au anaweza yeye kubadilika na kuanza kujinufaisha.
Ili tubadilike tunahitaji DIKTETA, tulazimishwe kubadilika la sivyo cha moto, halafu nchi ikikaa sawa basi tuendelee kwa mfumo huo mpya.

Kwa kujibu swali la nani angechaguliwa na Mwalimu, kati ya hao wawili, sidhani kama angemchagua yeyote kuwa anafanana naye kihekima, uadilifu .... etc. etc.
Angechagua mtu mwingine tofauti. Lakini sisi tunao hao wawili kwa hiyo uchaguzi ni wetu na tutaendelea hivyo hivyo - OVYO TU!
 
Je kama Baba wa taifa Mwl. Nyerere angekuwepo leo Je ni sera zipi na ni nani hasa angemuana anafaa kwa nchi yetu. Ni nani mwenye hekima kama zake, mwadilifu, mwenye uchungu na nchi, mwenye kupambana na rushwa, anaye ogopeka kwa ukali, mwenye kipaji cha akili, mwenye kujitoa muhanga kama yeye. Je ni Raisi wa sasa Kikwete au Dr. Slaa. Tusiangalie vyama kwani Chama alicho acha Nyerere sio hiki cha sasa cha CCM kuna mabadiliko mengi sana.

Hizi sifa ulizo mpatia Nyerere kwanza zenyewe inabidi zijadiliwe, sidhani kama alikuwa muadilifu, anaakili, kajitoa muanga kama unavyofikiria, inawezekana aliogopewa kwa udictetor na u-bully wake.

Justice haikuwepo wakatiwa Nyerere, mwenyenguvu muogope wakati wake, rushwa ilikuwa nyingi, mashirika yetu kila mwaka yalinusuriwa na tax payer, wakati huo huo viongozi wala rushwa waliamishwa shirika hadishirika jingine

Mwizi akikamatwa the next day yuko nje, ndio maana wa TZ wakachukua sheria mikononi kuanza kuwachoma wezi.

Katuchagulia Mkapa, ambae alikuwa mwizi wa National esource na kujilimbikia mimali hadi sasa watz hawana uwezo wa kumnyang'nya, hili lilikuwa chaguo la Bbaako wa taifa

Pengine anaweza fanana na Padri Slaa kwa sababu wote ni network ya kikatoliki na maamuzi yao yanatolewa huko Vatikan, Huwezi kumfananisha ni Kikwete, kwasababu atleast kikwete anasikilza na kupokea ushauri na kikwete anakubali kuwa criticised na anaambilika

Uchumi wa Tanzania uko kwenye shape nzuri ku-compare na uchumi ulioendeshwa na Nyerere, Shule za kumwaga sio wakati wa Nyerere shule chache.

Wa Tanzania wote prospered hakuna kundi moja la dini fulani kufaidika against dini nyingine kama wakati wa Nyerere pamoja na kuwa makundi mengine yalilalamika sana lakini Babaako wa taifa Nyerere hakutaka zikiliza....
 
Nyerere alikuwa mwanadamu kama wanadamu wengine hakuwa kamili lakini alikuwa kiongozi mwadilifu kuna mengi ambayo tunapashwa kujifunza kutoka kwake.Kila mwanadamu ana mapungufu hata kama alikosea ni mwanadamu.
Wewe Mwanafunzi unasema Dr.Slaa abakie kuwa kiongozi wa upinzani ili azidi kufichua maovu wananchi wajue swali kwako 'halafu tukishajua?'
mbona yamefichuliwa mengi hakuna kilichofanyika kwa maana hiyo wewe unaona ni nafuu tuendelee kudanganywa na kesi zisizo na mwisho. Dr.Slaa acha aingie Ikulu kieleweke heshima irudi sio mafisadi wanapeta wakati wananchi walipa kodi wanataabika. Jamani tuwe waungwana katika kufananisha haya mambo ni lini tutaelimika na kugeuka na kujua wakati wa ukombozi ni sasa tumechoooooooooooooooka kunyanyaswa!
 
Naomba nikuulize swali moja : makapuni na mashirika ya umma yamekufa wakati gani? na utupe sababu moja tu kwanini yalikufa.
 
Je kama Baba wa taifa Mwl. Nyerere angekuwepo leo Je ni sera zipi na ni nani hasa angemuana anafaa kwa nchi yetu. Ni nani mwenye hekima kama zake, mwadilifu, mwenye uchungu na nchi, mwenye kupambana na rushwa, anaye ogopeka kwa ukali, mwenye kipaji cha akili, mwenye kujitoa muhanga kama yeye. Je ni Raisi wa sasa Kikwete au Dr. Slaa. Tusiangalie vyama kwani Chama alicho acha Nyerere sio hiki cha sasa cha CCM kuna mabadiliko mengi sana.

Thanks Allah, JK hafanani na Dictactor Nyerere. Na kama Dr. Slaa anafanana na Nyerere basi hafai kuwa kiongozi; kwa sababu atakuwa Dictactor kama Nyerere. Hatutaki Madictactor kama Nyerere waongoze nchi yetu tena.
 
Haya mambo ya kufananisha ama sijui Nyerere yamepitwa na wakati

Wakati huu kinachotakiwa ni nani atakaye jenga mustakbali wa watoto wetu. Nyerere alikua Rais takribani miaka 25 lakini alifeli, saa hizi tuangalie ideology nyingine ya kutunasua. Haya mambo ya kufuata siasa zilizo feli ndo zinaturudisha nyuma.

Sijui azimio la arusha, sijui la msoma, sijui la zanzibar yote hayo wakati wake umepita.

Ndugu yangu MKAMAP pole sana kwa kusema Nyerer alifeli inaona uwezo wako wa kuchambua mambo ni FINYU SANA , na ukifanya uchambuzi unakuwa SUBJECTIVE badala ya kuwa OBJECTIVE,
nakupa mifano miwili kukuonyesha nyerere alikuwa na uwezo mkubwa na vision kwa nchi hii KIUCHUMI, KISIASA na KIJAMII
1. Katika sehemu yoyote duniani huwezi kuleta maendeleo kielimu, hospitali, maji barabara n.k kwa watu amboa wako scattered. Hivyo akaanzisha vijiji vya Ujamaa ili shule za msingi, zahanati, maji kama malambo, visima n.k, barabara zijengwe.

2. Nchi yyote kuendelea ya nchi kiuchumi lazima iwe na viwanda ili mali ghafi inayozalishwa nchini itumike kuzalisha bidhaa kukidhi soko la ndani na ku-export. Tanzania chini ya Nyerere na mpaka anaondoka madarakani kulikuwa na viwanda 50. Kwa uchache tulikuwa na viwanda vifuatavyo baiskeli, viatu, kusindika nyama, ngozi, nguo, zana za kilimo, ku-assemble magari, katani, kamba, tumbaku, almasi, chuma, viberiti, bia, sigara, chai, kahawa, korosho n.k

3. Ili kuleta amani ambayo chachu na ni muhimu kwa maendeleo alituunganisha kwa lugha ya kiswahili, akapinga vita ukabila, udini na pia kuwa na J.K.T ambayo wenywe mawazo mafupi waliona ni sehemu ya kupoteza muda.
USIONE VYAELEA VIMEUNDWA.

MWISHO si Kikwete au Slaa anayeweza kuwa a visonary leader kwa Tz sana sana wnapiga kelele ili watwale lakini si kutufikisha alipotuweka Nyerere.
 
3.

Ili kuleta amani ambayo chachu na ni muhimu kwa maendeleo alituunganisha kwa lugha ya kiswahili, akapinga vita ukabila, udini na pia

quote_icon.png
Originally Posted by MkamaP

boma2000 hapo umenena mkuu!!!
 
Nyerere alikuwa mwanadamu kama wanadamu wengine hakuwa kamili lakini alikuwa kiongozi mwadilifu kuna mengi ambayo tunapashwa kujifunza kutoka kwake.Kila mwanadamu ana mapungufu hata kama alikosea ni mwanadamu.
Wewe Mwanafunzi unasema Dr.Slaa abakie kuwa kiongozi wa upinzani ili azidi kufichua maovu wananchi wajue swali kwako 'halafu tukishajua?'
mbona yamefichuliwa mengi hakuna kilichofanyika kwa maana hiyo wewe unaona ni nafuu tuendelee kudanganywa na kesi zisizo na mwisho. Dr.Slaa acha aingie Ikulu kieleweke heshima irudi sio mafisadi wanapeta wakati wananchi walipa kodi wanataabika. Jamani tuwe waungwana katika kufananisha haya mambo ni lini tutaelimika na kugeuka na kujua wakati wa ukombozi ni sasa tumechoooooooooooooooka kunyanyaswa!
Umesahau kuwa alishasema anawafahamu wauza madawa ya kulevya woote na nini kimetokea! jamani tarehe 31 ipo mbali nataka nitimize wajibu wangu wa kumlima huyu mtu!
 
safi kapigeni kura kudhihirisha hayo msemayo ya kuchoka au kutochoka . kiuhalisia tunahitaji mabadiliko kwani tumeyumba mno na tunazidi kuyumba sidhani kama ni sahihi kuisha kwa kuyumba kiasi hiki huwezi hata kupumua ????!!!!du tulete mabadiliko jama.
:A S thumbs_up::biggrin1:
 
Thanks Allah, JK hafanani na Dictactor Nyerere. Na kama Dr. Slaa anafanana na Nyerere basi hafai kuwa kiongozi; kwa sababu atakuwa Dictactor kama Nyerere. Hatutaki Madictactor kama Nyerere waongoze nchi yetu tena.

Nyerere alikuwa dictator? Labda sielewi maana ya Dictator. Lakini mbona hali yetu ya maisha ilikuwa nafuu kuliko wakati wa Kikwete. Basi udikteta wa Nyerere ulitufaa kuliko demokrasia (sijui kama ndiyo kinyume cha Dikteta) ya Kikwete. Kuna maana gani kuwa na demokrasia ambamo wezi hawaguswi na wanyonge hawafaidi raslimali za nchi yao?
 
Hakuna namna yoyote ya ulinganisho. Kila mmoja anasifa zake na wakati wake. Ni ajabu kumfananisha Slaa na Nyerere au J.K na Nyerere. Kwa sasa kikwete anafaa kuwa rais na Dr. Slaa kuendelea kuongoza upinzani akwa kisiasa hapa Tanzania. Infact, bado siku chache sana aapishwe ba Slaa atabaki akilalama huku na kule asijue la kufanya. Zaidi wachaga watamtimua mara baada ya kuongeza mtaji wa ruzuku chadena.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi bora kwa wakati ule base na mchakato mzima wa maendeleo wa wakati ule, full stop. Mimi ni shabiki mkuu wa Nyerere, lakini nadhani kwa hali ya uchumi wa leo, siasa na maono ya mwalimu yanatatulea matatizo tuu.

Sasa JK hafanani na hatafanana na maono ya Mwalimu, likewise Dr. Slaa hafanani na hatafanana na maono ya mwalimu. End of the story.

Now to compare between JK and SLaa is a different story. Lakini, kumbukeni ya kwamba mwalimu alichukua Tanzania kukiwa na hakuna walimu, hakuna wauguzi na zaidi 80% ya watu walikuwa hawajui kusoma wala kuandika. 24 years later hizo namba zilikuwa flip bottom up. Sasa that is what you call changes.

Now JK plus Mkapa is 15 years, half of 24 now tell me how are we doing? Plus, which strategy mbadala that Slaa is present will cure the problem? Now analyze those two and in the end tutakubaliana Tanzania problem is so complex. And we need more than blah blah za majukwaani.
 
mi nadhani angekuwepo wla tusingefika hapa, angemchagua Salim Ahmed Salim kuwa kiongozi wa nchi yetu na leo hii wala haya mambo tusingeyanongelea hapa Jf tungekuwa na masuala na majukumu yetu mengine kabisa.
 
Wote wawili (Kikwete na Slaa) wanafanana na Nyerere:

Wote ni binadamu!

Wote ni wanaume!

Wote wana watoto!

Wote ni wa-Tanzania!

Wote ni wanasiasa!

Wote wanatongozwa na wadhifa wa u-Rais!

What a question!
 
Back
Top Bottom