Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Rais hastaili kulipa kodi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jembajemba, May 28, 2007.

 1. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 714
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Rais kutolipa kodi kwazua mjadala

  * Mshahara wake, marupurupu hayakatwi kodi
  * Wengi wasema sheria hiyo ya kikoloni, kibaguzi
  * Wataka kila anayepata kipato akatwe kodi
  * Mawaziri, Mamlaka ya Mapato watupiana mpira

  Julius Samwel na Ramadhan Semtawa

  SHERIA ya Kodi inayowapa kinga marais wa Jamhuri ya Muungano na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutokatwa kodi katika mishahara yao, imeibua mjadala mpya na kupokelewa kwa mitazamo tofauti na watu kutoka makundi mbalimbali ya jamii nchini, baadhi wakisema hiyo ni sheria ya kikoloni iliyowapa kinga wafalme.

  Kundi moja linalopinga sheria hiyo limeiita kama ya kibaguzi inayotoa mwanya kwa baadhi ya watu kutolipa kodi katika nchi huku wengine wakikamuliwa licha ya vipato vyao kuwa vidogo.

  Hata hivyo, kundi jingine linaonekana kuwa katikati likisema ni athari za kikoloni kwani imeegemea kwa mkoloni wa Tanganyika ambaye ni nchi ya Uingereza hivyo si ajabu sana kuona kinga hiyo.

  Sheria ya misamaha ya kodi imegawanyika katika makundi matatu, kuna misamaha inayotolewa kwa ajili ya ushuru wa forodha ya mwaka 1976, misamaha inayotolewa kwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya mwaka 1997 na misamaha inayotolewa kwa mapato iliyopo katika sheria ya mwaka 2004.

  Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofuati kuhusiana na sheria hiyo, wanasiasa, wasomi, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanasheria, wote wanasema kinachotakiwa ni kila mtu alipe kodi kulingana na kipato chake.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nestory Ngulla, alisema tatizo kubwa lililopo ni mfumo mzima wa sheria kwani unaumiza wafanyakazi zaidi kuliko makundi mengine ya kijamii.

  Ngulla alisema wafanyakazi wamekuwa wakikatwa kodi kubwa huku makundi mengine kama wafanyabiashara na wakulima wakizidi kupunguziwa mzigo huo kwa madai kwamba wanaondolewa kodi za kero.

  "Tatizo ni mfumo mzima wa sheria ya kodi, inaumiza zaidi wafanyakazi kuliko wakulima na wafanyabiashara, nafikiri kunahitajika mabadiliko katika mfumo mzima wa sheria yenyewe ya kodi," alifafanua Ngulla.

  Alisema kinachohitajika sasa ni kuwepo kwa mfumo wa kodi ambao utamfanya kila mtu kulipa kodi kulingana na ukubwa wa kipato chake.

  "Kuna mambo ya kufanya kama kuangalia distribution of income, (mgawanyo wa kipato), anayepata kipato kikubwa alipe kodi kubwa na anayepata kipato kidogo alipe kodi ndogo inayoendana na kipato chake," alisema Ngulla.

  Ngulla alisema kuna watu hapa nchini wanaishi bila kujua kodi inavyolipwa huku watu wengine wakizidi kuumia kwa kutwisha mzigo wa kodi.

  James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, alisema sheria hiyo ni ya kibaguzi na haipaswi kuwepo kwani inapingana na katiba ya nchi.

  Mbatia alisema sheria yoyote inapotungwa haipaswi kuwa na ubaguzi ndani yake kwa kupendelea kundi moja na kuumiza jingine katika nchi.

  Alisema kitendo cha Rais wa Jamhuri na SMZ kutolipa kodi hakikubaliki kwani mishahara na marupurupu yao ni makubwa hivyo kutolipa kodi ni sawa kufanya ubaguzi.

  "Sheria yoyote inapotungwa haipaswi kuwa ya kibaguzi, kwanini Rais wa Zanzibar na wa Jamuhuri wasilipe kodi wakati mishahara na marupurupu yao ni makubwa, hiki ni kitendo cha kibaguzi," alisema Mbatia.

  Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza kwa kifupi alisema sheria hiyo inaondoa uwajibikaji katika kulipa kodi nchini.

  Profesa Lupumba alisema, kimsingi kila anayepata mshahara anapaswa kulipa kodi katika nchi.

  "Sheria ya namna hii inaondoa uwajibikaji katika ulipaji kodi, kila anayepata mshahara anapaswa kulipa kodi," alisisitiza.

  Kwa upande wake Mhadhiri wa Kitivo cha Sheria Kutoka Chuo Kikuu cha Dares Salaam, Dk Ringo Tenga, alisema sheria hiyo ni urithi wa kikoloni ambayo sehemu kubwa ya nchi za Jumuiya ya Madola inaitumia.

  Dk Tenga alisema, yeye binafsi haoni kama kuna tatizo kwani ni athari za kikoloni ambazo hadi sasa zipo na kuongeza kwamba rais anafanyakazi kubwa hivyo hizo ndizo fursa zake za kupata.

  Mfanyabiashara wa samaki katika soko la Feri jijini Dar es Salaam, Salum Mkwama aliiambia Mwananchi kuwa sheria hiyo inawavunja nguvu wananchi wa kipato cha chini kama yeye kulipa kodi iwapo wakubwa wameenguliwa kulipa kodi.

  "Inanipa shida na kunivunja nguvu kulipa kodi iwapo wakubwa wa kaya hawalipi," alisema.

  Kwa mujibu wa sheria hiyo kiasi chochote cha fedha kinacholipwa kwa rais wa Jamuhuri ya Muungano au SMZ kama mshahara au fedha ya kujikimu kazini au kiasi cha fedha kilicholipwa kwa rais kutoka katika mfuko wa umma, hakitalipiwa kodi.

  Afisa wa juu katika Wizara ya Kazi,Maendeleo ya Vijana na Ajira, ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema sheria hiyo ni mbaya na kwamba inatoa nafasi kwa baadhi ya wananchi kukwepa kodi.

  Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma ), Hawa Ghasia alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa sheria hiyo alisema ofisi yake haishughulikii misamaha na kwamba anayepaswa kuulizwa ni Waziri wa Fedha.

  Zakia Meghji, Waziri wa Fedha alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, alijibu, "nafikiri ni vema ungeenda kuuliza watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato nchini).

  Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitllya, alipoulizwa alijibu, "kazi yangu mimi ni kusimamia sheria, fahamu hivyo, jukumu la kutunga sheria ni la wabunge si la kwangu".

  Alipoulizwa kwamba, haoni kama TRA ina nafasi kubwa katika mabadiliko ya sheria kutokana na kutoa mapendekezo serikalini, Kitillya alijibu, "hata nikitoa au TRA ikitoa maoni bado kukubaliwa ni jambo jingine, Waziri wa Fedha ndiye mwenye dhamana ya mwisho na mambo yanayohusu sera serikalini,"alisema

  Kitillya alisema hata kama sheria hiyo inatoa msamaha huo jambo hilo liliamuliwa na wabunge, na kuongeza " sasa kawaulize wabunge".
   
 2. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 714
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  kwani kuna ulazima gani wa kurithi sheria za kikoloni ambzo hazina faida kwa taifa??

  Mimi kwa mtazamo wangu naona Rais anastaili kulipa kodi kwani yeye ndio kigezo kizuri kwa Taifa, sasa ikiwa yeye halipi kodi wananchi watafanya nini?
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,388
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sheria za kikoloni ni nyingi sana kwani hata ukiangalia sheria inayoliendesha jeshi la police ni ya 1954 ikiitwa police ordinance act of 1954,

  Hii nchi ni ya ajabu kweli kwani mambo yanavyokwenda ni kama haina mwenyewe.
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,388
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Rais kulipa kodi alipaswa awe wa kwanza ama ndio maana anaogopa kuwaambia makampuni ya madini walipe kodi kwani watamuuliza kuwa mbona wewe hulipi?

  Rais Kikwete kama wewe ni muungwana basi anza leo kulipa kodi,na hililitatusaidia kujua hata mshahara wako ni kiasi gani.
   
 5. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 714
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Kama ni hivo basi kuna haja gani ya kujitawala ikiwa bado mpaka leo tunafuata sheria za kikoloni?
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 13,887
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hapa kama kawaida yetu tunakuwa emmotional for nothing, kama hatuipendi hiyo sheria kama wananchi at large, tunahitaji kuijadili kwa mapana na marefu na hatimaye kuamua kama kweli tunahitaji kuibadili hi sheria, lakini kuanza kumrushia maneno rais wetu kwa ajili ya sheria ambayo Mwalimu, na marais wote waliopita hawakuiona madhara yake, ndio ninaposema kuwa tunakuwa wote wasaniii kuanzia viongozi mpaka wananchi!

  Tukimruhusu rais kufuta sheria tu mradi hatuitaki tutakuwa weendawazimu, wananchi kwa kulitumia bunge letu ndio tunahitaji kuiangalai hiyo sheria na zingine nyingi tulizonazo ambazo ni mbovu!
   
 7. s

  starta2 Member

  #7
  May 28, 2007
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata rais wa marekani analipa kodi itakua kikwete wa tanzania.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 13,887
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kikwete as a person hahusiki na hiyo sheria, ni tatizo la bunge letu kuna anayohusika nayo kama ya safari nyingi zisizokuwa na faida, lakini la kodi ya mshahara wake ni ni sisi wananchi na bunge letu!
   
 9. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #9
  May 28, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 4,055
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 38

  I agree kwamba kumshambulia Kikwete kwa hii sheria haijakaa sawa; lakini yeye anapaswa kuonesha njia kama kweli amepania kuboresha mambo likiwemo jambo la utawala bora. yeye kuikalia kimya hiyo sheria maana anataka naye atende ujinga uleule wa wenzake. Kuongoza ni kuonesha njia, sasa Kikwete aoneshe njia katika hili pia. Aagize jambo hili litengenezwe marakebisho marekebisho bungeni haraka. Au nali hili wanasubiri mpaka Denmark wasitishe misaada?
   
 10. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 714
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Mwanasiasa,

  maneno hayo ......
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,049
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  Hapa ndipo tutaweza kukumbusha. Je, hata zile biashara zao wanazoanzisha kwa majina yao wakiwa Ikulu kumbe nazo hazilipiwi kodi? au ndio maana Ben na Anna walianzisha kwa kiburi kampuni inayoitwa Anna & Benjamin Mkapa kwa kifupi ANBEM na si Benjamin Mkapa & Anna (BEMAN) yaani kuonyesha msisitizo ni nani aliyeleta idea ya kuanzisha kampuni, yaani ni ile jadi ya biashara
   
 12. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 714
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  duh!!!! hawa watu wanatula kweli kweli, yaani wanatake advantage ya uraisi wao kuzidi kutukandamiza walala hoi - hawa ni watu wa watu kweli ???
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  May 28, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 8,058
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 48
  Check marais wa marekani wanavyolipa kodi hapa; tangu miaka hiyo ya "ukoloni"
   
 14. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #14
  May 28, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 4,055
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 38
  watu wengine tukisema hatuna uongozi katika ile nchi tunaonekana tuna nongwa. Tumehubiriani miaka mingi tena katika CCM hiyohiyo kuwa uongozi ni kuonesha mfano, sasa kama kiongozi hata kodi halipi hivi anaonesha mfano gani hasa?
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  May 28, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 16,619
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 48
  Mnayajua leo jamani?.... ndio Bongo hiyo kwani naposisitiza sheria ya viongozi kutoruhusiwa kufanya biashara niliyaona yote haya. Viongozi wetu wanapewa kila kitu ndani ya Uongozi wao tena kwa maisha ya Afrika wanabaki na akiba kubwa ya fedha kuliko kiongozi yeyote wa nchi za magharibi...Mishahara yao - they spent NOTHING! out of it!..yet leo wanajiongezea na nafasi za biashara, hawalipi VAT wala kodi yeyote ile inayomkabiri mwananchi wa kawaida. Kinachopelekwa TRA bandarini ni barua tu ya kuonyesha Tax Exemption!
  Barua toka kwa mzeee!
   
 16. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 4,085
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mshahara/marupurupu(Tax free) huduma zote kutoka serikalini mweeeh!!! he got it made ndio maana kila mtu anataka kukimbilia Ikulu, na ukistaafu bado unapeta na huduma za serikali.

  Nadhani wakati umewadia wa kubadirisha sheria nyingi zilizopitwa na wakati.
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 13,887
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mzee Idacon,

  Heshima mbele mkuu, maneno mazito!
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,049
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  Kwani ni huuduma pekee? Rais Mstaafu analipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hii ina maana kwamba Ben analipwa asilimia 80 ya mshahara wa JK. Achilia mbali anasafiri kila kukicha kupitia NGO ya kimataifa anayoitumikia. Pamoja na hayo anapewa walinzi, magari, nyumba na huduma zote ikiwamo za afya yeye na familia yake. Sasa bwana mmoja jana aliniuliza, mzee hebu niambie, yule mheshimiwa (Ben) anahitaji kilo ngapi kwa siku kwa ajili ya mlo? je, ana watoto wangapi wanaodaiwa ada ya shule? je, anadaiwa kodi ya nyumba kiasi gani? je, anahitaji nauli kiasi gani kwa safari ya kwenda kwao Masasi, Lushoto, Mtibwa au Afrika Kusini? Anahitaji kiasi gani kununulia Aspirini akiumwa kichwa? SIKUA NA MAJIBU ila nilipata uchungu na kutokwa na MACHOZI kwani watoto wangu wawili juzi walirudishwa nyumbani kwa kuwa nilichelewa kulipa ada hadi mwisho wa mwezi ndio nipeleke hizo pesa, wakati wenzao wanaendelea na masomo. Hayo ndio maisha INATIA UCHUNGU halafu anakuja mtu anaandika barua ndefu katika gazeti la serikali la DAily News kumtetea Mkapa, eti THISDAY wamepata wapi hizo habari ambazo eti ni za siri. HAwana hata aibu
   
 19. M

  Mama JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,906
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Rais aonyeshe mfano, amuru mabadiliko ya sheria husika katika hili, tena yaharakishwe.....sio kodi tu, ukatwe makato kwa ajili ya akiba ya uzeeni.
   
 20. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,142
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi majuzi (Jumanne) nilikuwa nafuatilia kipindi cha "Je tutafika?" kinachorushwa na kituo kimoja cha runinga hapa Bongo. Nilikuwa excited kusikia maneno kutoka kwa mmoja wa wana panel aliposema kuwa kuna mwaka huko nyuma, walimu nchini walifanya mgomo kudai maslahi. Kuonyesha kwamba anajali, rais wa awamu hiyo, the Late Mwalimu JKN aliamuru mshahara wake upunguzwe kwa ASILIMIA ISHIRINI (20%).

  Then I asked myself about presidents of this era in our country, Who can attempt even 5%? Hata kama ile deduction ya JKN (Mungu amrehemu) isingekuwa lolote kwa madai ya wafanyakazi wote waliogoma, but can you imagine the spirit of Mwalimu JKN?
   

Share This Page