Je, Rais Hajui maana ya Neno "SIJUI'??? Tumsaidie

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,416
85,844
Wapendwa, Topic hii si ya Kisiasa bali ni Lugha,
Hivyo naomba mawazo na michango yenu iishie hapo tu kama itawezekana.

Kwa kipindi kirefu sana nimekuwa nikimsikia Rais akinukuliwa au nikimsikia mwenyewe akitumia sana neno "SIJUI" katika mazungumzo na maongezi yake ambayo kauli hizo zimekuwa na maana kubwa sana kwa Taifa.

Kwa mfano, niliwahi kusoma na bado inaendelea kusemwa kuwa Rais eti :HAJUI" source ya umaaskini wa watu wake....
Pili, hebu fuatilia makala hii niliyoichukua kwenye gazeti fulani wakiwa wamenukuu maneno hayoo toka kwa Mkulu na jinsi yanavyobeba uzito;

“Hadi leo sijui kwa nini hasa watu (mawaziri) wanashindwa kuzungumza mambo yaliyofanywa na Serikali na kuwapa uwanja mpana wenzetu wa upande wa pili (wapinzani) ambao wanajua kweli kuvitumia vyombo vya habari. Sisi tunaendelea kulalamika kila siku kwamba hatuandikwi, nani atakuandika wakati hutoi taarifa,” alisema Kikwete

Hebu cheki na hii pia

"Sijui kwa nini hatuwi wepesi kuyasemea mafanikio mengi tuliyoyapata tukaacha wasiotutakia heri wanaosema hatukufanya kitu wasikike mpaka waonekane wanasema kweli," alisema.

Alisema hajui na hana majibu mazuri ya kwa nini Serikali imekuwa ikishindwa kuzungumza mambo mazuri yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitano na hata wakati mwingine kushindwa kuzungumza jambo hadi wampigie simu, kitu ambacho ni aibu.

Hii nayo Vipi??

“Unajua mimi sijui hadi leo ni kwa nini hasa watu wanashindwa kuzungumza mambo yaliyofanywa na serikali na kuwapa uwanja mpana wenzetu wa upande wa pili ambao wanajua kweli kuvitumia vyombo vya habari huku sisi tunaendelea kulalamika kila siku kwamba hatuandikwi, nani atakuandika wakati hutoi taarifa,” aliuliza Kikwete.

Haya na nyie tusaidieni ili tumsadie Mzee mwenzetu, matumizi ya haya maneno ianonekana yanamchanganya sana. Tumsaidieni
 
Hii yote ni kwa sababu hajui alikwenda kufanya nini Ikulu, tutamsaidiaje kwa sababu hajui nguvu ya madaraka ya Rais katika kuendesha nchi. Hajui kama ana uwezo wa kumfukuza kazi waziri asiyefuata maagizo yake ama asiye wajibika! Kama alishindwa kujua kwa nini alishindwa uchaguzi huu mpaka akatafuta maconsultant kum-intelligencia unategemea nini. Hajui kama madini tumeyatoa bure na hayarudi tutabaki na mashimo, utamsaidiaje mtu huyo.

Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba, ili kumsaidia yeye na taifa, tumshinikize atoke Magogoni la sivyo nchi itaharibika kama Zimbabwe!
 
Sijui kwa nini anawlealea watendaji wabovu serikalini,
Sijui kwa nini haelewi kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko ya kuonekana kwa vitendo,
Sijui kwa nini haelewi watu kwa sasa hawampendi hata vijijini,
Sijui kwa nini haelewi waandamizi wake ni wanafiki na wanmuogopa ili kulinda vyeo vyao,
Sijui lini atakuja kuelewa umasikini wa watanzania,
Sijui, Sijui kama yeye ndiye Rais, maana kila kukicha analamikia utendaji mbovu wa wateule wake!!
Sijui...........................................................................................................................................
Sijui..........................................................................................................................................
 
Hii yote ni kwa sababu hajui alikwenda kufanya nini Ikulu, tutamsaidiaje kwa sababu hajui nguvu ya madaraka ya Rais katika kuendesha nchi. Hajui kama ana uwezo wa kumfukuza kazi waziri asiyefuata maagizo yake ama asiye wajibika! Kama alishindwa kujua kwa nini alishindwa uchaguzi huu mpaka akatafuta maconsultant kum-intelligencia unategemea nini. Hajui kama madini tumeyatoa bure na hayarudi tutabaki na mashimo, utamsaidiaje mtu huyo.

Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba, ili kumsaidia yeye na taifa, tumshinikize atoke Magogoni la sivyo nchi itaharibika kama Zimbabwe!

Hivi kumbe ndio hivyo eeee, na mimi nilikua sijui
 
Sasa huko mbali huko, mkitumiwa sms toka Ikulu mnalalamika! ila hata mini kweli sijui kwanini hajui maana ya neno hajui
 
Wapendwa, Topic hii si ya Kisiasa bali ni Lugha,
Hivyo naomba mawazo na michango yenu iishie hapo tu kama itawezekana.

Kwa kipindi kirefu sana nimekuwa nikimsikia Rais akinukuliwa au nikimsikia mwenyewe akitumia sana neno "SIJUI" katika mazungumzo na maongezi yake ambayo kauli hizo zimekuwa na maana kubwa sana kwa Taifa.

Kwa mfano, niliwahi kusoma na bado inaendelea kusemwa kuwa Rais eti :HAJUI" source ya umaaskini wa watu wake....
Pili, hebu fuatilia makala hii niliyoichukua kwenye gazeti fulani wakiwa wamenukuu maneno hayoo toka kwa Mkulu na jinsi yanavyobeba uzito;

“Hadi leo sijui kwa nini hasa watu (mawaziri) wanashindwa kuzungumza mambo yaliyofanywa na Serikali na kuwapa uwanja mpana wenzetu wa upande wa pili (wapinzani) ambao wanajua kweli kuvitumia vyombo vya habari. Sisi tunaendelea kulalamika kila siku kwamba hatuandikwi, nani atakuandika wakati hutoi taarifa,” alisema Kikwete

Hebu cheki na hii pia

"Sijui kwa nini hatuwi wepesi kuyasemea mafanikio mengi tuliyoyapata tukaacha wasiotutakia heri wanaosema hatukufanya kitu wasikike mpaka waonekane wanasema kweli," alisema.

Alisema hajui na hana majibu mazuri ya kwa nini Serikali imekuwa ikishindwa kuzungumza mambo mazuri yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitano na hata wakati mwingine kushindwa kuzungumza jambo hadi wampigie simu, kitu ambacho ni aibu.

Hii nayo Vipi??

“Unajua mimi sijui hadi leo ni kwa nini hasa watu wanashindwa kuzungumza mambo yaliyofanywa na serikali na kuwapa uwanja mpana wenzetu wa upande wa pili ambao wanajua kweli kuvitumia vyombo vya habari huku sisi tunaendelea kulalamika kila siku kwamba hatuandikwi, nani atakuandika wakati hutoi taarifa,” aliuliza Kikwete.

Haya na nyie tusaidieni ili tumsadie Mzee mwenzetu, matumizi ya haya maneno ianonekana yanamchanganya sana. Tumsaidieni

kama utakua mpembuzi wa mambo, jitahidi kutafuta thread moja huwa imo humu jf, imeandikwa.... "Mh. Kikwete hii imekaaje?" kuna mwana jf moja anaitwa Sagna alitoa mchango wake mzuri sana kuhusu "SIJUI" za Baba Riz. Natumai utaipenda na kupata jibu kamili.
 
Kumbe hajui?
Tumrudishe kuwa katibu wa chama tandahimba, labda ndo anachojua.
 
I wonder = Sijui - Sijui hawa mawaziri wanafikiri nini!
Nadhani Kiingereza kimeathiri utumiaji wa neno jua/sijui
Maana I know = Najua
Sijui = I don't know
Aisee = ?
 
Aaaah, kwa hio ni athari za kiingereza kwenye kiswahili eeehh, kama wengi wenu mnavyosema "Mwisho wa siku" badala ya "Hatimae" neno ambalo mmelichukua kwenye "at the end of the day"! Basi tumsahihishe tu polepole maana wapo pia wanaosema hivi "tutakwenda kusoma" ikiwa ni kiingereza "we are going to read" haaaa Wabongo bana, hawawezekaniki!
 
Yani sijui kwa nini mkulu hajui kila kitu, anawalaumu watendaji wake kwa kulalamika wakti yeye ndio namba moja kwa kulalamika, anakaa kwenye runinga kutulalamikia kwamba hawafanyi kazi sasa sijui sisi tufanye nini
 
Si na yeye pia hajui??
 
Mimi sijui mpaka leo ni kura zipi zilimrudisha madarakani.

Hata mimi mpaka sasa SIJUI rais wa Tanzania ni yupi maana niyekuwa namfikiria kuwa huenda ndiye rais yeye kazi yake kila siku ni kulalamika tu
 
Waungwana, basi tumwache tu maana ni wazi kuwa HAJUI wajibu wa Rais na ni kwa nini yeye ni rais wa nchi, inaonekana pia hata yeye mwenyewe HAJUI ilikuwaje akawa Rais na hata watanzania HAWAJUI nini kilitokea mpka jamaa akawa Rais wao. Sisi sote HATUJUI, lakini wakati UNAJUA mustakabali wa taifa hili lenye baadhi ya wananchi WASIOJUA nini cha kufanya.

Mtu kama HAJUI na bado HAJUI kuwa HAJUI hawezi kujua kuwa HAJUI=..................................what happened mpaka akawa president, who blinded us ikiwa bado hajui na kila siku anakiri kuwa hajui?
 
Back
Top Bottom