Je, posho kwa wanachama si rushwa ?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,037
22,728
Nimekuwa najiuliza maswali kadhaa hivi karibuni:-

1. Kwa nini mfanyakazi anayelipwa mshahara alipwe posho ili kuhudhuria vikao vya kazini?
2. Kwa nini mwanachama wa chama cha siasa adai posho kuhudhuria vikao vya chama.
3. Kwa nini mbunge alipwe posho anapohudhuria vikao vya bunge?
4. Kwa nini posho, kweli tuna pesa ya kuchezea namna hii.

Je, posho ni kipato halali ama namna fulani ya ufujaji ?
Je, posho ni malipo halali ama ni aina fulani ya rushwa ?
Je, posho hutozwa kodi kama ni mapato halali ?
Je, posho kwa nini haitolewi kama mkopo ?

Kama tunashindwa kuwapa wanafunzi wetu mkopo kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha, mfanyakazi anayelipwa mshahara tunawezaje kumlipa posho isiyo na kodi eti ahudhurie semina, washa n.k.
 
Nimekuwa najiuliza maswali kadhaa hivi karibuni:-

1. Kwa nini mfanyakazi anayelipwa mshahara alipwe posho ili kuhudhuria vikao vya kazini?
2. Kwa nini mwanachama wa chama cha siasa adai posho kuhudhuria vikao vya chama.
3. Kwa nini mbunge alipwe posho anapohudhuria vikao vya bunge?
4. Kwa nini posho, kweli tuna pesa ya kuchezea namna hii.

Je, posho ni kipato halali ama namna fulani ya ufujaji ?
Je, posho ni malipo halali ama ni aina fulani ya rushwa ?
Je, posho hutozwa kodi kama ni mapato halali ?
Je, posho kwa nini haitolewi kama mkopo ?

Kama tunashindwa kuwapa wanafunzi wetu mkopo kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha, mfanyakazi anayelipwa mshahara tunawezaje kumlipa posho isiyo na kodi eti ahudhurie semina, washa n.k.
Positive think about posho is
ni one of motivation ndugu, ili watu waweze kusikiliza na ku act vizuri they need some kind of motivation,
negative
inajenga kizazi kisichoweza kujituma kunakuwepo na mmomonyoko wa maasili ndo maana watu waliotoka serikalini ni vigumu kufanya kazi kwenye private Institution, wamezowea kupewa bahasha then inakwenda unakuta boss anaforge risti hata km ni ya taxi unadhani ukimpa wizara ata forge risti za taxi???????? hapana ataenda level ya mikataba feki, Radar and Richmond....
hivi wizara hii ya ajira inafikiria nini wa angalie market price ya staff wake mtu ameenda shule analipwa laki 2, anaishi nyumba ya laki 3 kwa mwezi, gari la kifahari , watoto international hapo ndo ufisadi unapotungia mimba let move back yakishakomaa huwezi kuyafundisha tena yatalalama km karamagi kwamba yanaonewa sio kwamba anadanganya ndo hivyo anavoona ati....
 
Walengwa wa posho hizi wanaoingia JF hebu mtujibie maswali yaliyoulizwa.Huenda kuna maelezo mazuri kutoka kwenu yenye kuhalalisha posho hizi.
Ila sijui kuna jibu gani kuhusu kutokutoza kodi hizo posho maana ni income NA KUFUATANA NA SHERIA YA KODI KILA PATO LINALOFIKIA KIWANGO FULANI NI WAJIBU KUTOZWA KODI.
 
Katika hili ninalo weza sema ni kwamba, mishahara ya serikali ni midogo mno, hivyo watu huishi kwa posho hizo, vinginevyo ni balaa tupu!

Ebu fikiria ofisa mzima anaye ishi dar nikiwa namaana garama za usafiri na ughali wa maisha umzungukao halafu mwisho wa mwezi anapokea laki moja na nusu! Yaani hapo lazima atengeneze mazingira ya posho ili maisha yaende.

Ila ukiangalia garama zinazo tumika katika posho na workshop uchwara, nibora serikali ingepunguza hizo posho na kuwalipa wafanyakazi wake vizuri tena huenda ikapunguza garama kubwa zinazoumika kama posho.
 
Kwanza nampongeza aliefikilia swala hili. Najua matatizo ya ufisadi Bongo ndio yanayoibua hata maswali ambayo huenda yakakosa majibu mazuri kuharalisha uwepo wake.

Nadhani swala la posho limekuwa derived kutoka kwenye management and psychology. Ukisoma mambo ya theories of Motivation, 'Theory X and Y' nadhani unaweza pata sababu yauhalali wa posho. Kimsingi ni positive motivation ambayo inamfanya mtu kuwa indebted na mchango anaotakiwa kuutoa katika mjadala fulani. Hivyo inadhaniwa kuwa kumpa mtu posho kunamuanda kisaikolojia 'unasettle maindi ya mtu' asione kama anapoteza muda na kwamba angeweza kufanya jambo jingine likamuingizia kipato.

Kimsingi hata sisi watu wa private institution tunanamna zetu za kumotivate wafanyakazi more or less kama watu wa government. Vilevile swala la posho si swala la mishahara midogo. Hi inaweza kujidhihirisha kwa maboss wenye mishahara mikubwa lakini bado unakuta posho zao ni nono vilevile. Kuweka tax kwenye posho niswala linaloweza jadilika. Lakini nadhani madhara ya tax yako wazi. Kimsingi ukipose tax kwenye posho utaleta kitu kinachoitwa societal welfare loss. Hivyo basi kumaintain welfare itabidi uongeze posho (gross posho) ili baada ya tax ibakie kama ilivyokuwa mwanzo. Angalizo kama inafanyika hivi, baadhi ya private firm zitaacha kutoa posho hivyo madhara yatakuwa makubwa zaidi (welfare impact) na hivyo tija kuzorota.

Hivyo nadhani swala la posho waheshimiwa wapiganaji wenzangu tuliache kimsingi ni swala muhimu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom