Elections 2010 Je Obama anataarifa la jina Lake kutumika Kuwa-hadaa watanzania?

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,393
4,056
kwa mara ya pili katika muda wa wiki moja mgombea moja wa Uraisi ametumia jina la Raisi wa merekani ili kuvutia wapiga kura, mwanzo ni pale alitumia hotuba ya obam kwenye millinium goal challenge meeting, na sasa hivi ni hili la misaada bila kuzingatia zaidi ya hapo kwamba hiyo misaada sio ya kwake binafsi bali ni kupitia mikataba iwe ya nchi moja moja bilatteral au ya nchi nyingi multi-latteral na zaidi ya hapo hata akija lipumba/slaa misaada hiyo itatoka tu.
 
Lazima Kijana yupo update, network yake si mchezo, na kwa jinsi alivyo, anaweza kuwaamuru wasaidizi wake, wamtwangie simu huyu anayetumia jina lake vibaya muwa aache mara moja. BO si mchezo, unakumbuka Uganda ktk kikao cha nchi za Africa mwezi wa nane? mwakilishi wake alisoma hotuba kwa niaba yake na akaweka wazi kuwa, atafanya ushawishi kwa mataifa mengine makubwa duniani ili kwamba viongozi wote wa Africa walioweka fedha zao ktk mabenki ya nje, atazitaifisha. That guy is No nonsense......Republican wenyewe pale wamenyosha mikono juu.
 
Niliongelea ulimbukeni wa kumhusisha sana Obama katika uchaguzi wa Tanzania. Watanzania makini wakikusikia unaongelea sana habari za Obama watakuona utakuwa kiongozi kibaraka wa Wamarekani tu, watajiuliza unataka kuendeleza maslahi ya Watanzania au Wamarekani? Una fikira za kujitegemea au za uomba omba ? Unaweza kujiamini na kumpinga Obama kama maslahi ya Watanzania yatakutaka kufanya hivyo?

Nimeongelea zaidi upuuzi wa kuabudu viongozi wa nje katika chaguzi zetu paragraph ya kumi hapa
 
Back
Top Bottom