Je ni Sahihi na Halali Kuyasimamisha Mabasi yenye Chasis za Malori?

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Kuna jitihada zinaendeshwa na Jeshi la Polisi Idara ya Usalama Barabarani la kuyasimamisha mabasi yenye chasis za malori kutokufanya safari. Ninachajiuliza mimi ni hiki:

1) Ni namna gani mabasi haya yaliweza kupata uhalali ya kuingia barabarani?

2) Hao akina Kombe waliosoma sana (kama alivyojisifia mwenyewe jana kwenye vyombo vya habari) walikuwa wapi kubaini chasis hizo kabla ya kuzipa leseni za kufanyia safari.

3) Je hii siyo hasara kwa taifa pia kutokana na gharama za ujengaji bodi zilizotumiwa na wafanya biashara? (Hapa nisieleweke kuwa nafurahia ajali za mabasi)

4) Kwa nini wahusika waliyoyaidhinisha mabasi haya kuingia barabarani wasiwajibike pia kwa ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kazi zao?

Ushauri wangu kwa hili ni kwamba Mabasi yaliyokwisha pata TLB yaendelee na kazi ya kusafirisha abiria, ila zisitolewe TLB kwa mabasi mengine yenye chasis za malori
 
Back
Top Bottom