Je, ni sahihi Mwanajeshi na Polisi kutolipa nauli?

hivi wanapokwenda kula restaurant napo wanalipa????

mwanafuzi analipa nauli na ananyanyaswa!!!!!!!!!

mjeda halipi na adadekezwa!!!!!!!!

na ma-dr je wakivaa sare za kazi wasilipwe.
 
Fikiri nje ya box rafiki askari huwa anahitajika mara nyingi katika hali dharula sasa ukisema alipe nauli huoni itakuwa tatizo kiulinzi maana naye ni mtu huwa anaishiwa pesa je akishindwa kufika sehemu ya tukio sababu ya nauli itakuaje kwa wale wanaotaka kuokolewa? Kumbuka kuwa askari hufutilia watuhumia au mashaidi kupitia usafiri huo je atalipa nauli mara ngapi kwa siku? Tukumbuke ndani ya gari akiwepo askari ndiyo huwa msuluhishi wa migogoro ikitokea,. Fikiri vizuri askari usimfananishe na mwanafunzi
 
Mwanafunzi anaweza akawa mtoto wa askari hivyo ukimfananishia naye ni kuwakosea hishima walinzi wa nchi yetu.kumbuka kabla ya chochote kutendeka kwa binadamu ulinzi na usalama ni kitu cha kwanza nje ya hapo hakuna taifa. Kumbuka kuwa walinzi wetu hawa ndiyo walinaoshikilia roho zetu wakifanya uzembe kidogo tu mamilioni ya watz wanapoteza maisha. Shikamoo wanajeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama maana bila nyie hakuna tanzania. acha kabisa kusumbua hao watu. kwanza kwenye daladala huwa 2 au 3 tu na wapo kaz
 
Hivi kuna sheria inayowaruhusu wanajeshi kutokulipa nauli?

Ina maana hawana kipato cha kuwawezesha kulipa nauli?

Mbona wakienda dukani kwa Mangi hulipa bei kamili?

Kama mimi mwalimu wa shule ya msingi, mimi nisiye na kazi hapa mjini, mimi kinyozi wa salooni huku uswahili, mimi mama ntilie nalipa nauli, kwa hawa jamaa wasilipe?

Hapa nimekaa nao watatu, sisi tunachajiwa nauli, wao wanapiga soga tu, konda amewaangalia kwa unyonge na kuondoka zake.
 
Hao wamezoee vitu vya bure sana, hadi nguo za ndani hupewa bure

Pia hadi pombe hupewa za bei ya bure.

Ni mazoee ya kijinga tu. Hakuna sheria yeyote.

Wazee vya bure
 
Teh teh wadaini muone kama si mnarudishwa mlikotoka sasa hivi!
Hivi kuna sheria inayowaruhusu wanajeshi kutokulipa nauli?
Ina m,aana hawana kipato cha kuwawezesha kulipa nauli?
Mbona wakienda dukani kwa Mangi hulipa bei kamili?
Kama mimi mwalimu wa shule ya msingi,mimi nisiye na kazi hapa mjini,mimi kinyozi wa salooni huku uswahili,mimi mama ntilie nalipa nauli,kwa hawa jamaa wasilipe?
Hapa nimekaa nao watatu,sisi tunachajiwa nauli,wao wanapiga soga tu.
Koda amewaangalia kwa unyonge na kuondoka zake.
 
Sijui ilitumika sera gani kupitisha hilo!!Hivi huwa kuna mahali hiyo kanuni/sheria/taratibu/sijui ni nini ilipoandikwa au??
 
wana kipigo ki kali hao uyo kondakta alivyo wa angalia ki unyonge mpaka raha dizaini kama na muona vile.
 
Lakini kumbuka kuwa wametoa uhai wao kwa ajili yenu ninyi kuwa salama, hivyo sioni kama kuna tatizo endapo wasipotoa nauli ukilinganisha na kazi wanayoifanya.
 
Back
Top Bottom