je ni sahihi kwa waziri mkuu kupanga kukutana na madaktari siku ya ibada??

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
wakuu naomba kusikia maoni yenu kuhusu hatua ya waziri mkuu kupanga mkutano na madaktari siku ambayo ni mapumziko na siku ya kufanya ibada.je waziri mkuu haeshimu uhuru wa kuabudu wa madaktari?usahihi wa suala hili uko wapi?
je uhalali wa kufanya makubaliano na serikali siku ambayo officially sio siku ya kazi uko wapi?wanasheria mpoo??
 
wakuu naona bado mnatafakari.basi tutafakari pamoja ili tuje na majibu sahihi.
 
...kila siku ni siku ya ibada, labda kama unazungumzia kundi maalum. Kwa mtizamo wangu siku si tija ila maudhui ya mkutano husika. Hata Yesu aliponya siku ya sabato.
 
Serikali haina dini na ndiyo maana shughuli zake huendeshwa bila kujali ni siku gani.... hata hivyo ratiba iliyokuwa imepangwa ilikuwa inatoa nafasi kwa watu kusali asubuhi.
 
Nafikiri ni siku muafaka,kwa kuwa wagonjwa wanateseka,muhimu aje na suluhisho utatuzi/ufumbuzi upatikane hali ni mbaya sana
 
wakuu naomba kusikia maoni yenu kuhusu hatua ya waziri mkuu kupanga mkutano na madaktari siku ambayo ni mapumziko na siku ya kufanya ibada.je waziri mkuu haeshimu uhuru wa kuabudu wa madaktari?usahihi wa suala hili uko wapi?

Majibu uliyopata yanakutosha ..... serikali haina siku katika utendaji kazi wake, hata magwanda leo wengine wako Zanzibar, Mzumbe na Ali maua kumwaga sumu ya kuchaguliwa kushika dola 2015. Siku siyo sababu na ninakukumbusha tu kuwa kila siku ni ya sala mzee.
 
Nafikiri ni siku muafaka,kwa kuwa wagonjwa wanateseka,muhimu aje na suluhisho utatuzi/ufumbuzi upatikane hali ni mbaya sana
tumeanza kutangaziwa kuwa wagonjwa wanateseka kuanzia lini?
 
Jamani watanzania hatuwezi tukaacha jambo lipite tu? Whats the Big deal? Mambo mangapi huwa yanafanyika Siku za ibada na watu hawaongei? By the way this is an emergency.
 
Majibu uliyopata yanakutosha ..... serikali haina siku katika utendaji kazi wake, hata magwanda leo wengine wako Zanzibar, Mzumbe na Ali maua kumwaga sumu ya kuchaguliwa kushika dola 2015. Siku siyo sababu na ninakukumbusha tu kuwa kila siku ni ya sala mzee.
kwa nini hatuendi kazini siku za jumapili na siku nyingine kama za christmas n.k
si kuna siku tuliwahi kupinga mkataba ulioingiwa siku ya jumamosi?
 
swali lako linafanana na swali aliliolizwa nabii Issa bin Mariam na Mafarisayo miaka 2000 iliyopita. "walimuuliza, wakisema je ni halali kuponya watu siku ya ibada(sabato)?" Akawajibu ni yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asIyemshika na kumuopoa? Je mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi?. Kwa maana iyo ni halali kutenda mema siku ya ibada (Mathew 12:1-14).

Tuludi kwenye mada iliyomezani,je tendo analotaka kufanya Pinda leo la kukutana na madaktari linatofauti gani na huu hujumbe wa miaka elfu mbili iliyopita? Tafakari!!!
 
Kwa mujibu wa biblia kwani siku ya ibada ni lini?
 
mkuu huu mfano ni tofauti kabisa!! je huyu kondoo aliingia shimoni siku ya sabato??kwa nini hakutolewa shimoni mpaka tusubiri sabato imefika ndo tunajidai tunahangaika.swali langu linabaki palepale kuna usahihi wowote wa kukutana na madokta jumapili?
 
Hii thread ilitakiwa ipelekwe Chit Chat maana huko ndipo ambapo ingejadiliwa vizuri! mleta mada ana akili za ki-chit chat!
 
Hii thread ilitakiwa ipelekwe Chit Chat maana huko ndipo ambapo ingejadiliwa vizuri! Mnalete mada ana akili za ki-chit chat!
rudi kule kule chit chat kwa sababu sio mtu makini kabisa.hata unachokiandika hukielewi.
 
Back
Top Bottom