Je, ni sahihi kwa nchi moja moja za kiafrika kuota Maendeleo? Je, sio kujidanganya?

Mheshimiwa Jingalafalsafa inaelekea hujachukua muda wako mwingi kutafakari kunijibu. Kwa Afrika kuwa moja hiyo ni ndoto isiyoweza kutimia kwa sasa mpaka nchi mojamoja kutengeneza solid foundation katika nchi zao. Wawe womoja, wazalendo na wenye kujitambua kama Taifa moja moja wakifikia hatua hiyo ya kujitambua kwao kama Taifa hapo ndipo watakapo kuwa na uwezo wa kujiunga na kuwa kitu kimoja.

Huwa napenda kusema hivi "TEMESHAZIKWA HAI, SASA TUSIWAACHE WATOTO/VIJUKUU VYETU VIKUTWE NA HAYA YETU, TUWAFANYIE JAMBO"
Kamwe sijawahi kuamini kuwa Afrika inaweza kuungana leo au kesho! HATA SIKU MOJA! Na ikitokea hivyo, basi NITAKULA KIAPO CHA MIAKA 10 KAMA ITADUMU AU NIFE. Lakini...HILO HALITETERESHI UKWELI WA MAMBO KWAMBA, BILA AFRIKAMOJA, WATU WAKE WATAENDELEA KUWA WANYONGE KIZAZI HADI KIZAZI. Yupi ni mzazi bora? Je, si yule ampandiaye mnazi mwanae japo mwenyewe hatokula?
Napenda nijulikane kama Mwanaafrika, napaswa kujivunia Afrika kwanza kabla ya Tanzania! Mzalendo wa Afrika, ni tofauti sana na mzalendo wa Tanzania au Kenya! Mzalendo wa Uganda Amin alipigana vita na Mzalendo wa Tz, Nyerere 1978! Kumbe basi, "KADRI TUNAVYOWAFUNDISHA WATU WETU KUWA WAZALENDO WA VITAIFA VYAO,NDIVYO TUNAVYOUKIMBIA UMOJA NA KUJENGA MIPAKA YENYE UADUI, CHOYO, HILA, VISASI, TAMAA, n.k baina yetu WAAFRIKA, vinavyojengwa na dhana, SISI na WAO, UMIMI-UBINAFSI! Uzalendo wa Kenya au Tanzania Ukikomaa, ndivyo Uadui navyo unavyokomaa, mwishoe ndivyo Afrika inavyomeguka na ndio shuka la unyonge wetu hilo! TUTAFIKA KWELI!?
Uzalendo ni kumfundisha Mtanzania kwanza kuwa yeye ni Muafrika sawa na yule wa Kenya, Uganda, Ghana, Botswana, n.k Chochote afanyacho anatakiwa Atangulize Uafrika wake kwanza! Mkenya akiwa hivyo, Mtz na wengineo, Afrikamoja itajongea! Hilo ni suala la FIKRA, ni rahisi sana kubadili tabia ya mtu lakini sio FIKRA! Kwa kutambua hilo ndio maana nasema, SIO KAZI RAHISI...LAKINI NDIO NJIA PEKEE...NA INAWEZEKANA!
Sasa hivi imekuwa jambo la kawaida kusikia Nchi fulani ya Afrika imesaidia silaha waasi wa nchi nyingne ya Afrika! Wako sahihi, kwani wameapa kuitendea chochote nchi yao ni wazalendo, UAFRIKA UMEWEKWA PEMBENI, UTAZUIA VIPI HAYO?
Mungu wetu anaita sasa!
 
Nanukuu:

"Kinachojenga Taifa ni elimu, ni maadili yanayochangiwa na kila mmoja ndani ya jamii; ni mitazamo inayoshabihiana miongoni mwa wanajamii; ni tabia na haiba. Yote haya hufundishwa kupitia elimu iliyoasisiwa na kuendelezwa na jamii husika, si na waziri wala rais, bali na wanajamii walioafikiana juu ya aina ya elimu ya kuwapa watoto wao na aina ya elimu ya kuirithisha toka kizazi hadi kizazi.

Tukishindwa kulielewa hili, kama ambavyo naona tumeshindwa, basi tuelewe kwamba hatujengi taifa moja. Iwapo tumekubali kwamba kila anayeweza ana hiari ya kuwafundisha wanawe kadri anavyojua, basi tuelewe kwamba tunajenga mataifa mengi ndani ya nchi moja, na tutambue kwamba iko siku mataifa haya hayataiva ndani ya chungu kimoja."

Jenerali Ulimwengu, Raia Mwema, Februari 20 - 26, 2013, uk.7,Elimu tofauti zitazaa mataifa tofauti, na hayataiva chungu kimoja.
 
Matukio yanayotokea nchini, mabishano yaliyopo mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kama JF, tension zinazokua kila siku, serikali iliyoacha mambo yajiendee kama yanavyotaka, ndio yamenifanya nimnukuu Jenerali hapo juu, namheshimu sana huyu mtu.

Tumeukubali ujinga kuwa sehemu ya jamii yetu basi tukubaline na yote yaletwayo na ujinga.

Moja ya viashilia vya ujinga ni, kutojitambua, hapa ntagusia hilo tu.
Nauona ugumu wa watanzania kujitambua na kuutambua utanzania wao achilia mbali uafrika. Hawajitambui wao ni nani ndani ya nchi yao wala nafasi yao ndani ya Afrika. Wamekua wakijitambulisha kwa makundi ya dini, chama, elimu n.k, wanaojitambua kama waafrika na watanzania ni wakuhesabu siku hizi. Na mtu asiyeweza kujitambua huwezi kumuhubiria uwajibikaji, sahau.

Nani anaitambua Afrika na anatambua uafrika wake katikati ya watu wanaouana wakigombania kuchinja nyama? Tumefungwa na minyororo ya ujinga wa mapokeo ya mabwana zetu wa kikoloni mpaka tunauana wenyewe kwa wenyewe? Tumefika huku Tanzania?
Na kwenye hili hatupo peke yetu, wapo ndugu zetu wa Mali, Nigeria, Sudan, Kenya, wote tunatiana pembe kuwa "impress" mabwana wetu wa kikoloni.

Huyu ndio mwafrika wa Tanzania ninayemuona, Mwafrika anayeitelekeza elimu kwa kasi, Mwafrika anayesubiri kufanyiwa kila kitu na mabwana zake wa kikoloni, anayetaka mwongozo hadi kwenye imani, anamuua mwafrika mwenzake kwa jina la mungu wa mashariki ya kati.
Mwafrika wa Tanzania anamwogopa mwafrika yoyote yule anayempita kidogo maarifa, muulize mtanzania yoyote kuhusu jumuiya ya afrika mashariki, wengi wao watakwambia wanaogopa wakenya watachukua ajira na ardhi yao. Wakati mwafrika wa Rwanda anatia juhudi katika elimu, mwafrika wa Mali anataka kujigawa katika makundi ya dini, mwafrika mwingine wa Afrika kusini anamchoma moto mwafrika mwenzake kwa sababu anakuja kuchukua ajira zao kwa makaburu. Hii ndio afrika ya leo.

Tusipowekeza katika elimu, afrika inarudi mikononi mwa mkoloni,tofauti ya zamani na sasa ni kuwa safari hii tutawaita na kuwakabidhi wakoloni ardhi, vichwa na mioyo yetu sisi wenyewe, kwa sababu kiwango chetu cha ujinga ni kikubwa kuliko kile cha mababu zetu!
 
Ni ngumu sana kupata Afrika moja sasa!
Hapa ndipo ninapo ungana na Kwame Nkrumah,na kutofautiana na baba wa taifa mwl. Nyerere.
Wazo la Nkrumah lilikuwa,"Ni muhimu mataifa ya Afrika yakaungana sasa {Kipindi kile cha 1960s} kabla ulafi na u mimi haujajengeka miongoni mwa nchi za kiafrika."
In contrast,Mwalimu Nyerere yeye alisema "Muungano wa kiafrika uanze na muungano wa kikanda katika kanda mbalimbali,na baada ya miungano hiyo kufanikiwa,ndipo Afrika nzima iungane".
Sasa tunaona miungano ya kanda kama SADC,ECOWAS,EAC etc imekuwa dhaifu,huku kila raia wa nchi husika wakijenga uzalendo kwa nchi zao,na hivyo muungano wa Afrika kuwa kitu kigumu kutekelezeka kwa sasa.
Bado tuna safari ndefu.
 
Asante Mkuu wangu Mourinho. Hakika umenena kilicho bora kabisa! Na kinatia mwale wa moto moyoni hakika! Pamoja sana.
ELIMU NA KUJITAMBUA. Kujitambua ni kuijua thamani yako halisi unayoistahili ama kuwa nayo. Thamani ya mtu hujengwa na MAZINGIRA na NYAKATI halisi za eneo alilopo mtu. Ajitambuae ni yule mwenye ufahamu wa eneo alilopo, mazingira yake na nyakati zake mahususi kwa eneo hilo, mwishowe atambue na kuishi WAJIBU wake kulingana na mazingira na nyakati mahususi za eneo husika.
Tafsiri kuu ya kwanza ya maisha ni FURAHA, kila mtu anataka kuishi ili afurahie. Kama umezaliwa ukakuta jamii yako ina Furaha, basi ni wajibu wako kuitunza furaha hiyo kulingana na mazingira na nyakati za eneo hilo. Lakini kama umezaliwa ukakuta jamii yako inalia, basi wajibu wako ni kuinyamazisha na kuwapigania kuipata furaha yao ya kweli wanayostahili kulingana na Mazingira na Nyakati zao! FURAHA ya kweli ni zao la mahusiano sahihi yaliyopo baina ya Mazingira na Nyakati mahususi kwa eneo husika. Mahusihaono hayo sahihi mimi naita MANTIKI, yaani UTU/KUFIKIRIANA.
Ili kujenga hayo, ndipo Elimu inapochukua nafasi yake. Hakika mkuu wangu, Elimu ni nyenzo bora kabisa katika kujitambua. Ikumbukwe tu kuwa, elimu si kuingia darasani tu na kumaliza vidato hadi kuitwa Prof. ama mheshimiwa. Ila, Elimu ni ule uwezo alionao mtu wa kutambua mambo, kuyameng'enya na kutolea maamuzi sahihi, mwishowe kuyawajibikia yaani kuchukua hatua zinazostahili. Hiyo ndio elimu! Uwezo huo haujengwi darasani tu, bali hujengwa na kila kitu tukionacho, kukisikia, kukihisi, kukitafakari, kuonja, nk. Kwa kifupi ni experiences zote tuzipatazo kupitia milango yetu yote ya fahamu! Vyote hivyo vina nafasi sawa katika kum-shape binadamu na uwezo wake.
Muhimu sasa ni kujiuliza, je Mazingira na Nyakati zetu zinashabihiana kwa kiwango gani? Kama ni kwa kiwango kikubwa, basi ni lazima experiences zetu nazo zihusiane kwa kiwango kikubwa. Binafsi sijaona kutofautiana sana kinyakati wala kimazingira kwa waafrika. Watu weusi TUNAFUNGANA VIKUBWA SANA KULIKO VILE TUNAVYOTOFAUTIANA. Cha ajabu sasa, Mazingira yaleyale, nyakati zilezile, lakini different experiences, hili ni JANGA. Mfano ni hapa kwetu Tz. Tangu kusini-kaskazini, mash-magh kimazingira na nyakati tunafungamana, lakini hao hao, kuna wa international schools na zetu St. Kayumbas, kuna First Class na sie Kajamba nani hospitalini, tena ya serikali. Kuna wa Mwanza na Singida, Dar na wa Lindi, Osterbay na wa Tandale, kuna wa Mungu allah na Jehovah, kuna wa juu ya mkeka na sofa, kuna wa Prado na wa pekua, kuna wa viraka mvua na jua, na wa kiyoyozi, kuna wa uvundo na wa marashi, kuna yule aonaye masikini kila siku, na yule ashindaye sehemu ghali kila siku, kuna yule atafakariye atapataje panado ya mwanaye mkekani na kikombe cha uji na yule wa kutafakari hoteli gani akale na watoto wake, n.k mbaya zaidi JAMII IMERUHUSU HAYO NA KUYAHALALISHA NA KUYAONA YA KAWAIDA. Tumesahau kuwa hayo ni mafunzo, maana kila kimuingiacho mtu kupitia milango yake ya fahamu kina nafasi sawa katika ku-shape aina ya mtu. Matokeo ya mafundisho tofauti tofauti, ni kupata wabomoa nchi wengi kuliko wajenga nchi. (.........)
 
...... Hakika, chanzo cha kupata wabomoa nchi wengi, ni kuruhusu mafundisho tofautitofauti, tena yanayokinzana. Tutawezaje kujenga uwezo sawa wa kielimu kwa watu wetu ili wote wawe wajenga nchi na si wabomoa nchi kama leo? Mazingira na Nyakati ni zilezile, lakini experiences tofauti. Tumekosa jambo hapa, kuna jambo limekiukwa katika kuhusianisha mazingira na nyakati, hakuna Uuwiano sahihi kati ya Mazingira na Nyakati zetu, hayashabihiani. Mahusiano yaliyopo ni yale yanashawishi mtu kuvaa kawoshi Makambako! Something misses, that is LOGIC/MANTIKI. Mimi naita UTU. Ili kujenga mahusiano hayo sahihi, ni lazima kuwepo na misingi imara ya kuwajengea watu wetu uwezo huo, binafsi sioni njia nyingine ya kujenga mahusiano sahihi katika jamii ila tu kuyafanya kuwa IMANI KUU ya taifa, taka usitake utafuata tu. Nayo ndiyo ITIKADI KUU ya Taifa. Hii ndio itakayoamua mtoto asikie nini, aone nini, ahisi nini, aonje nini, anuse nini, atafakari nini, ajifunze nini. Hapo ndipo tutakapopata elimu sawa, kama tutaishape kupata wabomoa nchi, basi watapatikana kwa wingi, kama wajenga nchi basi watapatikana. Hilo leo halipo! Ni JANGA na UPUMBAVU. Kuwe na meza mahususi za kutolea mawazo mbadala, sio kuyatoa tu kokote na ku-interrupt yaliyopo!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Mkuu JINGALAFALSAFA, ahsante kwa hoja nzito ulizozimwaga hapa.

Nashukuru tunakubaliana kwamba, kukosekana, kwa elimu, na kama ipo ni elimu isiyosadifu mazingira yetu,
ndio kumetufikisha hapa tulipo. Ngoja nichanganue kidogo hapo.

Hapa kwa kifupi ntaizungumzia ile elimu basic (ya msingi) ya kumsaidia binadamu kujitambua na kutambua mazingira na wakati husika. Azijue mila, desturi, imani na maadili kwa ujumla yanayoitambulisha jamii yake. Aweze kujua simple mathematics, aweze kuandika, kusoma, ajue majira ya mwaka, ajue usafi wa mwili na mazingira yake, ajue kazi za mikono, ajifunze kujieleza na taratibu ajifunze kujitegemea hata kama ni kwa asilimia ndogo. Hii ni elimu ya lazima na haki ya kila mwanajamii.

Ni ya lazima kwa sababu ndio inahakikisha uhai wa jamii husika, kulinda maarifa ya jamii hiyo, kuyaendeleza ili yasadifu mazingira na wakati na kuyarithisha kwa vizazi vijavyo. Ndio maana inakua ya LAZIMA na ni HAKI ya kila mwanajamii.

Lakini Elimu yetu haisadifu mazingira na wakati wa jamii yetu, sio zao la tamaduni na falsafa (kama ipo) ya jamii yetu, kwa maana nyingine hakuna mantiki katika elimu inayotolewa kwenye jamii zetu. Kazi kubwa inayofanya ni kutufanya tujichukie na tudharau UTU wetu na tupende na kukumbatia tamaduni za watu wengine hasa wazungu na waarabu.

Kingine ni kuwa hii elimu haina uwiano kati ya nidhamu moja na nyingine, ngoja nitoe mfano hapa;
Mtoto yuko kwenye somo la historia, anafundishwa kuhusu utumwa na ukoloni, anaambiwa kati ya vitu vilivyosababishwa Afrika ikatawaliwa ni dini. Akiwa kwenye somo la imani na kuabudu ( dini) anafundishwa kwamba kabla ya mkoloni, mababu zetu walikua wajinga, hawakumjua "mungu wa kweli" bali waliabudu mawe na miti.
Imagine ni nini kinamwingia mtoto huyu kichwani, je tunaweza kusema bila ya wasiwasi kwamba anapata Elimu hapa? Baadae anatoka shule hadi chuoni akiwa mpumbavu, akidhani kuelimika ni kudharau tamaduni za jamii yake na kujitahidi sana kuwa kama mzungu wa Ulaya na Amerika.

Sasa kama elimu haisadifu mazingira na wakati wa jamii husika, tunaweza kuiita elimu at all? Ina msaada gani na jamii yetu? Na kwanini bado tumeikumbatia?

Hebu tuwaangalie wenzetu wa mashariki ya mbali, China, Japan, Singapore, Malaysia, mbona wapiga hatua na wanapata heshima ya UTU wao mbele ya dunia bila ya kutupa, kukashifu wala kudharau tamaduni zao?
Mturuki anapata shida sana kuwa mwanachama halali wa EU kwa sababu moja tu, utamaduni na falsafa yake inakinzana sana na tamaduni na falsafa za wanachama wengine. Na hapo ndio utajua hata kwa hao walioendelea bado utamaduni na falsafa ya jamii husika unaplay party kwenye maamuzi makubwa kama hayo, ila Afrika hailioni hilo.

Kwa hiyo pamoja na kutambua kwamba elimu ndio itatutoa hapa lazima pia tutambue aina ya elimu tunayoitaka, elimu isiyosadifu mazingira na wakati wetu haiwezi kamwe kuikomboa Afrika, kuna haja za kuifikiria upya hii kitu tuiita elimu kwa manufaa ya mwafrika na Afrika!
 
Ni ngumu sana kupata Afrika moja sasa!
Hapa ndipo ninapo ungana na Kwame Nkrumah,na kutofautiana na baba wa taifa mwl. Nyerere.
Wazo la Nkrumah lilikuwa,"Ni muhimu mataifa ya Afrika yakaungana sasa {Kipindi kile cha 1960s} kabla ulafi na u mimi haujajengeka miongoni mwa nchi za kiafrika."
In contrast,Mwalimu Nyerere yeye alisema "Muungano wa kiafrika uanze na muungano wa kikanda katika kanda mbalimbali,na baada ya miungano hiyo kufanikiwa,ndipo Afrika nzima iungane".
Sasa tunaona miungano ya kanda kama SADC,ECOWAS,EAC etc imekuwa dhaifu,huku kila raia wa nchi husika wakijenga uzalendo kwa nchi zao,na hivyo muungano wa Afrika kuwa kitu kigumu kutekelezeka kwa sasa.
Bado tuna safari ndefu.

Hakika Mkuu wangu Mpenda Yesu, ni ngumu sana kupata Afrikamoja kwa sasa. Na nafasi bora kabisa tulishaipoteza, ni ile iliyopendekezwa na Kwame na Nyerere akaipinga....lilikuwa kosa kubwa linalotugharimu leo.
Nafurahia unaposema kuwa tuna safari ndefu sana, kwani naona imani uliyonayo kwamba japo ni kazi ngumu sana, lakini "AFRIKAMOJA INAWEZEKANA". Na huo ndio ukweli, na ndio SULUHU PEKEE YA UNYONGE WETU. Tutambue tu kwamba, sisi si kitu tena, TUMESHAZIKWA HAI NA TUMEOZA TAYARI TUNANUKA. Hivyo haka kachembe kadogo ka uhai kalichobakia, ni fahari kwa mzazi mwema kukatoa sadaka kwa watoto wake!
AFRIKAMOJA I MIKONONI MWETU LEO.
Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU. Mantiki haijawahi kufa, na kamwe haitakufa. Kama Harakati za AFRIKAMOJA ni MANTIKI, hakika ITASIMAMA. Kila mtu na apime uzito wa hilo, kisha atuambie kama ni MANTIKI ama UBATILI. Kama ni MANTIKI, anza mara moja kuishi hilo. Hata kwa kuanza kuamini tu.
Mungu wetu anaita sasa! A4AFRIKA!
 
Vyema Mkuu Mourinho! Na hiyo ndio sifa kubwa ya Elimu, Kusadifu Mazingira na Nyakati katika eneo fulani.
Katika hilo yatupasa kutafakari juu ya Elimu na Maarifa na Mafunzo. Binafsi, Elimu ni Maarifa ambayo mtu hujifunza tangu kuzaliwa kwake. Lakini si kila maarifa ni Elimu. Maarifa ni zao la kujifunza/mafunzo. Lakini ni ukweli kwamba si kila ajifunzacho mtu ni mahususi kwa Mazingira na Nyakati ya eneo alipo na atakalo fanyia application ya mafunzo yake. Mfano, ikitokea mtu yuko jangwani, akajifunza namna ya kuvua samaki atapata maarifa ya kuvua samaki, lakini si Elimu "NO RELEVANCE", kwa maana ili maarifa yawe Elimu ni lazima maarifa hayo YASADIFU watu, sura yao ya nchi, mahusiano yao kwa maana ya imani, tamaduni n.k. Elimu ni maarifa yanayosadifu Mazingira na Nyakati za eneo husika. Ndio maana tunasema Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Elimu ni msaada kwa mwanadamu kukabiliana na maisha. Ndio maana ujuzi wa kuvua samaki jangwani au kulima mahindi si Elimu kwa maana hauna msaada.
Leo hii, tulichonacho ni MAARIFA tu, si ELIMU ndio maana haijawa ufunguo wa maisha yetu. Tu WANYONGE bado. Maarifa haya tufundishwayo, labda ni elimu kwa wenzetu lakini sio sisi, kwetu ni UBATILI NA UPUUZI MKUBWA.
Ni wajibu wetu kuchambua maarifa yatufaayo, hakika yaliyopo YAMEOZA na hayatatufikisha.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Vyema Mkuu Mourinho! Na hiyo ndio sifa kubwa ya Elimu, Kusadifu Mazingira na Nyakati katika eneo fulani.
Katika hilo yatupasa kutafakari juu ya Elimu na Maarifa na Mafunzo. Binafsi, Elimu ni Maarifa ambayo mtu hujifunza tangu kuzaliwa kwake. Lakini si kila maarifa ni Elimu. Maarifa ni zao la kujifunza/mafunzo. Lakini ni ukweli kwamba si kila ajifunzacho mtu ni mahususi kwa Mazingira na Nyakati ya eneo alipo na atakalo fanyia application ya mafunzo yake. Mfano, ikitokea mtu yuko jangwani, akajifunza namna ya kuvua samaki atapata maarifa ya kuvua samaki, lakini si Elimu "NO RELEVANCE", kwa maana ili maarifa yawe Elimu ni lazima maarifa hayo YASADIFU watu, sura yao ya nchi, mahusiano yao kwa maana ya imani, tamaduni n.k. Elimu ni maarifa yanayosadifu Mazingira na Nyakati za eneo husika. Ndio maana tunasema Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Elimu ni msaada kwa mwanadamu kukabiliana na maisha. Ndio maana ujuzi wa kuvua samaki jangwani au kulima mahindi si Elimu kwa maana hauna msaada.
Leo hii, tulichonacho ni MAARIFA tu, si ELIMU ndio maana haijawa ufunguo wa maisha yetu. Tu WANYONGE bado. Maarifa haya tufundishwayo, labda ni elimu kwa wenzetu lakini sio sisi, kwetu ni UBATILI NA UPUUZI MKUBWA.
Ni wajibu wetu kuchambua maarifa yatufaayo, hakika yaliyopo YAMEOZA na hayatatufikisha.
Mungu wetu anaita sasa!

Heshima kwako mkuu!
 
Najaribu kuumiza kichwa, aje sisi watu weusi tunaweza kuondokana na UNYONGE tulionao, lakini nimeshindwa na sioni njia wala suluhu yoyote kama hatutakuwa WAMOJA. Hii inajenga imani yangu kuwa, AFRIKAMOJA si muhimu tu bali ni LAZIMA. Inaweza kuwa ni ndoto kwa sasa, lakini heri yake aotae hivyo kuliko yule AJIDANGANYAE ustawi wetu unawezekana nje ya umoja huo!
Naamini katika UKOMBOZI WA FIKRA kama msingi mkuu wa kuleta mabadiliko yoyote, vilevile ninaamini katika mambo makuu matatu muhimu katika ku-shape FIKRA HAI kwa watu wako, nayo ni ELIMU, SANAA na HABARI. Kama unataka kujenga watu wazembe basi wewe pandikiza uzembe au hubiri uzembe kupitia mambo hayo, ndani ya miaka 5 utaona matokeo yake.
Napenda kuitazama nafasi ya elimu leo, aje tunaweza kutega HESABU zetu katika elimu kuifanya ijenge FIKRA tunazozitaka kwa wahusika wote za kwamba "AFRIKAMOJA LAZIMA" ili kuumaliza Unyonge wetu.
Katika hilo, japo ni ka-element kadogo sana, lakini kakitegwa vizuri na kuchezwa vizuri, kana nafasi nzuri ya kujenga FIKRA tutakazo kwa watu wetu, ninawaza hivi wakuu wangu katika elimu... Aje kama tutakuwa na japo SOMO moja ambalo litasimamiwa na AU na kuingizwa katika mitaala ya elimu ya nchi zote za Afrika na kufundishwa kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ya juu, na liwe ni somo la lazima kwa kila mwanafunzi katika ngazi zote nchi zote? Somo hilo libebe Falsafa kuu ya UAFRIKA WETU, Fahari yetu kama wamoja, wajibu wetu kama ndugu, haki zetu kama wajamaa, nguvu na imani yetu, nafasi yetu katika umoja wetu, ibebe kila kifaacho katika kujenga "FIKRA za AFRIKAMOJA LAZIMA na INAWEZEKANA", vipo vingi sana, muhimu ni kila mwanafunzi regardless nchi aliyopo atafundishwa hicho kulingana na ngazi aliyonayo, kwa kuwafanya wasome kitu kimoja tu, ni hatua nzuri ya kujenga the spirit of Unity. Somo liweje, lifundishweje, ni hatua nyingine ila muhimu kwanza, ni wazo la kuwa na somo litakalolenga kujenga FIKRA kwa watu weusi wote ya kuwa AFRIKAMOJA LAZIMA na INAWEZEKANA. Majukwaa ya siasa HAYATOSHI tena hayana uwezo huo!
Katika kufanikisha hilo kuna adui mmoja mkubwa sana, ambaye anaweza kukwamisha hilo, naye ni dhana ya HURIA-demokrasia. Tangu unapoanza kutafakari wazo hili, popote utakapoliwekea mizani ya kihuria ama demokrasia, UMESHALITUPA TAYARI. Ninawasilisha....
Mungu wetu yu tayari kutupigania. Anaita sasa!
 
'Time Will Tell' What is the time? Why should it be the one to tell? Je si FIKRA zi-shape-zo Muda? Je, muda si FIKRA!? Kipi kinachoamua chini ya Jua? Je, si FIKRA? Nani hana hizo Fikra? Muda ni FIKRA, na tuzifanye kuwa moja leo, ili zisikwaruzane na tufikie maamuzi!
Hatuwezi kujisubiri wenyewe... "WE ARE THE TIME TO MAKE DECISION" "We are the Time to Tell, lets make it"
anaita sasa!
 
JingalaFalsafa hebu soma kwanza historia. Anzia na League of Nations kisha rudi hapa tuongee.

Nani kakuambia sisi wanyonge?

Vyema Mkuu MwanaHaki, karibu kumeng'enya ulichoguswa nacho! Muhimu ni kutofungwa na aina yoyote ya urasmi(formality) ila tu Mazingira na Nyakati zetu.
Unyonge wetu ni madhila yanayotusumbua kama watu weusi(vita, magonjwa, njaa, utumwa, wizi, chuki, ukoloni), ndio shuka letu la kila siku tujifunikalo! Lakini, licha ya unyonge huo ambao mtu mweusi anao, ninaamini kwa zaidi ya 100% kwamba, mtu mweusi anaweza kuyashinda! Sisi si wanyonge katika kuondoa Unyonge wetu, ila tu Umoja na Kuthubutu ndiko kunakohitajika! Tukikaa chini kama wamoja, tukaingia katika tafakari/kuumiza vichwa kama waafrika wenye mazingira na nyakati zetu binafsi, basi hakuna njaa, vita, wizi, unyonyaji, mauaji, wala ubinafsi utakaosimama! Uwezo huo upo, hivyo ni kweli sisi si wanyonge! We are strong enough kuondoa unyonge wetu! Ninakubali.
Mkuu wangu, nitaipitia historia hiyo kutambua zaidi kilichomo. Ninakusikiliza ndugu!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom