Je ni sahihi kuweka uzungu kwenye majina ya kikabila?

Ushamba tu watu kuona majina ya kizungu ni mali !

And it is only in Afrika tumecopy kila kitu cha wazungu...angalia China, Japan have kept their names!

Ajabu US/Ulaya hakuna wanaocopy majina yetu!

Ni swala la mindset yetu sisi haswa Waafrika!

Mkuu,
Nimependa points zako.
USA blacks wanajitahidi sana kujipa majina ya kiswahili kama vile "Tukijaaliwa" Malaika n.k.japo hawabadilishi yale majina ya kizungu na kuyaandika kiswahili.
 
Ndugu zangu majina ya kikabila ni yapi? Uliyoyataja mwazilishi wa mada hii sijui niyaite ya kiswahili au ya kikabila? Sina jibu.

Ninachoweza kusema ni ulimbukeni tu kubadili majina na kujiita majina unayoyataka. We waache wabadili majina, kuna siku yatawatokea puani. Kuna jamaa mmoja alikuwa na mtindo wa kujiita majina anayotaka, yeye ni Matayo. Alitumia jina hili akiwa shule ya msingi na sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne, pia cheti cha kuzaliwa kina jina la Matayo. Alipoanza kidato cha tano, akajua kimombo kidogo, akajiita Matthew, alipomaliza akapata nafasi ya masomo nje ya nchi, alipoenda uhamiaji kutaka passport akaandika Matthew. siku ya siku alipotakiwa kupeleka cheti cha kuzaliwa na passport, hapo ndipo jasho lilipomtoka hadi kwenye nywele. Safari hakwenda na nje hakwenda hadi sasa. Badili majina kama nguo, kuna siku utajua kubadili majina ni nini?

BYE
 
Waungwana,
Kuna kitu kimekuwa kinanitatiza kwa kipindi kirefu. Kitu hiki kinahusu kugeuza majina ya kikabila na kuyapa uzungu bila sababu za msingi.Labda kuna sababu ambayo siijui. Inakuwaje kwa mfano mmaasai anayeitwa Laiza kugeuza jina na kujiita " Laizer/Laiser", au mchaga anayeitwa Hoi-se na kujiita "Hoyce"..
wapo pia wale wanaoongeza "s" mwisho wa majina yao kama "Mnzavas", "Matingas" au kugeuza kabisa jina kama vile Juma kujiita " "Jimmy"
Inakuwaje hii? watu wanaonea aibu majina yao au wanafikiri kuyapa nakshi ya kizungu/kigeni ndio ujiko?Nahitaji somo hapa.

Ki ukweli hali kama hiyo sio katika majina tu ukingalia mazingira yetu yote kutokea miaka ya mwisho ya 80 na kufikia hapa tulipo tumekuwa tukibadilika kwa kasi sana ikiwa majina au mazingira na utamaduni na madili kitu ambacho binafsi nahofia hukousoni siku za mbele tunaweza kuja kujuta kama vile wanavyopiga kelele baadhi ya wamarekani weusi na kulalamika kuwa wamebadilishiwa kila kitu ambacho kilikuwa chao na kupewa cha watawala wao walikuwa na maana kama vile majina utamaduni NK lakujiuliza kwetu sisi sote jee tupo tayari kubadilisha utamduni wetu wa kiafrika na kitanzania tuwe kama wazungu itakuwaje itakapofika wakati hatuna utamaduni na mila zetu na kulizwa swali kama vile hivi nyinyi WATANZANIA utamaduni wenu ni upi hasa ??naimani kuna baadhi yetu mtatowa ufafanuzi zaid
 
Nchi za wenzetu kama Denmark na Norway state ina interest na majina..yaani mtoto kumpa jina lazima liendane na majina yao..laa sivyo mtoto hatapewa jina! Ili kuhifadhi utaifa na tamaduni zao!

Angalia majina yao...Hansen, Oystein, Harald, Christiansen, Knut n.k. Yaani ukipeleka jina kama Bahati, Shida hayatakubaliwa!

Kwa hiyo ni sera ya nchi!
 
Hata waandishi wa habari wanachangia kuvuruga jinsi majina yanavyotakiwa kuandikwa. Kwa mfano, mimi huwa sioni sababu ya gazeti kuandika "Machuppa" badala ya "Machupa", sasa hata Machupa inahitaji iwekewe double p? Kuna mengi tu, kama Pawassa, Wassira, EL naye wanamuwekea double s, etc. Usishangae siku moja Rwechungura ikaandikwa Rwechungurra !!

Opaque,
Hii tabia ya kubadilishabadislisha..kuna siku tutajikuta tumepoteza kila kilicho chetu...kuanzia rasilimali hadi lugha zetu! Watu wanachukulia juu juu hii ishu.

Nilikuwa pia naangalia ukuaji wa kiswahili kila siku.... nikajikuta nashangaa jinsi wataalamu wetu wamekaa kukumbatia maneno ya kigeni kujaa katika lugha ya kiswahili kama vile chanzo cha maneno ni ama kiarabu au kiingereza.Kuna hili neno kwa mfano " mihadarati".Hivi katika lugha zetu Tanzania hakuna neno lingeweza kuchukuliwa na kuwekwa kwenye kiswahili? Najua kwa mfano "bangi" ni zao haramu linalolimwa katika mikoa mbalimbali Tz na kwamsingi huo, kutokana na sifa ya kuwa na ulevi,lazima maeneo husika yangekuwa na neno lenye maana sawa na mihadarati.Wataalamu wetu hebu wajitahidi tusipoteze kila kitu.
Kwenye majina..pamoja na kuwa tuna uhuru katika hili..nadhani ni wakati muafaka tuwe wazalendo zaidi tujitahidi kulinda kilicho chetu.Sipingi watu kujiita mfano "Grace" badala ya "Rehema","Moses" badala ya "Musa","Precious" badala ya "Aziz/Aziza" etc..lakini basi pale nitakapotaka kujiita "Muhogo" mchungu nisibadili na kuandika " Muhogow" maana haileti maana yoyote!
 
Nadhani wengi mtamkumbuka Mobutu. Alizaliwa na kuitwa Joseph-Désiré Mobutu, lakini katika utawala wake akaamuru watu wa nchi yake wabadili majina kutoka ya kizungu na kuwa ya kiafrika, na kwa kuanzia yeye mwenyewe akajiita Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga, na nchi yake ikaitwa Zaire badala ya Belgian Congo, huku makao makuu yaliyokuwa yakiitwa Leopoldville yakichukua jina la Kinshasa.
 
Waungwana,
Kuna kitu kimekuwa kinanitatiza kwa kipindi kirefu. Kitu hiki kinahusu kugeuza majina ya kikabila na kuyapa uzungu bila sababu za msingi.

Sijui ni Inferiority complex ama low self esteem? Huko ughaibuni hasa Marekani haka ka-ugonjwa kanawasumbua walio wengi, zaidi wanawake na hawaishii katika kubadili majina tu bali utamaduni wao wote!! Kuanzia mikorogo, mawigi ya kizungu, mavazi, vyakula nk. utakuta mtu anatumia almost income yote anayoipata katika ku-maintain stupid life style na ndio anamaliza miaka na mfukoni hana senti tano!
wenzetu Waganda na Wakenya wao wana afadhali kidogo.
 
Hii ni kali!
 
Ksababu kubwa mbili za kubadilishiwa jina.

Mfano mimi mwenyewe nilibadilishiwa jina na walimu wangu nilipoingia darasa la kwanza, niliongezewa herufi nne hivyo kuwa na jina tofauti na nililobaitizwa nalo. So inawezekana wengine wetu walibadilishiwa katika uandikisho katika shule tulizosoma.

Pili inaweza kuwa sababu ya kutaka liwe la kizungu zungu hivi na hapa ndio wapo wengi mfano

Amina =Emmy
Bakari= Becker
Lazaro= Laiser, Lazarus e.t.c
Feruzi= Ferrous
Jaklini = Jackline
Haruni = Aron
Said = Side
Jumanne= J4
Chausiku =Siku ama Chiku

the list is long.....

Na tatizo kubwa lipo kwa vijana wetu wa bongo flavour na wasanii wengine.
wanadhani majina yao hayatamkiki ama hayavutii so either wanabadilisha ama wanaishia kujipa majina mengine yanayofanana fanana na uzungu.

Kama tunataka kumaliza hili tatizo tuanze na wasaniii
 
Opaque,
Hii tabia ya kubadilishabadislisha..kuna siku tutajikuta tumepoteza kila kilicho chetu...kuanzia rasilimali hadi lugha zetu! Watu wanachukulia juu juu hii ishu.

Nilikuwa pia naangalia ukuaji wa kiswahili kila siku.... nikajikuta nashangaa jinsi wataalamu wetu wamekaa kukumbatia maneno ya kigeni kujaa katika lugha ya kiswahili kama vile chanzo cha maneno ni ama kiarabu au kiingereza.Kuna hili neno kwa mfano " mihadarati".Hivi katika lugha zetu Tanzania hakuna neno lingeweza kuchukuliwa na kuwekwa kwenye kiswahili? Najua kwa mfano "bangi" ni zao haramu linalolimwa katika mikoa mbalimbali Tz na kwamsingi huo, kutokana na sifa ya kuwa na ulevi,lazima maeneo husika yangekuwa na neno lenye maana sawa na mihadarati.Wataalamu wetu hebu wajitahidi tusipoteze kila kitu.
Kwenye majina..pamoja na kuwa tuna uhuru katika hili..nadhani ni wakati muafaka tuwe wazalendo zaidi tujitahidi kulinda kilicho chetu.Sipingi watu kujiita mfano "Grace" badala ya "Rehema","Moses" badala ya "Musa","Precious" badala ya "Aziz/Aziza" etc..lakini basi pale nitakapotaka kujiita "Muhogo" mchungu nisibadili na kuandika " Muhogow" maana haileti maana yoyote!

Lugha ya Kiswahili ni lugha yenye maneno ya Kiarabu,Kiingereza,Kihindi,Kireno n.k.Kwa mfano neno "mihadarati "limeopolewa kutoka lugha ya Kiarabu.Umeona ingelikuwa bora kutumia neno "bangi" lakini hata hilo pia limeopolewa kutoka lugha ya Kihindi..bhang..

Utagundua kuwa kuongezeka kwa msamiati wa Kiswahili au lugha nyingine yoyote hutokana na kuingiza maneno ya lugha nyingine.Utashangaa lakini hapo juu wewe mwenyewe umejikuta ukitumia maneno mengi ya Kiarabu,Kihindi ,Kireno,Kibantu n.k.

Umetumia maneno ya Kiarabu hapo juu kama: "Tabia,kubadilishabadilsha,raslimali,lugha,kiswahili,wataalamu,haramu,sifa,lazima,maana,sawa,uhuru,nadhani,muafaka,tujitahidi...n.k..

Maneno ya Kihindi kama "bangi",Kireno kama "muhogo"..Kiingereza kama "ishu"..."precious" n.k

Jaribu kutafuta maneno mbadala...kujieleza utakuta huwezi kueleweka!
 
Umeniacha na kizunguzungu.
Kumbe basi hata lugha yetu wenyewe hatuna???? sitaki kuamini.Najua kuwa Kiswahili ni matokeo ya mjumuisho wa maneno kutoka /lugha nyingi za kigeni na makabila ya hapa nchini.Ila kinachonishinda ni je? lugha zetu za asili ni maskini kiasi kwamba hatuweza kuazima maneno ya kutosha kukijenga kiswahili?
 
[B said:
WomenofSubstanc;377317]Opaque,
Hii tabia ya kubadilishabadislisha..kuna siku tutajikuta tumepoteza kila kilicho chetu...kuanzia rasilimali hadi lugha zetu! Watu wanachukulia juu juu hii ishu.
[/B]

Huu ndio utandawazi mama, hizi ni juhudi za kufanya dunia nzima kuwa na utamaduni wa kufanana. Na utamaduni huo hautatoka mbinguni ila ni kwa wale wenye nguvu za kiuchumi. Tukipunguza kulalamika na uafrika wetu ni dhahiri hii ni tabia ya kibinadamu, kutafuta maendeleo zaidi na kuimarisha mawsiliano baina ya watu. Kwa mfano hii inayoitwa Tanzania leo haikuwahi kuwepo hapo awali bali ni ilikuwa ni mkusanyiko wa jamii mbalimbali zenye mila na tamaduni tofauti.Kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea kukua kwa jamii, nyingi kati ya hizi zinaelezea jinsi jamii ilivyoanza kwa vikundi vidogovidogo vya watu waliokaa pamoja na jinsi maendeleo ya teknolojia na mawasiliano yalivyo viunganisha hivi vikundi hadi kuwa jamii moja kubwa. Ukifuata mtiririko huu ni wazi kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaelekea kuziunganisha jamii zote duniani. Kuna ushahidi wa kutosha jinsi watu wanavyoanza kufanana kitabia duniani kote mfano, vyakula wanavyo patiwa watoto wa kindergaten kwenda navyo shule siku hizi ni sawa kwa mtoto wa china, marekani au hata tanzania. Kwa mfumo huu Tanzania haiwezi kuwa salama kwani nguvu za mfumo huu ni sawa na nguvu za wakati.Nashangaa umeona majina tu, kuna vitu vingi tu ambavyo tunafuata mfumo huo uliouita wa kizungu mfano elimu, tiba, utawala n.k sio kweli hatuna elimu ya kiafrika au tiba au mfumo wa utawala ila kinacho wasukuma watu kuyaandika majina yao kizungu ndicho hicho kinachokusukuma wewe kutafuta tiba ya kizungu. Unaweza kusema kama tiba ya kizungu inafaida sana kuliko hasara lakini hasara za kuwa na jina la kizungu pia ni zipi? Mimi nafikiri kabla hatuja hoji kwanini watu wanaandika majina yao kizunguzungu ni bora tukahoji majina ya kiafrika yanaandikwaje? mbona herufi hizi tunazozitumia ni za kirumi, sasa kuandika jina la kiafrika kwa herufi za kirumi ni sawa?
Swala hili ni pana sana ila kufupisha hadithi jibu lake ni utandawazi na hatuna jisi ya kuukwepa ni vyema tukatafuta njia sahihi za kuishi nao. Mfano kujifunza zaidi juu ya tamaduni, mila na desturi hizi kabla ya kuzikumbatia au kuzikimbia.
 
Mkuu heshima na Amani kwako!
Nadhani sijakataa kuhusu utandawazi....wala sijasema watu wasiwe na majina ya kizungu/kihindi kichina etc... my point is write it as it is! Usilizungushie jina lako liwe la kizungu ilhali ni la kizaramo! thats my point.
Kuhusu herufi.... basi kama una herufi za kiafrika tujuze ..maadam tumezoea kutumia za kirumi tuzitumie kwenye majina yetu ipasavyo !
 
Najua sijakosea na huo ndio ukweli na ukweli unauma na unapouma watu hujikuta wako kwenye denial na kuanza kuukataa ingawa hukataa kwa maneno tu huku macho na dhamiri zao zikiwasuta.
Wacha dhamira/dhamiri? ziwasute na ukweli uendelee kubaki ukweli.
 
Na nyie mbatizao watoto majina kama Godlisten, Godliving, Loveness, Highness, Purity......???!!!
 
Back
Top Bottom