Je, ni sahihi kusema..?

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Kumekuwa kukiandikwa na kutangazwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kwa kutumia msemo huu" Inahofiwa watu kadhaa wameumia katika ajali hiyo". Neno KUHOFIA linaleta maana iliyokusudiwa katika sentesi hii? Na je, KUHOFIA maana yake ni nini?
 
ukiweza kufafanua kukaliwa/kukalia au kurudia/kurudiwa...utapata maana halisi ya swali lako
 
kuhofia limetoka katika kuhofu yaani kuogopa. hapo ina maana kwamba mzungumzaji anaogopa kusikia kuwa(e.g. abiria wote wamefariki ajalini!) sijui naeleweka???!!!
 
ukiweza kufafanua kukaliwa/kukalia au kurudia/kurudiwa...utapata maana halisi ya swali lako
Mkuu, aulizaye ataka kujua. Kama swali litajibiwa kwa swali basi hakutakuwa na haja ya kuuliza swali.
 
kuhofia limetoka katika kuhofu yaani kuogopa. hapo ina maana kwamba mzungumzaji anaogopa kusikia kuwa(e.g. abiria wote wamefariki ajalini!) sijui naeleweka???!!!

Mkuu nimekuelewa, nashukuru kwa ufafanuzi. Labda tusubiri michango ya wadau wengine.
 
Kaka huo unasibu wa lugha! muktadha wa matumizi ya neno kama ulivyobainisha ni shahihi.Neno hofu kama lilivyotafsiriwa na mdau hapo juu lina maana ya kuwa katika hali woga, wasiwasi hatihati na hali nyingine zinazofanana na hizo! Kwa vyovyote vile hali ya watu kuumia katika ajli si ambo la heri. Kwa sababu hiyo mzungumzaji lazima aonyeshe hofu juu ya tukio hilo na mara nyingi neno hili hutumika pale ambapo hakuna uthibitisho wa idadi kamili ya majeruhi au vifo katika tukio husika. Vinginevyo lingeweza kutumika neno inasadikiwa/ taarifa za kusadikika n.k.Ni mtazamo tu!
 
Lugha bwana hata aliyeitunga haijui,yaani hata yeye anabahatisha tuu,ikieleweka ndio imetoka hiyo!!
 
ndugu yangu hicho si Kiswahili sanifu ni yale yale mambo ya kutumia miundo na maneno ya Kiingereza na kulazimisha iendane na kiswahili
kuhofia uliyoitaja inatokana na wazungumzaji wa Kiswahiil kuathiriwa na neno FEAR la Kiingereza
Unajua unaweza kusema katika Kiingereza ten people are feared dead in.......
Hivyo kwa ujuzi wangu wa Kiswahili hakuna neno watu kadhaa wahofiwa kufa.
 
Mkuu kwa maelezo yako haya, inaonyesha kuwa huafiki na si sahii kusema "inahofiwa watu kadhaa..." Kwa maoni yako, unafikiri ni neno gani sahii lingefaa kutumika hapa?
 
Kaka huo unasibu wa lugha! muktadha wa matumizi ya neno kama ulivyobainisha ni shahihi.Neno hofu kama lilivyotafsiriwa na mdau hapo juu lina maana ya kuwa katika hali woga, wasiwasi hatihati na hali nyingine zinazofanana na hizo! Kwa vyovyote vile hali ya watu kuumia katika ajli si ambo la heri. Kwa sababu hiyo mzungumzaji lazima aonyeshe hofu juu ya tukio hilo na mara nyingi neno hili hutumika pale ambapo hakuna uthibitisho wa idadi kamili ya majeruhi au vifo katika tukio husika. Vinginevyo lingeweza kutumika neno inasadikiwa/ taarifa za kusadikika n.k.Ni mtazamo tu![/QUOTE]
Pamoja na maelezo yako mazuri hapo juu, bado napatwa na sintofahamu kuhusu maneno niliyokoleza hapa. Kwamba, unakubali kuwa si sahihi kutumia "kuhofia" mahali pa "Kusasadikiwa/kukadiriwa"?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom