Je ni sahihi kumpatia polisi wa usalama barabarni leseni akiomba aione

nsangaman

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
275
42
Salam wana JF
Naomba msaada wa kufahamu kama ni halali kwa polisi wa usalama barabarani kupewa leseni ya dereva husika pale anapoomba aione
Na je ni halali kuing'ang'ania na kugoma kuirudisha kwa dereva?
Asanteni
 
Salam wana JF
Naomba msaada wa kufahamu kama ni halali kwa polisi wa usalama barabarani kupewa leseni ya dereva husika pale anapoomba aione
Na je ni halali kuing'ang'ania na kugoma kuirudisha kwa dereva?
Asanteni

Kuomba leseni ni sahihi lakini kung'ang'ani siyo halali. Hiyo ni dalili ya kutaka rushwa.

Kama unakosa akuambie na kama ikibidi upigwe notofication kama una makosa.
 
Kuna tabia ya kung'ang'ania funguo za gari pia! Muambie tu gari yangu na funguo sikupi! Damn all trafic police in tz!
 
mkuu wana haki hasa ukizingatia nchi imeshachafuka awachelewi kujazana na feki leseni so akiangalia ana hakiki ,kingine inategemea aina gani ya leseni na cheo gani cha traffick alichonacho.....kuna aina za leseni awezi kukukamata traffic ana ka v kamoja tena umpi hata dk 2 kuongea nae...ila kwa kukusaidia kama umehamishiwa dar na kale kastarlet ushakaleta we usiumize kichwa wengi wao awavuti nyingi kubwa sana BUKU 3 yaani 3000..so kila ukiamka asbh weka kama alfu 4 za buku buku kwenye kadubwasha cha mbele utaendesha klwa amani na hata ukitaka kupita taa nyekundu ruksa hali una cha kuwasitiri
 
Mkuu hawa jamaa ni watanzania halisi kabisa. Hata siku moja hawawezi kung'ang'ania leseni kama huna kosa. Siri ya hawa ni kuwaheshimu na kuheshimu kazi yao. Kwani mara ngapi wametukamata na makosa wanatusamehe tena wakati mwingine bila hiyo hiyo bk 3 ya kawaida? Kwa sababu wabongo tunapendana ndiyo maana traffic anakubali kupokea elfu mbili ili akupe muda ukarekebishe makosa yako. Mimi naamini kabisa 50% ya magari huku barabarani yana makosa. Tena ukizingatia waendesha magari ni wengi kuliko madereva! kwa kifupi trafik akichukua leseni yako ana mpango wa kukusaidia, wewe toa tu ushirikiano hata kama huna kitu. Je uandikiwe 60,000 kwa kukosa safety eqpmnts au akusamehee kwa bk 3 ukanunue safety eqpments zako zote kwa 15,000?
 
Back
Top Bottom