Je, ni nani wanamtumia mwana JF huyu?

Duh!! mwenyewe nimeingia humu, got my breakfast on the table.. ready to read huyu mtu anayetumiwa hapa JF!! Nusura nipaliwe! Kumbe yamekuwa hayo... Anyway, nashukuru ndugu zangu kwa support, but I think it is enough. I'm getting really nervous, nadhani tumsamehe dada Bi. Senti, na kama ni ujumbe nadhani umefika au ni jaribio jingine la kutufanya tukwepe kuzungumzia hoja nyingine. Duh.. hii kali.

Miye nimeshamsamehe baada ya kusoma reply mbili tu kwenye thread hii. Hajui atendalo na tumsamehe.

Smart people learn from other people's mistakes, rich people learn from their own mistakes!

BTW Mkjj, hiyo breakfast yako iliambatana na paja la sungura au kipapatio cha kuku wa mama Rhoda?! :D

SteveD.
 
Du! Kumbe ndio maana mara nyingi wahenga wanasema kuwepo na wazee karibu ni kitu muhimu, idadi kubwa ya wachangiaji against na mtoa hoja lazima watakuwa hawako karibu na mababu zao sasa, au hawajapata bahati ya kuhadithiwa ... ni hivi mimi niko tofauti na ninyi wote mnaomshambulia mtoa hoja, kwa sababu ya usemi mmoja tu! nao ni...

"MJUMBE HAUWAWI"
 
What.....?

Sitaki kuamini kuwa bi senti anatumiwa kuja kutoa vitisho hapa..
Nisingependa kumlaumu sana kwa sababu makala hii ya kasungura ka lowasa inaigusa serikali pabaya..... this is what is going on all the time....

Ila ningemuhakikishia bi senti kuwa Tanzania ya sasa imebadilika na sio ile ya zamani ya kutishia watu ili wanyamaze... yule mtoto wa form one anayetishwa sasa hivi kwa kumuuliza lowasa swali anaweza kuogopa, JF is another beast.... jiulize maswali kabla ya kutoa vitisho hapa.... kuna mysterious power hapa...

Mkjj big up...... haters na wakwamishaji watakuwapo all the time!
 
Du! Kumbe ndio maana mara nyingi wahenga wanasema kuwepo na wazee karibu ni kitu muhimu, idadi kubwa ya wachangiaji against na mtoa hoja lazima watakuwa hawako karibu na mababu zao sasa, au hawajapata bahati ya kuhadithiwa ... ni hivi mimi niko tofauti na ninyi wote mnaomshambulia mtoa hoja, kwa sababu ya usemi mmoja tu! nao ni...

"MJUMBE HAUWAWI"

Sema unachotaka kusema sio kuanza kuhukumu membaz kuwa hawako karibu na mababu zao sasa.......
 
Wakuu naomba niiweke hii makala yenyewe hapa japo sijapata ridhaa ya Mwkjj ili muweze kuiona kama yasemwayo na Bi. Thumini kama yana uzito au la.

M. M. Mwanakijiji



KUNA michezo mingi ya kitoto ambayo ukikaa chini kufikiria inakuwa kama methali yenye maana. Baadhi ya michezo hiyo bado tunawaona watoto wetu wakiicheza leo hii sehemu mbalimbali nchini. Na kuna nyimbo nyingi za michezo ya kitoto ambayo watoto wetu nao huiimba siku hizi wakicheza kila jua lichwapo na giza liingiapo.

Mojawapo ya nyimbo bado ninazozikumbuka za tangu utotoni ni ule wa "Kakuku ka mama Rhoda". Sijui ni nani alianzisha wimbo au ni kwa nini waliutunga, lakini kwa vyovyote vile huyo mtu alikuwa na lake kwani kuku wa jirani alikuwa anakula mpunga wa mtu huyo na kila akitaka kukafukuza basi mama Rhoda alikuwa "anamkataza."

Sehemu ya wimbo huo ilisema "Kakuku ka mama Rhoda, kanakula mpunga wangu, nikitaka kukafukuza, mama Rhoda ananikataza,". Sasa usijisikie vibaya kujikuta ukiuimba wimbo huo kimoyomoyo kwani hata mimi ninavyoandika hapa najikuta nacheka kimya kwa kubania.

Ninapofuatilia mambo yanayoendelea nchini leo hii hasa katika medani za kisiasa ninajikuta kama mtu yule ambaye kuna "kuku" wa jirani anayekula mpunga wake, na inakuwa kazi kumfukuza kwani jirani mwenye nguvu zaidi anakataza.

Lakini leo sitaki kuzungumzia kuku huyu wa jirani, ninachotaka kuzungumzia ni jambo jingine nadhani mtu analoweza kulitungia wimbo na watoto wakaucheza. Jambo hilo linahusu ‘kasungurak ka Mheshimiwa Lowassa kaligowanywa vipande vipande.

Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alipokuwa akihutubia mkutano wa wananchi wilayani Sengerema katika ziara yake huko iliyomalizika siku chache zilizopita, aliamua kutumia mfano mwingine wa kuelezea hali ya kiuchumi ya Tanzania na hasa mgawanyo wa fedha katika bajeti iliyopita.

Waziri Mkuu alinukulikuwa na vyombo vya habari akisema: "Tumekaa bungeni kwa siku 67 tukigawana sungura...mnapaswa kujua mlipata mguu, maini au steki, ni haki yenu kujua ili muweze kufuatilia matumizi yake"

Ni haka "kasungura" ka Lowassa ndiko ninakotaka kukazungumzia kwa leo japo kwa kidogo tu. Baada ya kuja na majigambo ya kupaa kwa uchumi wa Tanzania mwanzoni mwa kikao hicho cha bajeti na kurudia tena wakati akitoa hoja ya kuhitimisha Bunge, leo hii amebadilika na kuja na mfano ambao ni kinyume kabisa na mfano wa ndege yenye kupaa. Lowassa ameamua kutumia mfano wa sungura kuelezea mgawanyo wa fedha za taifa katika sekta mbalimbali.

Lengo la mfano huo wa sungura lilikuwa kuonyesha jinsi gani "kile kidogo" tulichonacho au tulichokipata tumegawana kama taifa. Mfano wa sungura una lengo la kuonyesha kuwa tulichonacho ni kidogo na tunagawana kidogo kidogo na hivyo sisi sote tuwe waangalifu.

Kwa watu wengine mfano huo unaweza kuwa umewapita pembeni, lakini kwa mzee wenu kama kawaida ninaweza kusoma maneno ndani ya maneno. Nilipokaa chini kutafakari maneno hayo ya Waziri Mkuu nilijikuta nikikabiliwa na maswala kemkem.

Kwa nini tugawane ‘kasungura' wakati tuliona wamenunua ng'ombe? Walipokwenda kuwinda (kuomba misaada na kukusanya kodi n.k) walijitamba kuwa wamenunua ‘ng'ombe', lakini leo sisi wananchi tunaletewa kasungura imekuwaje? Kuna mtu anahitaji kutupa maelezo fedha zetu za ng'ombe zimekwenda wapi? Au ni nani huyo aliyekula ng'ombe wetu wa taifa na kutuachia sisi watu wa Sengerema, Nansio, Bunda, Ndali, Mabokweni, Endabash, Ujiji, na kwingineko ‘kasungura?'

Wakati walipokwenda kununua ndege ya bilioni 50 na rada ya bilioni 50 sawa walitumia kwa ujumla karibi bilioni 100 na ushee na waliponunua magari mawili ya ofisi yake kwa karibu milioni 200 nina uhakika hatuwezi kusema hako ni ‘kasungura'. Leo hii mawaziri na manaibu wao jumla ya watu 60, madereva, na wasaidizi wao wanapita vijijini kutuambia jinsi tulivyogawana sungura huyo.

Hivi kuna mtu amewauliza wanatumia gharama ya kiasi gani kutuuzia habari za sungura aliyekatwakatwa vipande vipande? Makisio ya rafiki yangu mmoja mwenye kujua undani wa ziara ni kuwa waheshimiwa hao watatumia karibu shilingi bilioni mbili, kutunadia gharama ya sungura ‘mjanja'. Tukisema ufisadi tunaambiwa tunawasingizia. Ufisadi si rushwa tu, hata matumizi mabaya ya ofisi yanaingia humo humo.

Rafiki yangu mmoja (mwalimu wa chuo kikuu kimoja Marekani) nilipomwelezea habari hizi mpya za Lowassa ilikuwa kama bahati hivyo. Siku chache zilizopita yeye na wenzake walikwenda kuwinda sungura, na baada ya majaribio ya hapa na pale walijikuta ili kujitosheleza kwa ‘mboga' walihitaji kujipatia sungura watatu, kwani sungura mmoja hatoshi. Sijui ni nani aliyempa mfano huo Waziri Mkuu maana mifano mingine inatolewa kwa lengo zuri lakini maana yake inakuwa kubwa kuliko ilivyokusudiwa.

Nikiendelea kuzungumzia huyu sungura wa Lowassa yeye aliyemaanisha ni fedha za wananchi wao bungeni walizokaa kuzigawa na akatamba kule Sengerema kuwa mwaka huu serikali imetenga fedha nyingi kabisa ikiweka kipaumbele kwenye sekta kadhaa. Majigambo hayo yanastahili makofi kwa mtu asiyehoji, lakini katika Tanzania hii wananchi walioameanza kuamka, tatizo haliko katika kasungura kenyewe, bali wale wanaotugawia sungura huyo.

Leo hii kashfa mbalimbali zinazungumzwa na karibu shilingi trilioni moja zinadaiwa kupotea katika mikataba mbalimbali mibovu na maamuzi mbalimbali mabovu. Na hizo ni fedha unazoweza kuchunguza kwa kuangalia vitabu. Lowassa mwenyewe huko huko Mwanza aliwaasa kwa mara nyingine tena (ndiyo mara nyingine nikianza kuwahesabia itabidi niandike makala nyingine) wakurugenzi wa halmashauri kuwa "mkurugenzi atakayerudisha fedha kwa kushindwa kuzitumia katika miradi iliyopangwa atachukuliwa hatua." Vitisho hivi vya Waziri Mkuu ni vitisho tulivyovizoea tangu walipokwenda Ngurdoto wakatuletea ndoto yao.

Rais mwenyewe, makamu wake na hata mawaziri wengine (Dk. Mwinyi karudia tishio hivi karibuni) wamekuwa wakivitoa kama wimbo wenye ubeti mmoja. Ukweli ni kuwa vitisho hivi vimezoewa na watendaji mbalimbali wa serikali.

Rafiki yangu mwingine aliyeko Dar es Salaam ameniambia kuwa siku hizi kwenye klabu za usiku kuna baadhi ya watu wananyanyua glasi zao za mvinyo na kugongeana wakisema kwa kejeli "maisha ya neema yanawezekana, kwa wana-CCM". Hakuna mtendaji anayeogopa vitisho vyao, kwani wanajua kuwa "nani atamnyonyeshea nani kidole".

Leo hii Lowassa na viongozi wengine wanasisitiza wananchi wawafichue wanaofuja mahali za umma na wanaokula fedha za umma. Bahati nzuri Mtanzania mwenzao Dk. Slaa na Watanzania wengine kama kina Tundu Lissu wamejitolea kuwaonyesha wananchi kuwa kale kasungura kalikuwa kamezaa na kuna watu wamekula vitoto vya sungura ndio maana tunaendelea kugawana kasungura kamoja! Watawala wetu hawataki kukubali na badala yake wako kwenye jaribio kuu lililoshindwa la kukana.

Na tatizo kubwa ni kuwa hata kukana kwenye hakuna mantiki. Hivi kama watu wamechafuliwa majina na wametuhumiwa vitu vya uongo kwanini wanaitisha vyombo vya habari kuwaambia ni jinsi gani hawakutendewa haki? Hivi kwa watu wasomi kama kina Dk. Mgonja na kina Rutabanzibwa wanaona ugumu gani wa kwenda Mahakamani?

Binafsi kama kuna kitu kimenichekesha ni kitendo cha watu hawa wote kukimbilia kwa waandishi wa habari na kusema ati watakwenda mahakamani. Hivi nani amewaambia kuwa ili kwenda mahakamani hadi waombe kibali toka kwa wahariri na waandishi?

Binafsi ningefurahi kuona ndugu zetu hawa wakikimbilia mahakamani ili kuwaonyesha wananchi kuwa wao ni waadilifu na wanaofuata utawala wa sheria. Na wakati wakienda huko mahakamani nina uhakika kuwa mahakama itapotoa hati za kuita mashahidi watakaoitwa wataheshimu mamlaka hiyo ya mahakama.

Bila ya shaka kama wakienda mahakamani baadhi ya wananchi ambao wanaweza kuitwa mahakamani ni pamoja na Rais Mkapa, Waziri Mkuu Lowassa, na aliyewahi kuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini Jakaya Kikwete. Nina uhakika kama kuna wakati ambapo demokrasia yetu itatiwa moyo na utawala wa sheria kuinuliwa juu ni pale tutakapowaona kina Mkapa, Lowassa na Kikwete wakinyosha mikono juu kula kiapo pale Kisutu kuwa watasema "kweli na kweli tupu"! Waliotishia kwenda mahakamani sidhani kama wamefikiria hilo.

Sasa hivi viongozi wa serikali na CCM wameanza ziara ya kwenda kwa wananchi kuelezea na kujibu hoja za wapinzani. Bila ya shaka watajaribu kutuelezea kale kasungura ketu kalipatikana vipi, ilikuwaje kasizae licha ya kukalisha kwa kila chakula bora na mashudu! Sitashangaa uhakika wananchi watawapokea kwa mabango yenye kuuliza "kasungura sawa, ng'ombe wetu vipi?" Na sitashangaa wananchi wakiuliza "Aliyekula ng'ombe ni nani, mbona mwatupa sungura?" Usalama wao itakuwa ni kwenda kuwaelezea viongozi wenzao wa CCM wa huko vijijini.

Viongozi wa CCM waache kukurupuka na badala yake wakae chini, watafakari uzito wa hoja zinazotolewa na wajibu hoja hizo kwa hoja. Mambo ya kuwafanya Watanzania hawawezi kufikiri au kwamba hatuwezi kusoma alama za nyakati ni kututukana matusi ya rejareja.

Kama CCM na serikali yake wanafikiri kuwa watawaburuza tena Watanzania kwa hoja zisizo na mkia wala kichwa alimradi vimulimuli, bendera na parapanda zinapigwa, basi wao wazinduke katika jinamizi hilo, maana limewakaba.

Hoja ni lazima zijibiwe kwa hoja. Kutuma wapambe, mawaziri, manaibu waziri au vikundi vya nyimbo kuwataka wananchi wapuuzie hoja ni kutaka kuwaweka mtegoni kwani wananchi wamejiandaa kuwazomea na kuwakatalia majibu yasiyoeleweka. Uwingi wa maneno si uzito wa hoja! CCM na serikali yake wanajitahidi kusema mengi pasipo kusema lolote lenye maana huku wakitumia vyombo vyao kuupotosha umma ili kupoteza mwelekeo wa hoja. Safari hii wameshikwa mashati na hawaachiliwi hadi watoe majibu yenye kueleweka.

Watoe majibu ilikuwaje Rais na Waziri wake wawe na hisa kwenye kampuni ambayo wao wenyewe wamehakikisha kuwa inapata mkataba mkubwa wa serikali? Watoe majibu ilikuwa kampuni inayoitwa ni ya serikali iandikishwe nje ya nchi na kwenye vipengele vya uundwaji wa kampuni hiyo hakuna mahali panaposema kuwa ni ya serikali?

Watoe majibu ilikuwaje kwenye kampuni hiyo urithishaji uende kwa watoto wa wakurugenzi wa "serikali" na wajukuu wao? Watoe majibu yanayoeleweka ya maswali hayo na wajibu swali baada ya swali si kama walivyofanya juzi kwa kuchagua maswali mawili matatu kuyajibu.

Mtu unapopewa mtihani unatakiwa kujibu maswali yote hata kama utakuwa umekosea, lakini kuruka maswali ni kujitakia alama za ‘si vyema' za bure. CCM mmejichimbia shimo na ni nyinyi wenyewe mjitoe humo!!

Wananchi wamechoka kuambiwa maneno matupu alimradi yanatoka kwenye "tamko rasmi la serikali". Ndugu zangu wananchi haya ni mapambano ya kifikra.

Mapambano haya yalianza rasmi Mei 1995 wakati Mwalimu alipojenga hoja nzito ya "wapi tunatoka, wapi tulipo na wapi tunataka kwenda". CCM sasa hivi wamebanwa kwenye uwanja wa hoja, na wanatapatapa; fikra zao zinaonekana kuwa ni dhaifu hata kama watazipigia matarumbeta na kuziwashia vimulimuli na kupiga ving'ora! Hoja dhaifu ni hoja dhaifu hata itolewe kwa ngoma na muziki wa jadi!

Ushauri wangu wa bure ni kwa CCM kukaa chini, wapime uzito wa hoja, na watambue wapi makosa yalitokea, wazungumze na wananchi na kuwaambia wananchi ukweli. Wawaambie kuwa kulikuwa na makosa kwenye mkataba wa Buzwagi, kwamba viongozi kadhaa hawakufuata maadili ya uongozi, na ya kuwa kulikuwa na upotevu wa fedha nyingi na hatua zinachukuliwa dhidi ya wahusika (ikiwamo kufilisiwa) na kuwaahidi wananchi kuwa mambo kama hayo hayatotokea tena.

Wakubali kuwa kuna mtu aliboronga na mtu huyo lazima awajibishwe. Kwa wao kuendelea kung'ang'ania kuwa "hakuna tatizo" na ya kuwa "hoja hizi ni za wapinzani waliopoteza uchaguzi 2005" ni kutudharau Watanzania na kutudhania kuwa hatuwezi kupima pumba na mchele.

Kabla sijamaliza naomba nitoe ombi kwa wachora katuni wa vyombo vyetu vya habari. Katika nchi mbalimbali ambako mwamko wa fikra za kimageuzi zimeanza kusambaa, basi kambi zinazopingana zinakuwa na alama zao. Kenya kulikuwa na Machungwa na Ndizi, na kule Uganda walikuwa na majani ya migomba!

Hapa Tanzania bado hatujawa na alama za pande mbili za kisiasa zinazogongana sasa hivi kifikra. Hivyo, napendekeza kuanzia sasa "sungura" awe ndiyo alama ya CCM, kwanza kwa jinsi alivyotumiwa na Lowassa lakini kubwa zaidi kutokana na ujanja wake katika masimulizi ya fasihi yetu.

CCM imeweze kujijenga na kujijengea mazingira ya kutawala kutokana na kuwa na ujanja wa kisiasa. Hivyo sungura atawakilisha wale wote wenye mawazo ya CCM na ambao maisha yao yamenufaika na kufaidishwa na maisha ya kijanja kijanja.

Kwa upande wa upinzani, napendekea alama ya punda. Nimemfirikia punda kwa vile ni mnyama wa kazi huenda anayetaka kwenda na mara nyingi hawezi kwenda mahali pasipo kusindikizwa na punda mwingine. Zaidi ya yote, punda anatabia ya kuchoka anapotwishwa mzigo kuliko uwezo wake hivyo hata achapwe mijeledi kiasi gani akigoma kagoma.

Ni kiburi cha ‘utu' wake na hadhi yake kuwa kuna mizigo mingine habebi. Hivyo punda basi atawakilisha wale wote ambao kutwa kucha hufanya kazi kwa kujituma ili wajitengenezee maisha mema ya mafanikio. Watu hao wamefikia mahali sasa hawakubali tena kuburuzwa au kulazimishwa kwenda wasikotaka kwenda, kukubali visivyokubaliwa, na kupigia makofi visivyoshangiliwa.

Mwisho kabisa niseme kuwa watawala wetu wanapokuja na maelezo ya sungura wa Lowassa, wakumbuke kuwa wananchi nao wanajua kilichonunuliwa kuwa ni ng'ombe, tena si ng'ombe mmoja. Kwa muda mrefu wananchi wamekaa kimya kwa heshima lakini sasa wanataka kujua iweje wao wapewe sungura wakati wachache watetewe na walindwe walipokula ng'ombe na mbuzi wa kijiji?

Wakati umefika tukatae kuendelea kugawana kasungura ka Lowassa kanakonadiwa na viongozi wa CCM. Tuwaambie kwa heshima kubwa na taadhima, kuwa tumechoka kugombea kasungura! Na sisi tunataka ng'ombe!

Kama kwenye ndege iliyopaa mmepakiana wenyewe, basi angalau kwenye kula ‘ndama' na sisi mtugawie! Na hilo si ombi ni takwa, kwani tumemlipia huyo ng'ombe na tumemlisha! Iweje wenzetu mle hadi mrithishane mapaja na mbavu, halafu mje kutuuzia habari za sungura!?

Vinginevyo, tutawatungia wimbo kama ule wa "kakuku ka mama Rhoda" Hatutakubali kuendelea kukatazwa kukafukuza kakuku hako kanakokula "mpunga wetu". Na maneno ya kwanza ya wimbo huo yatasema "kasungura ka Lowassa kamekatwa vipande vipande, nani kala sungura, na nani kala ng'ombe?"

Niandikie: mwanakijiji@jamboforums.com
Sikiliza mahojiano na Tundu Lissu: http://www.mwanakijiji.podomatic.com

Haka kasungura katamuuuu! ngoja niwahi salala, maana mguu mnofu wake mdogo?
 
Bi 50 cent au haya maneno umeyatoa katika kikao cha kamati kuu ya Sisiemu jana,?
mwenye data atuambie nini walizungumza jana?
 
acheni ujinga wa kuuliza ushahidi wa kila kitu, kama kasema anatumiwa na huyo mtu anaandika makala then why kutoa ushahidi mwingine wakati ashatoa ? upuuzi huo jamani usiokuwa na maana !
 
yeye kauliza na mnachotakiwa ni kujibu kwamba anatumiwa au la ! na si vinginevyo ! na huo ni upuuzi kabisa mwafrika wa kike unaposema mtu anakuja kutoa vitisho wakati hamna chembe ya kitisho unachosema ! acheni tabia zenu hizo, either mjibu swali au mngeuchuna ! bi. senti 50 wee komaa nao !
 
Duh!! mwenyewe nimeingia humu, got my breakfast on the table.. ready to read huyu mtu anayetumiwa hapa JF!! Nusura nipaliwe! Kumbe yamekuwa hayo... Anyway, nashukuru ndugu zangu kwa support, but I think it is enough. I'm getting really nervous, nadhani tumsamehe dada Bi. Senti, na kama ni ujumbe nadhani umefika au ni jaribio jingine la kutufanya tukwepe kuzungumzia hoja nyingine. Duh.. hii kali.

MM Mwanakijiji,hivi ni vijimambo tu,hakuna lolote hapo,hivyo ni vitisho mbuzi tu,mzee una point kweli kweli,kumbuka shujaa huwa harudi nyuma.Vitisho dhidi ya mashujaa havijaanza leo,tokea enzi
za akina Mandela ,Martin Luther King Jr,Nyerere,hata Obama kuna kipindi alipewa vitisho,kwa hiyo hilo si jambo la kukatisha tamaa,tena vitisho kutoka kwa hawa manyang'au na kisungura chao,wapi bwana,hizo ni longolongo tu.Mwanakijiji kipaji chako cha uandishi ulichopewa na Mwenyezi Mungu kitumie vizuri katika kuelimisha jamii yetu,binafsi nakuombea kila la kheri,God Bless You Man,wewe ni shujaa.Tunakuomba jtano ijayo tuchambulie speech
ya mwl Nyerere huko Mbeya,ukijaribu kulinganisha na hatima ya Tanzania kwa sasa,nadhani makala yako kuhusu hizo speech unaweza kujaza kurasa nyingi sana,endapo neno moja la ka sungura lilitolewa na EL umeweza kuliandikia makala ndefu na nzuri kiasi kile,why not speech za Mwl Nyerere uki-compare na nyang'aus wa sasa.
 
Baada ya kusoma makala ya mmoja wa wanachama wenzetu hapa kwenye Tanzania Daima siku ya Jumatano, nimeanza kuamini kuwa ndugu yetu huyu ana lake jambo au kuna watu wanamtumia kumsakama Waziri Mkuu. Ni nani anamlipa na kumtumia kumuandama kiongozi wa Taifa namna hii? Makala yake ya mwisho (Ukiingia Tanzania Daima bonyeza "Gazeti la Jana hadi ufikie Jumatano) ina kichwa cha habari ya "Ka Sungura ka Lowassa, na Aliyekula Ng'ombe". Hapa ofisini watu walikuwa wananyang'anyana gazeti ili kusoma kitu hicho na ameanza kujipatia mashabiki wengi.

Jambo moja tulilokubaliana ni kuwa kuna mtu au kikundi cha watu kinamtumia. Namshauri tena apunguze kasi au achukue breki, siyo wote wanafurahia maandishi yake. Ni ushauri mwingine wa bure.

Asante.

Hivi Watanzania hawana haki ya kutoa maoni yao bila kutumiwa na mtu? Hili linasikitisha sana! Baada ya miaka 46 ya uhuru, watu wanyamaze tu hata kama nchi inaelekea pabaya, wakisema basi wanatumiwa na mtu! Bado tuna safari ndefu sana!
 
Mike in Brazil ( Hawaiian Punch ) na wee komaa vile vile na makala zako za sungura na lowassa, hakuna aliyekutisha hapa, nadhani ni waandishi wanaotwist maneno kusema umetishiwa wakati hamna kitisho chochote ! wasalaam.

Mwanakijiji ningekukaribisha kula pilau lakini naskia wee mbaya kweli katika mambo flani flani.
 
Hivi Watanzania hawana haki ya kutoa maoni yao bila kutumiwa na mtu? Hili linasikitisha sana! Baada ya miaka 46 ya uhuru, watu wanyamaze tu hata kama nchi inaelekea pabaya, wakisema basi wanatumiwa na mtu! Bado tuna safari ndefu sana!

nadhani tukiangalia katika mstari wake wa mwisho huyo bi senti 50 tunaona kwamba kaandika ni ushauri wake wa bure, na sio vitisho ! kwa hiyo katoa ushauri, either take it or we dont, lakini sio kumshambulia from no where !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom