Je ni nani kiongozi muadilifu na anayehitajika Tanzania?

hasan124

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
716
128
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia posts zinazowekwa na wanaJF, in general karibu kila kiongozi aliyekuwa na uthubutu wa aidha kukemea, kukaripia, kuweka hadharani uozo ama kuhusishwa nao wa ama sirikali au waziri fulani/katibu mkuu/mkurugenzi/meya na hata prezidenti na wengine weengi kama hao basi kwa namna moja amekuwa criticised kwa namna moja ama nyingine.

Tumeona viongozi kama Sita, F. Mbowe, Lowasa, Z. Kabwe, Madame Spika, G. Lema, Hamad Rashid, J. Mnyika na wengine weengi wakitolewa shutuma nzito kutokana na misimamo yao tofauti tofauti na wengine aidha kuhusishwa na tuhuma hizo direct while wengine kuonekana kushikia bango wenzao kwa namna ya kujichukulia chati VIA tuhuma/kashfa husika.

Swali langu linakuja, Je, ni nani kiongozi mwenye kujali maslahi ya taifa na anayestahili kweli kuwepo ktk nafasi aliyopo ama kupata cheo zaidi bila kujali itikadi za kichama na KWA nini unadhani anastahili? AMA JF ipo kwa ajili tu ya kupigana madongo kwa kila upande kuvutia kwake na kujifanya mtakatifu?
 
Nimekuwa nikifikiria nakujiuliza maswali kama leo ningeambiwa nimchague mtu ambaye nimwadilifu mcha mungu bila kujali itikadi za vyama ningemchagua nani...
 
Kwa kweli tunahitaji kiongozi,mwenye hofu ya Mungu,mchapakazi,mwerevu,na mwenye kujituma na mwenye kuipenda nchi yake,huyu si mwingine ni great visionaire ama mbunge wa wilaya ya ilemela mwanza mwaka 2015
 
Back
Top Bottom