Je ni mhimu kupenda kwa moyo wa dhati?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Kulikuwa na msichana kipofu aliyejichukia mwenyewe kwa ajili ya upofu.Alimchukia kila mtu isipokuwa boyfriend wake.Siku moja akamwambia boyfriend wake kama ningefanikiwa kuona dunia tu kwa macho basi ungenioa.
Siku moja akapewa macho na mtu asiyemfahamu,akafanikiwa kuona kila kitu,akafanikiwa kumwona boyfriend wake.
Boyfriend wake akamwuliza ''umefurahi?umeridhika?sasa naweza nikakuoa?........Msichana akashtuka sana kumwona boyfriend wake ni kipofu na akakataa kuolewa.
Boyfriend akaondoka huku akilia machozi....akamwambia girlfriend '''nakutakia maisha mema,naomba uyatuze macho yangu''

Je kuna umuhimu wa kumpenda mpenzi wako kwa dhati na kujitolea kwa ajili yake?
 
Ni raha sana kupenda, kama hujawahi penda basi naamini kuna kitu kitamu sana hujawahi pata.

Kuumizwa ni kitu kingine, pamoja na hayo bado kupenda muhimu.
 
yaani mpaka umejitolea na kuwa kupofu kwa ajili ya mtu halafu ukatoswa
 
Upendo wa dhati ni wa muhimu na wa raha pale tu ubahatike kupata anaekupenda pia
 
Mwenye nguo mbili ampe moja yule asie na nguo,,,hvyohvyo huyu mwenye macho mawili alitakiwa ampe moja huyo mwenzi wake....kakurupuka tu cjui kawaza na kichwa part II.!!! By tha way ni muhmu kupenda kwa dhati,lakini bongo(akili) yako iwe active
 
basi jamaa kaingia chaka
 
Ako kastori kamenifurahisha sana na kunisikitisha pia!!

Ila kama walivyosema wapendwa hapa, hayo ni mambo ya kawaida tu katika mahusiano,
Sema tu hapo imenogeshwa na kisa cha upofu na kugawana macho......

Inatupasa mara zote kutoa penzi lote hasa pale unapopenda hasa, sababu kujibana bana nayo inamadhara makubwa kuliko upofu...!

Mkuu Excellent, usiruhusu jeraha moja la kimapenzi kukufanya kukugeuza uwe mnyama... ie kujibana kutoa penzi lote ni unyama lol
 
We penda tu......ukiumizwa basi, unaendelea na safari nyingine!

Dunia ikijazwa na watu kama nyie... itakuwa safi sana....
Afu mara nyingi hao waumizaji huwa hawafiki mbali, mfano Ex angefuatilia stori ya huyo kipofu baada ya kumuacha mwenzie, utakuta wala hakufika mbali.
 
Alafu najiuliza huko mbeleni anaenda kuishije na kufurahia mapenzi au maisha kwa ujumla....huku akiwa na macho ya mwenzie?? Je, hilo halitamtesa nafsi yake hasa pindi aonapo vipofu wengine wakihangaika? Dah.....kuna watu wana roho kwakweli!!
 
Ako kastori kamenifurahisha sana na kunisikitisha pia!!

Ila kama walivyosema wapendwa hapa, hayo ni mambo ya kawaida tu katika mahusiano,
Sema tu hapo imenogeshwa na kisa cha upofu na kugawana macho......

Inatupasa mara zote kutoa penzi lote hasa pale unapopenda hasa, sababu kujibana bana nayo inamadhara makubwa kuliko upofu...!

Mkuu Excellent, usiruhusu jeraha moja la kimapenzi kukufanya kukugeuza uwe mnyama... ie kujibana kutoa penzi lote ni unyama lol

Mkuu ndo hivo,tunaweza tukapenda ila tunapopenda isiwe sababu ya kupoteza nafsi zetu na majuto ktk maisha
 
Alafu najiuliza huko mbeleni anaenda kuishije na kufurahia mapenzi au maisha kwa ujumla....huku akiwa na macho ya mwenzie?? Je, hilo halitamtesa nafsi yake hasa pindi aonapo vipofu wengine wakihangaika? Dah.....kuna watu wana roho kwakweli!!

Hicho kinakuwaga kiwewe cha muda tu kinachotokana na kuchanganyikiwa kwa ulimbukeni wa hali flani...
Baadae mtu anapoa na kujitammbua kuwa mambo hayapo kama alivyotaka kuyapeleka
 
Back
Top Bottom