Je, Ni Kweli Watu Weusi Wana Akili Ndogo?

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Nlilipokuwa nasoma darasa moja ambalo Instructor na wanafunzi wote ni wazungu isipokuwa mie mweusi peke yangu katika moja ya mataifa makubwa siku ya kwanza nikaona kama ni kiinimacho ukitilia maanani kuwa wao lugha ni yao ya kuzaliwa na mie ulimi mzito kidogo tokana na kimatumbi changu. Utundu wao ndio ulinifanya nianze kuamini kwamba hatutofautiani kwa kunishirikisha mijadala kadhaa ili kuzoea lafundhi yao na ulimi wangu aunze kuondoa jiwe zito lilizofungwa na hivyo kuwa mwepesi kama wa kuzaliwa bongo na kukulia ughaibuni. Darasa lilipokolea nikaona elimu yangu ni juu zaidi yao, kumbe ni lugha tu niliyokuwa najitahidi kuwafukuza niwashike na nilipowashika walishika adabu.

Suala hilo naona limejenga hoja kwa kutegemea maendeleo ya mahali na wala si kigezo cha mfumo wa kisayansi katika ubongo wa binadamu unavyofanya kazi. Mfumo wa ubongo wa binadamu ni ule ule kwa maana hiyo hakuna hitilafu kati yao kadiri ya bayolojia isipokuwa tunatofautiana mfumo wa rangi tokana na asili ya mtu na cell anazorithi toka kwa wazazi.

Kigezo cha maendeleo ni dhahiri mtu anayeishi pwani mazingira yake ni tofauti na anayeishi Mikoa ya Nyanda za juu au kando ya maeneo ya nyanda za juu kama Lushoto, Arusha. Kwa mantiki hiyo anayeishi maeneo ya hali ya hewa ya baridi anahitaji jitihada zaidi ili kujilinda na hali ngumu ya maisha ya baridi kuliko anayeishi mazingira ya joto kama pwani kwani pengine watu wamekuwa na kawaida ya kuyaacha makazi yao na kwenda lala pwani kukwepa joto kali na hivo kupata upepo mwanana ufukweni mwa bahari. Kwa maana hiyo tofauti ya maendeleo yamechochewa na mazingira ya watu, hali ya hewa, muingiliano wa watu nk.

Kwa mfano mataifa ya ulaya yalikuwa na mwingiliano sana wa watu hivyo ikawa rahisi kubadilishana mawazo na maarifa. Kwa mfano Marekani imekuwa ndio kinara wa kugundua mengi katika maendeleo ya uchumi duniani kama ugunduzi wa bulb ambao ulifanya na Thomas Edson wa West Orange City NJ, ugunduzi wa magari yanayotumia engine badala ya kukokotwa na farasi, ugunduzi wa air craft na nukilia. Kwa nini nchi ya Marekani imekuwa kinara wa ugunduzi wa mengi duniani katika maendeleo? Jibu ni rahisi, taifa la marekani limeundwa na mataifa mengi duniani, na hivyo mchanganyiko wa mataifa mengi, uhuru wa raia wake na uhuru wa dini umesaidia katika mengi kugundulika kwani mataifa mengine ingeonekana kama kushindana na Mungu ni dhambi.

Kasoro kubwa bara Afrika ambalo linatafsiriwa kama watu weusi ni kutanguliwa na mataifa ya ulaya katika maendeleo na hatimaye kudumazwa kwa vile nguvu kazi ikachukuliwa na waliotutangulia kwenda kuendesha uchumi wao, na waliobaki wakawa wanaishi kwa wasiwasi na kujificha hapo maendeleo yaliyofikiwa yakadumaa. Viwanda vingi vya kutengeneza zana za kilimo, viwanda vya nguo vilidumazwa vilidhaliliswaha na kusimama tokana na wazungu kuvizuia ili kupata soko la bidhaa zao, kwetu ikawa ndio chimbuko la malighafi kwa ajili ya viwanda vyao.

Nilishangaa wakati nilipokuwa chuoni nikawa pia nafanya kazi kiwanda cha kutengeneza electronic parts, nilishangaa kuona matani na matani ya madini toka Zambia yakiteremshwa kiwandani kutengeneza vifaa ambavyo vinauzwa tena zambia kwa bei mbaya. Nikakumbuka somo la uraia na somo la historia jinsi utajiri wa afrika ulivyotajirisha mataifa makubwa. Kazi za watumwa zilizofanywa katika mataifa makubwa huwezi amini kama Jumba la makao makuu ya Marekani na White House ni kazi ya watumwa toka afrika.

Nikirudi nyuma nilishangaa wazungu walivyowaendesha darasani waafrika na wabaki wameduwaa bila kutegemea, na mweusi alipozidi kuzoea na kuonyesha uwezo wake akawa mwanafunzi na mkufunzi msaidizi.

Tumeshuhudia uwezo mkubwa wa watu weusi katika mambo mbalimbali kisiasa, kiuchumi, kimichezo na kimaisha, matokeo hayo yote ni kuonyesha kiwango cha juu kabisa cha watu weusi kiakili na uwezo wa ubongo wao kuwa sawa tu na watu weupe.

Kwa maana hiyo watu weusi na weupe hatuzidiani kiakili ila mazingira yametufanya tutofautiane kimaendeleo kitu ambacho si kigezo cha kuzidiwa watu weusi kiakili na watu weupe.

Candid Scope

mjengwa
 
Sasa mbona umeweka kama swali wakati umeshapata jibu tayari?Nwyz udogo haupo kwenye akili upo kwenye matumizi ya hiyo akili!
 
Tuwe wa kweli jamani....wenzetu wana akili zaidi hata za kufikiri tu ukikaa na mtu mweupe wako sharp sana......wenzetu walituacha zamani sana....hata wakituachia vitu vya maana na kutufundisha namna ya kuviendesha bado tunashindwa na vinakufa.....................they have a veyr higjh iq
japo ukweli unauma acha ukweli uchukue mkondo wake alafu tupater hasira tupige kazi
 
Umeisha jibu swali lako! Akili Mungu katupa wote sawa ila tatizo wavivu!!! t

unapenda mambo mazuri ila kazi hatupendi tukipata kasababu ka kutofanya kazi tuna kang'ang'ania weee tukidhani siku zinaganda! Watanzania sasa hivi woote tumekuwa wana siasa siasa ikishuka joto tunatafuta kitu kingine kama mpira (ligi za ulaya!!), kucheza ngoma, muziki na kadhalika! of course hata wazungu wanacheza ngoma za kikwao, Mpira ila ikifika kufanya kazi ni kazi tu. Upo hapo.
 
Tuwe wa kweli jamani....wenzetu wana akili zaidi hata za kufikiri tu ukikaa na mtu mweupe wako sharp sana......wenzetu walituacha zamani sana....hata wakituachia vitu vya maana na kutufundisha namna ya kuviendesha bado tunashindwa na vinakufa.....................they have a veyr higjh iq
japo ukweli unauma acha ukweli uchukue mkondo wake alafu tupater hasira tupige kazi
Umeniacha hoi hapo nakumbuka viwana vya viatu vya bora,bata na zana za kilimo Ufi,kiwanda cha Urafiki na kadharika vyote vimekufa!
 
Sote tuna akili sawa Wazungu na Waafrika,na hata darasani tunaweza kuwazidi sana tu...ila tatizo ni kuwa sisi mwisho wetu wa kusoma ni kwenye vyeti tu...wenzetu wanaenda mbele zaidi na kuitumia akili kwenye ugunduzi na kufanya mambo mapya zaidi...Waafrika tuna tatizo katika innovation.Matokeo yake tunabaki kujisifia vyeti tu,BILA kuangalia tumetumiaje akili yetu kubadili maisha yetu na ya jamii zetu na nchi zetu
 
Malipula hilo nalo neno man tunapenda sana kuona A kwenye vyeti ni sio practicals
 
Tuwe wa kweli jamani....wenzetu wana akili zaidi hata za kufikiri tu ukikaa na mtu mweupe wako sharp sana......wenzetu walituacha zamani sana....hata wakituachia vitu vya maana na kutufundisha namna ya kuviendesha bado tunashindwa na vinakufa.....................they have a veyr higjh iq
japo ukweli unauma acha ukweli uchukue mkondo wake alafu tupater hasira tupige kazi

Mzungu na mweusi wakizaliwa na kukua katika mazingira sawa wana akili sawa na kila kitu ni sawa isipokuwa rangi. Nafahamu wazungu wengi tu wajinga kuliko baadhi ya weusi ninao wafahamu.

Kama utamaduni fulani ukiwa injected kwa waafrika(weusi) kuna uwezekano mkubwa sana wakabadilika. HataTanzania ukiangalia hata makabila yana tofauti, wengine wanasemekana wana akili wengine hawa.

Hakuna sayansi iliyothibitisha kuwa mtu mweusi hana akili. Lakini vitendo ambavyo vinatokana na socialization ndio vinaonesha waafrika wako nyuma saaana kuliko wazungu. Jibu ni social factors, sio in born.
 
Back
Top Bottom