Je ni kweli viongozi wakuu wa nchi hii wamekuwa wakijihusisha na Freemason?

swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
38


Sir Andy Chande akiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Andy Chande akiwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.
...Andy akiwa na Mzee Mwinyi.
...Chande na Karume.
....Chande na Sumaye.
Na Elvan Stambuli
JAMII ya Siri (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito naviongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Madai hayo, yametokana na kile kinachoonekana kwamba Kiongozi Mkuu waFreemason, Afrika Mashariki, Sir Andy Chande, amekuwa akijiweka karibu naviongozi wakuu wa nchi hii kila awamu, hivyo kuonesha kuwa kuna kituanakitafuta.
Kikubwa kinachodaiwa ni kuwa Chande anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwambakila kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya siri.
Inazidi kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za hali ya juu kujiweka karibu naIkulu, ikiwa na mpango wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni memba wajamii hiyo katika awamu zinazokuja.
Uchunguzi wa Uwazi umeonesha kuwa Chande amekuwa karibu na Ikulu tangu Awamu yaKwanza chini ya Baba wa Taifa, Hayati MwalimuJulius Nyerere na amedumu kujiweka karibu na viongozi wa nchi mpaka awamu hiiya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Wakati inabainishwa hivyo nchini, wachambuzi wa mambo ya jamii za siri, ikiwemoIlluminati na Skull & Bones, wamekuwa wakiitaja Freemason kuwa na njama zakuitawala dunia kwa kuhakikisha kwamba kiongozi mkuu wa kila nchi dunianianakuwa memba wa jamii hiyo.

MKAPA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwamadarakani aliwahi kualikwa akiwa na mkewe katika shughuli ya Freemasonskutimiza miaka 100 nchini, sherehe iliyojumuisha wageni waalikwa 350 kutokanchi mbalimbali duniani japokuwa hapa nchini haikutangazwa sana.
Kwa mujibu wa Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi mkongwenchini, Ernest C. Ambali wa Gazeti la The Guardian, lililokuwa mitaani Oktoba8, 2004 alitaja waziwazi kuwa mgeni rasmi katika shughuli yao ni Rais BenjaminiMkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Katika shughuli hiyo pia walikuwepowafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia, mawaziri n.k.

NYERERE
Sir Andy Chande akiwa nchini Indiakatika Mji wa Chennai kuzindua hekalu lao la East Star, alieleza kwamba maraiswawili wa kwanza wa Tanzaniahawakuwa Freemasons lakini walifahamu taasisi hiyo ni nini na inafanya ninikatika nchi hii.
Aidha, aliwahi kuweka wazi kuwa hata Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiijuataasisi hiyo na aliwahi kuikingia kifua ilipotaka kunyang’anywa jengo laoambalo lipo Sokoine Drive,katikati ya Jiji la Dar es Salaam linalofahamikakama Freemasons Hall.
Uchunguzi umeonesha kuwa viongozi wengi wakuu wa serikali wanafahamu shughuliza taasisi hiyo, hali iliyothibitishwa na kiongozi wa Freemasons, Sir Chandeambaye amekuwa akipiga nao picha mara kwa mara wakati wa hafla.
Viongozi wengine wa nchi waliowahi kualikwa au kumualika kiongozi wa taasisihiyo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, WaziriMkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Rais Mstaafu, Sheikh Ally Hassan Mwinyi.


KITABU CHAKE
Rais mstaafu, Mkapa katika kitabu cha Sir Andy Chande kiitwacho ‘Shujaa waAfrika, Safari kutoka Bukene’ ameandika utangulizi akisema Chande alikuwaakijulikana kama JK na alifahamiana naye baadaya kumuingiza katika bodi ya Shule ya Shaaban Robert.
Mkapa amesema Sir Chande ametambuliwa na kupewa heshima na vyombo vya taifa navya kimataifa, heshima ambayo anaistahili kabisa. “Mimi nafurahi kuhusishwa nakutambuliwa kwa sifa na heshima anayopewa,” alisema Mkapa katika maandishiyake.
Mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye amekuwa akiandikamakala za Freemasons katika gazeti hili, alipohojiwa na mwandishi wetu kama viongozi hao wanafahamu taasisi hiyoinajishughulisha na nini, alisema japokuwa hakuna anayejua wanachokifanyawanachama wa Freemasons huku uraiani lakini anaamini kuwa viongozi wakuu wanchi wanajua kila kitu.
“Kwa kawaida huwezi kualikwa katika chama au taasisi fulani bila kujua shughulizao hasa kwa viongozi wakuu kama hawa, sasa kamawaheshimiwa Mkapa, Mwinyi, Sumaye, Karume na Kikwete waliwahi kualikwa aukumualika Sir Andy Chande ni wazi kuwa wanafahamu shughuli zake na taasisiyake,” alisema Maalim Hassan.

KIMATAIFA
Hivi karibuni, nchini Kenya, aliyekuwa Waziri wa Usalama, Profesa GeorgeSaitoti aliyefariki kwa ajali ya helikopta, kifo chake kimehusishwa naFreemasons kwa kudaiwa kuwa alipokuwa Makamu wa Rais wa Kenya wakati wa utawalawa Daniel Arap Moi, aliwahi kupiga marufuku makanisa au dini zinazojihusisha naimani za kishetani.
Imeelezwa kuwa wengi wanadhani kuwa angeweza kuwa Rais wa Kenya iwapo angegombea hivyokurejesha amri yake ya kupiga marufuku imani ambayo yeye haiamini.
Aidha kuna baadhi ya viongozi duniani wanahusishwa na Freemasons baada yakuonekana picha zao wakionesha alama za taasisi hiyo, baadhi yao ni Rais Barack Obama, George Bush, SadamHussein na Muammar Ghaddafi.

Source: Gazeti la Ijumaa 19 -06 -2012
 
Mtandao mzito huu. Tafuta kwenye internet, web nyingi zimeandika. Nenda You tube utapata na video nyingi zinatoa habari zaidi na za kusisimua. Fanya utafiti huo mkuu.
 
cku zote nimrkuwa nikimind my own busness, maana ukifuatilia sana haya mambo utaumwa kichwa tu, huji kuujua ukweli zadi ya kujua uvumi usio na ushaidi, cha msingi we fuata mambo yako ya wenzako waachie wao maana wawe huko freemason wasiwe hawakuongezei kitu wala hawakupunguzii kitu.
 
Back
Top Bottom