Je, ni kweli tulimuelewa mwalimu Nyerere?

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Katika moja ya hotuba zake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kusema "......katika utawa wangu yapo mambo mazuri tulifanya, lakini pia yapo mambo ya hovyo hovyo tulifanya! Ndiyo tulifanya!!! Sisi ni binadam tulifanya! "

Mwalimu alisema katika hotuba ile kuwa alitarajia kuwa tawala baada yake zingeyachukua yoote mazuri yaliyofanywa na utawala wake na kuyaendeleza huku yale ya hovyo hovyo yakitupiliwa mbali.

Akistaajabia kuzikwa kwa azimio la arusha akasema anashangaa kuona mambo mazuri waliyoyafanya ndio yanaachwa na yale ya hovyo hovyo ndio tunayaendeleza.

Tayari mziki wa Dar mpaka Dom unarindima.

Je, Mwalimu alitumia vigezo vipi kulinganisha jambo la hovyo na jambo zuri?

Kwa muktadha huo, tumejithibitishiaje kuwa tunaendeleza jambo zuri la Mwalimu Nyerere la kuhamia Dodoma (ambalo halikutekelezwa kwa kwenye zama za Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na Kikwete)

Au tunaendeleza jambo la hovyo na tunashindwa kumwambia Amiri jeshi mkuu wetu?
 
Akiwa mgombea hakuwa na dira wala vision akasema anasubiri apewe!! Leo amekuja na kuhamaia dodoma ameitoa wapi? Ameuliza sababu za kuhamia za miaka ile 1973? Je leo zina mashiko???? Ana washauri huyu?? Anakubali kushaurika?? Kuna sababu ya kitaofa kwenda dodoma kwa sasa??mbona azimio harudishi kama kila mamauzi anafuata??
 
Back
Top Bottom