Je ni kweli Mgomo haukuathiri mtihani kidato cha sita?

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema kuwa wanafunzi wanaofanya mtihani wa kidato cha sita na ualimu, walifanya mtihani huo jana licha ya kuwapo kwa baadhi ya waliochelewa kufika katika chumba cha mtihani kutokana na mgomo wa mabasi juzi na jana.

Baraza hilo lilisema kuwa pamoja na kuwapo kwa changamoto ya usafiri, watainiwa hao walianza mtihani huo Mei 4, wanatarajiwa kumaliza Mei 27 mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde (pichani), alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa jumla ya watahiniwa 40, 758 walisajiliwa kufanya mtihani mwaka huu kati yao watahiniwa wa shule ni 35,385 na ualimu ni 19,924.

"Tangu mtihani ulipoanza, mitihani 12 ya kidato cha sita na stashahada ya ualimu hadi jana, imefanyika kwa utulivu na amani katika mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar," alisema Dk. Msonde.

Alisema pamoja na kuanza mtihani huo kukiwa na mgomo wa mabasi ya daladala, watahiniwa walifika katoka vituo vya na kufanya mitihani kwa mjibu wa ratiba ilivyopangwa.

Alisema Necta ilipoona kuna mgomo ilitoa taarifa kwa wasimamizi wasiwazuie wanafunzi watakaochelewa na kufidia muda waliochelewa
.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom