Je ni kweli GPA Kubwa iliniponza!! Nimechemsha au!!

Mkuu pole sana, naona upo katika dimbwi la mawazo kuhusu mafanikio ya wenzako uliokuwa nao school, hata wewe hujachelewa maana mafanikio ni kujipanga na kutekeleza yale unayoitajika kuyatekeleza kama hawa jamaa hapa chini wanavyosema: "There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure." - Colin Powel "The man who follows the crowd will usually get no further than the crowd. The man who walks alone is likely to find himself in places no one has ever been." - Alan Ashley-Pitt "Successful people are always looking for opportunities to help others. Unsuccessful people are always asking, 'What's in it for me?'" - Brian Tracy "If you don't set goals, you can't regret not reaching them." - Yogi Berra "Success is achieved by those who try and keep trying with a positive mental attitude." - W. Clement Stone "A Native American grandfather was talking to his grandson about how he felt. He said, 'I feel as if I have two wolves fighting in my heart. One wolf is the vengeful, violent one, the other wolf is the loving compassionate one.' The grandson asked him, 'Which wolf will win the fight in your heart?' The grandfather answered, 'The one I feed.'" - Blackhawk
 
Kaka shukru Mungu kwamba unayo hiyo elimu ya kutosha na unao huo mshahara uanouita mdogo.Kupata GPA kubwa hakukufanyi uwe tajiri wala maskini.Mimi kwa mtazamo wangu ukiwa na kazi ya uhadhiri na bado ukawa maskini ni kama unajitakia vile...uhadhiri ni moja ya ajira chache Tz zenye mshahara wa kueleweka zaidi ya hapo wahadhiri mnakuwa na muda mwingi sana free kuweza kuendesha miradi yako binafsi../.Natamani ningekuwa na hizo GPA nipate kazi ya uhadhiri.Buni miradi itakulipa,kuenedelea kujilinganisha na wenzako kutakuletea pressure bure...

Huo muda mwingi sana free ni muda gani ndugu huo unaouongea. Mtu unafundisha darasa la watu si chini ya 150, 200 wengine mpaka 500 kwa darasa moja tu, na bado utakuta una madarasa mawili mpaka matatu kwa semester, uwatungie test, Exam, umark karatasi za idadi hiyo ya wanafunzi. ufanye kazi za ziada za kitengo chako bado kuna sup etc etc etc. huo muda mwingi sana wa free unaouongea ni upi ndugu, kama sio fitina hizo!!, ungejua kwamba sisi hatuna weekend, usiku wala mchana. usingethubutu kusema kitu kama hicho. Wengi wahadhiri wamejaliwa uvumilivu tu lakini najua ipo siku watashindwa kuendelea kuvumilia.

Hata huo Muda wa kufanya hizo research, biashara zingine mtaani, sijui mtu unautoa wapi. Jamani hebu acheni fitina, Kiatu ambacho hujakivaa usiseme kitakutosha.
 
Kaka maisha ni kuchagua,sijui wewe ni mhadhiri wa chuo gani na umeingia mkataba wa aina gani na muajiri wako ila mimi nimesoma chuo ambapo wahadhiri wenye michongo yao mtaani nilizoea kukutana nao darasani tu baada ya hapo hawaonekani chuo au wala ofisini isipokuwa wale wachache wasio na michongo ndo nilizoea kuwaona wakishinda maofisini wakisoma magazeti na kusambaza ukuda kwa wanafunzi.Kama waona ajira yako inakubana sana na haikupatie kile unahitaji hauna sababu ya kulalamika sana,piga chini kazi ujaribu maisha mengine mtaani ila be aware hata huku mtaani kwa waliojiajiri kuna kupata na kukosa na ukiendelea kulinganisha mafanikio yako na yale ya wenzako utaishia frustrated.Fanya maamuzi sahihi,GPA yako haihusiki kwa vyovyote hapo tatizo itakuwa ni uwezo wako wa kuchagua......kama uliingia ukawa TA ukaona ubaya wa kazi yako bado ukaenda masters na Phd na ukaona hao maprof wanaotaabika (ambao si wote,nawajua maprof wajanja wenye mkwanja aibu) .Samahani ulifanya phd yako katika field gani?
 
Sitasahau ushauri niliopewa na rafiki yangu mmoja.Yeye ana masters.Alinambia,'ukitaka kua na maisha mazuri,usiwe na elimu ndogo sana wala elimu kubwa sana,kuwa na elimu ya kawaida tu e.g degree level au masters level inatosha.
 
Usikate Tamaa ingia REDET kama mkandara mambo yako yatakua safi tu,kuna jamaa tulimaliza nae chuo miaka hyo alikua na Bonge la GPA alisaga lami mwaka na nusu mtaani.

Kama uliniona vile mkuu, mi mwenyewe mule mule ila i hope one day Mungu atafungua mlango.
 
Huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wala hana PHD kama anayo basi ya kwenye mtandao. Maisha na kufahuru wapi na wapi, wangapi hawajasoma kabisa na ni matajiri

Na mvivu maana maprof. siku hizi wanatengeneza pesa nzuri sana kwa kufundisha vyuo mbali mbali

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

sasa wewe ndo unaonesha umaskini wa mawazo kabisaaa! eti maprofesa wanaingiza ela kwa kufundisha vyuo vingi,nani kakwambia inalipa? iyo ela unayoita nyingi kwa majukumu ya mtu mzima ni viela vichache sana ukilinganisha wazo la mleta mada wakati anajilinganisha na mjasiliamali....yani hata profesa afundishe vyuo vitano kwa siku bado hailipi na yet returns on hihgly invested brain is almost at break even kwa kuwa mtu anaji over work ili ku make!.......ki ukweli hata mimi nlipata wakati mgumu sana kufikiria kwa nini maisha yanatight ivi baada ya kukaa sana darsani wakati colleagues washatangulia a lot of miles ahead!ukichukua rate ya per hour lecture,ukajua msaa magapi per day times days in a month plus other allowances bado unashindana na muuza mitumba mchikichini ambaye anaweza kuingiza net profit ya 2mil per month,anaanza biashara saa3 au 4 na kufunga saa 11 jioni daily wakati wewe ni wa kwanza kuamka na wa mwisho kurudi kwa familia yako...SOMETIMES LETS CALL A SPADE A SPADE...UALIMU ni wito,yani ktk maisha hautaishi kama maskini wala hautawaishi kuishi ktk maisha ya satisfaction, kama una malengo makubwa kimaisha unaweza kuhisi umepotea!Kwa mfumo wa taifa wa thamani ya elimu apa nchini haumpi msomi maendeleo,yet ukichukua salary slip hata ako kasungura na allowance hukatwa kodi kama kukomoana ivi...mfano nikijitolea mfano mimi,yani kodi per salary ni kubwa zaidi ya mara 3 ka kima cha chin cha serikali,yani kwa mfumo huu nawalipia mishahara watumishi zaidi ya wawili wa kima cha chini cha gvt....KI UKWELI ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA ILA SI MAISHA YENYEWE,hii si kukatishana tamaa ila ndo ukweli mchungu,pia ojeni uone,you shall testify!
Gsana.
 
Nashawishika kuungana na wazo la Jamco. Sidhani kama mtu aliyesoma akapata GPA kubwa, akaenda masters na PhD anaweza kuwa na hoja nyepesi ivyo eti ashauriwe aache kazi! Duuh, pia nimeisoma michango ya wadau wengi hapa it seems most of you are not aware of the difference between "rich person" and "wealthy person".
 
Sidhani kama wewe na huyo mwenzako kama mmeelewa mada!. mnatumia akili ipi kusoma!!!.
 
sasa wewe ndo unaonesha umaskini wa mawazo kabisaaa! eti maprofesa wanaingiza ela kwa kufundisha vyuo vingi,nani kakwambia inalipa? iyo ela unayoita nyingi kwa majukumu ya mtu mzima ni viela vichache sana ukilinganisha wazo la mleta mada wakati anajilinganisha na mjasiliamali....yani hata profesa afundishe vyuo vitano kwa siku bado hailipi na yet returns on hihgly invested brain is almost at break even kwa kuwa mtu anaji over work ili ku make!.......ki ukweli hata mimi nlipata wakati mgumu sana kufikiria kwa nini maisha yanatight ivi baada ya kukaa sana darsani wakati colleagues washatangulia a lot of miles ahead!ukichukua rate ya per hour lecture,ukajua msaa magapi per day times days in a month plus other allowances bado unashindana na muuza mitumba mchikichini ambaye anaweza kuingiza net profit ya 2mil per month,anaanza biashara saa3 au 4 na kufunga saa 11 jioni daily wakati wewe ni wa kwanza kuamka na wa mwisho kurudi kwa familia yako...SOMETIMES LETS CALL A SPADE A SPADE...UALIMU ni wito,yani ktk maisha hautaishi kama maskini wala hautawaishi kuishi ktk maisha ya satisfaction, kama una malengo makubwa kimaisha unaweza kuhisi umepotea!Kwa mfumo wa taifa wa thamani ya elimu apa nchini haumpi msomi maendeleo,yet ukichukua salary slip hata ako kasungura na allowance hukatwa kodi kama kukomoana ivi...mfano nikijitolea mfano mimi,yani kodi per salary ni kubwa zaidi ya mara 3 ka kima cha chin cha serikali,yani kwa mfumo huu nawalipia mishahara watumishi zaidi ya wawili wa kima cha chini cha gvt....KI UKWELI ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA ILA SI MAISHA YENYEWE,hii si kukatishana tamaa ila ndo ukweli mchungu,pia ojeni uone,you shall testify!
Gsana.

mkuu hii kitu hapo juu ndo ile katika labour economis tunaiita REAL WAGE.
 
Ni kweli hali ya hawa jamaa si nzuri vile tunafikiria. Ila wengi ni wapole mno na wamegawanyikagawanyika, wapo wenye nazo sana ambao nadhani ndio inaonekana kama vile wote ni mambo safi. Lakini kumbe wengi wao ni shida tupu!!. Wengi ambao ni mambo safi inategemea na background za familia zao au uwezo wa wenza wao kutokana na kazi wanazofanya. Lakini wale ambao wanategemea ualimu moja kwa moja ni bila bila.

Mi ushauri wangu kwa BIG Banned, kama unaona hauridhiki na una uwezo wa kupata kazi nzuri zaidi. CHAPA LAPA haraka iwezekanavyo. Siku serikali ikaona kuna umuhimu wa kuboresha masilahi kwa wahadhiri, na ikafanya hivyo, rudi.
 
1. Lakini pia ni wavivu kuchanganyika na watu wa kitaa hawa wasomi wetu......wanajiona special na wanadhani wanajua mambo mengi eti.....jamani eenh mafanikio ya ofisini yanapatikana kwa watu wachache saaana ambao wanapata gud pay.....wengi ni deal tu kwenda mbele na hawa wasomi wengi sio wazuri kwenye mishe za kitaa ambazo ndo zinatusua

2. Wahadihiri wamezoea superiority huko vyuoni na baadhi wanakuwa na attitude flani kama ya mtoa mada kwamba amesoma so anatakiwa awe juu kimapato n ol that ndo maana wakija huku kitaani hata wakipewa michongo wanaona kama sio ya hadhi yao vile......jishusheni kidogo na mjue Street Uni. inasongaje kwa Bongo hapa
 
Nimesoma kwa makini maelezo yako mkuu, kwa mtazamo wangu naona kuwa wewe kama mhadhiri hujajitambua unapaswa kufanya nini! Pia hiyo PhD haijakusaidia bado. Ninavyoelewa kazi ya mhadhiri siyo kufundisha tu kama unavyoeleza wewe. Mhadhiri anatakiwa afanye tafiti, na consultancy mbalimbali. Kufanya tafiti ni muhimu kwa mhadhiri kumbuka, tafiti hizi ndizo zitakuongezea kipato na kukuwezesha kutoa machapisho, yatakayokusaidia kupanda cheo na ngazi ya mshahara. Kazi za Consultancy pia zina fedha, inategemea tu Network yako na ushirikiano wako na wenzako. Inaonesha kuwa wewe huna chapisho hata moja kwani unafundisha tu! Kumbuka "you either publish or perish" Je Chuo chenu kina " journal? " Research policy je? Research funds je? Yawezekana pia tatizo lisiwe lako kwani kama Chuo hakitilii mkazo masuala ya reserach basi wahadhiri mtakuwa kama mwafundisha sekondari! Sincerely, nakupongeza kwa kuwa na Phd. Please usikate tamaa kiasi hicho na kuona umepoteza muda. Ni wewe mwenyewe tu sasa ujue kuitumia hiyo elimu uliyoipata.
 
Mkuu kuna mtu alisema pale ambapo haupo ndo pazuri, ukiwauliza hao unaosema wana maendeleo utakuta nao wanatamani kuwa na phd kama wewe (kama nimekuelewa vizuri unayo phd), na wewe unawatamani pia.

Lakini niseme hivi, maisha (i.e kupata mali) hakuna fomula kabisaaaaa, ukiangalia vizuri kuna wengine uliwaacha miaka hiyo 6 na hawajafanya chochote, si shule si utajiri, mambo yao bado magumu. So nakushauri wala usikate tamaa, furahia phd yako, kuwa na matumaini, weka malengo na kwa kuwa umesoma vya kutosha nakuhakikishia unaweza kutoka ndani ya miaka 2 au 3 ukawapita hao unaowaona wameendelea sana, ila fanya kazi kwa moyo na watendee haki wateja (students) wako.
Ila pia kila mtu anayo maisha yake, Mungu ni mwema kwa kila mtu haijalishi, so its fine to be challenged and put effort to archieve but dont be jealous, trust God he gave u a phd he will give u the rest of your good desires on due time.

Excellent!
 
Nilimaliza chuo miaka kadhaa iliyopita na sasa ni mhadhiri chuo kimoja hapa TZ. Ukweli ni kwamba GPA nzuri (ambayo sasa mi naiita mbaya!) ndio iliyonifanya nishawishiwe na kushawishika kubaki hapo nilipo!, Nikapata nafasi ya kwenda kusoma masters then PhD kwa takriban miaka kama 6 hivi. Tulipomaliza Undergrad kama kawaida watu/classmates tulitawanyika kila mtu kutafuta maisha kwa namna yake. Sasa kwahiyo miaka sita niliyopoteza kwa kusoma, wenzangu walibaki nchini wengine walipata kazi serikalini, wengine kampuni binafsi ambapo huko ni watu wenye vyeo na experience nzuri sana. Ukiachana na hayo ukweli ni kwamba wenzangu wapo mbali sana kimaisha kiasi kwamba nahisi mimi kama vile nilipotea au ile GPA niliyopata ndio iliniponza ingawa kwa wakati ule nilijihisi mi ndio mwenye bahati, lakini naona ni tofauti kabisa hasa nikijilinganisha na wenzangu na hiyo miiaka sita nimefanya maendeleo gani, wenzangu wana mengi sana ambayo mi ndio nafikiria kuanza.

Mbaya zaidi uhadhiri haulipi kabisa, yani ni kutegemea mshahara tu!. Na nikiangalia masenior wangu (Professors etc) hawana maendeleo yoyote, wanalia na njaa tu, wapo wanahangaika na vibiasharabiashara vidogo ambavyo kweli vinachangia kwa wahadhiri wengi kutojiandaa vizuri wanapoingia madarasani kufundisha. Maisha na heshima ya mwalimu wa chuo ni vitu viwili tofauti kabisa (sivyo vile watu wanavyofikiria)!.

Kweli uwalimu ni wito!, lakini kama hauridhiki na unachokipata na hauwezi kujikwamua na maisha magumu na majukumu ambayo unayo kila siku, kweli uwezekano wa kufunza tu ilimradi siku ziende utakuwepo tu miaka yote, sababu utakuwa unatumia muda mwingi kufanya madili mengine nje na kazi ya kufundisha.

Je ni Kweli GPA kubwa iliniponza!! Niache hii kazi nitafute nyingine!!.

Du! una PHD kweli wewe? mbona hoja yako kama hujasoma?

Hakuna utajiri hapa duniani kama elimu. uliowaacha na unaodhani wamefanikiwa wengi wao niwezi na mafisadi.
Lakini pia labda ungetuelewesha una define vipi maendeleo.
Baada ya hapo ndo tuendelee na mada. Lakini kama una maanisha nyumba na gari basi sina la kusema.
Ushauri wangu:
Tumia vizuri phd yako na kuorodhesha matatizo a yako halafu ya transform to OPPORTUNITIES! Fikiri kama mtu mwenye PHD! soma magazeti kuna requests kibao za ku express interests.
Tumia KALAMU na kichwa chako kutunisha mfuko wako wakati ukiendelea na kazi yako ya uhadhri lakini kwanza tuambie MAENDELEO NI NINI?

ALAMSIKI....PROFESA KILAZA
 
Nilimaliza chuo miaka kadhaa iliyopita na sasa ni mhadhiri chuo kimoja hapa TZ. Ukweli ni kwamba GPA nzuri (ambayo sasa mi naiita mbaya!) ndio iliyonifanya nishawishiwe na kushawishika kubaki hapo nilipo!, Nikapata nafasi ya kwenda kusoma masters then PhD kwa takriban miaka kama 6 hivi. Tulipomaliza Undergrad kama kawaida watu/classmates tulitawanyika kila mtu kutafuta maisha kwa namna yake. Sasa kwahiyo miaka sita niliyopoteza kwa kusoma, wenzangu walibaki nchini wengine walipata kazi serikalini, wengine kampuni binafsi ambapo huko ni watu wenye vyeo na experience nzuri sana. Ukiachana na hayo ukweli ni kwamba wenzangu wapo mbali sana kimaisha kiasi kwamba nahisi mimi kama vile nilipotea au ile GPA niliyopata ndio iliniponza ingawa kwa wakati ule nilijihisi mi ndio mwenye bahati, lakini naona ni tofauti kabisa hasa nikijilinganisha na wenzangu na hiyo miiaka sita nimefanya maendeleo gani, wenzangu wana mengi sana ambayo mi ndio nafikiria kuanza.

Mbaya zaidi uhadhiri haulipi kabisa, yani ni kutegemea mshahara tu!. Na nikiangalia masenior wangu (Professors etc) hawana maendeleo yoyote, wanalia na njaa tu, wapo wanahangaika na vibiasharabiashara vidogo ambavyo kweli vinachangia kwa wahadhiri wengi kutojiandaa vizuri wanapoingia madarasani kufundisha. Maisha na heshima ya mwalimu wa chuo ni vitu viwili tofauti kabisa (sivyo vile watu wanavyofikiria)!.

Kweli uwalimu ni wito!, lakini kama hauridhiki na unachokipata na hauwezi kujikwamua na maisha magumu na majukumu ambayo unayo kila siku, kweli uwezekano wa kufunza tu ilimradi siku ziende utakuwepo tu miaka yote, sababu utakuwa unatumia muda mwingi kufanya madili mengine nje na kazi ya kufundisha.

Je ni Kweli GPA kubwa iliniponza!! Niache hii kazi nitafute nyingine!!.

Pole sana mkuu aliyeseam ujanja kupata si kuwahi alikuwa na maana sana. Tanzania imekuwa corrupted na siasa. Miaka sisi tunasoma ilikuwa kubakizwa kuwa mwalimu wa University ni big deal na wengi walikuwa wanaishi maisha mazuri sana na yenye mafanikio. Kinachoua elimu Tanzania ni greed ya wanasiasa siku hizi utakuta mshahara wa mwanasia mwenye elimu ya darasa la saba aliyejipachika katika nafasi ya uongozi kwa uwezo wa kuchonga mdomo na kusifia waliopo juu yake anaishi maisha ya hali ya juu sana. Ndiyo maana ukiangalia watu wanakimbia chaki madarasani na kukimbia profession zao kuingia kwenye siasa na kugombea ubunge.

Wanasiasa wanajilimbikizia malipo ya kufuru huku watu waliotumia muda wao kusoma kwa ajili ya Taifa wakibakia kuwa ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa wanasiasa wenye elimu duni dhidi yao. Nchi yetu imekuwa haiheshimu tena wataalam ndiyo maana wengi wa wataalam wame-compromise taaluma kwa kuwasikiliza wanasiasa wenye uelewa finyu na hata wakati mwingine kudiriki kuwafuata wanavyotaka mradi tu wasipoteze nafasi za kupata hata hicho kidogo.

Bado ninaamini kabisa kama tuna nia ya kuwa-retain watu kama wewe kwenye elimu ya juu tunatakiwa kuwaonesha kuwa education pays. Otherwise sooner or later utajikuta na wewe unapata mawazo ya kupanda jukwaani na kuizika taaluma yako, matokeo yake taifa linazidi kushuka chini. Tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanataaluma kuingia kwenye siasa maana ndipo kunalipa kwa sasa. Ukiangalia baadhi ya taaluma za wabunge waliopo bungeni leo utaona kuwa unaweza kutoa Univeristy moja yenye kukamilika kwenye kila nyanja kwa jinsi wanataaluma walivyojikita huko.

Lakini hata hivyo usikate tamaa, kama una PhD unaweza tafuta kazi nchi zinazothamini elimu kama Botswana na hata Rwanda na kujikuta miaka yako mitatu tu unakuwa sawa na wale uliomaliza nao undergrad. Wao wansisitiza uzalendo huku wakijilimbikizia, its time sasa na wewe kutafuta sehemu muafaka nchi ikitengemaa utarudi kuijenga.

Wanasiasa wanathamini wale watu wanaofanya na kudumisha uwepo katika madaraka kama vile majeshi, polisi tena wale wenye vyeo vya juu. Mwalimu kama wewe unaonekana si lolote kwani suala la elimu bora au duni haliathiri madaraka yao. Mkianza kukimbilia kwenye nchi zenye masilahi kwa wenye taaluma huenda watastuka.

Bonus video hiyo chini, ukiwa na taaluma ni kama vile huyo mwenye convertible car body, hata mtu akikuwahi vipi utapark gari na kumuacha akihangaika kutoka.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma kwa makini maelezo yako mkuu, kwa mtazamo wangu naona kuwa wewe kama mhadhiri hujajitambua unapaswa kufanya nini! Pia hiyo PhD haijakusaidia bado. Ninavyoelewa kazi ya mhadhiri siyo kufundisha tu kama unavyoeleza wewe. Mhadhiri anatakiwa afanye tafiti, na consultancy mbalimbali. Kufanya tafiti ni muhimu kwa mhadhiri kumbuka, tafiti hizi ndizo zitakuongezea kipato na kukuwezesha kutoa machapisho, yatakayokusaidia kupanda cheo na ngazi ya mshahara. Kazi za Consultancy pia zina fedha, inategemea tu Network yako na ushirikiano wako na wenzako. Inaonesha kuwa wewe huna chapisho hata moja kwani unafundisha tu! Kumbuka "you either publish or perish" Je Chuo chenu kina " journal? " Research policy je? Research funds je? Yawezekana pia tatizo lisiwe lako kwani kama Chuo hakitilii mkazo masuala ya reserach basi wahadhiri mtakuwa kama mwafundisha sekondari! Sincerely, nakupongeza kwa kuwa na Phd. Please usikate tamaa kiasi hicho na kuona umepoteza muda. Ni wewe mwenyewe tu sasa ujue kuitumia hiyo elimu uliyoipata.

Soma comment no. 32
 
Back
Top Bottom