Je! ni kweli dunia inazunguka jua?

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,704
39,781
tumesoma kwenye jografia kua dunia inazunguka jua hivyo tunapata majira ya mwaka kama kiangazi na masika je ni kweli? galileo alikuwa sahihi?

Fikra ya kawaida
chukulia umepanda ndege au hellcopter halafu unaenda marekani then ile hellcopter ikasimama juu angani kwa muda mrefu lets say mwezi mmoja, je dunia itakuacha? kama haikuachi hio dunia inazungukaje kwenye orbit? na zile satelite ambazo zipo angani kama dunia inazunguka kwenye orbit mbona hatuzigongi? tunaambiwa dunia inazunguka kwa speed kubwa sana ina maana satelite zinamatch speed ya dunia?

Theory ya taycho brahe
Jamaa huyu mdanish (denmark) alitoa theory yake ambayo inamashiko tu

-sayari nyengine kama mercury na venus zinazunguka jua
-then jua na mwezi vinazunguka dunia

Tychonian_system.svg

Kama theory ya juu ipo sahihi inamaana hata dunia haizunguki bali jua ndio linatuzunguka.

Mnaonaje hii ipoje? kuna mtu ana point za kuprove kuwa galileo yupo sahihi?
 
Chief-Mkwawa,

Kwanza tambua ya kwamba Sayari yetu ya Dunia inazunguka kwenye muhimili wake, halafu unavyoruka na ndege bado umo Duniani sasa kwanini Dunia ikuache wakati wewe umo ndani yake?

Dunia haiwezi kukuacha wewe ndiyo unaweza kuicha Dunia kama ukifikia mwendo (escape velocity) fulani then utatoka kwenye Sayari ya Dunia na kuingia space!

Satelite kwanza haipo Duniani na kila Sayari ina njia yake, ukikokotoa Kepler's Equations nafikiri kanuni ya pili ya Kepler itakwambia pamoja na Gravitational Law utapata jibu ni kwanini sayari zinabakia kwenye njia zake na hazianguki!

Last edited by a moderator:
limetumbuka,

Mfano nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?

halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?

satelite.jpg
 
Last edited by a moderator:
mfano nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?

halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?

satelite.jpg
Man you need to learn Astrophysics!
Gari linakimbia Speed gani na linakuwa limesogea umbali gani unapokuwa juu? Thats one question out of many you should have asked!

Hilo la Sayari kazisome tena utagundua statement yako iko too amateurish. Inaonekana eneo hili unahitaji kujisomea kwanza!
 
ndo nahitaji hio elimu kaka, mimi sipingi/kubali kitu hapa, na ndio maana ya kuanzisha hii thread
 
mfano nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?

halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?

satelite.jpg

Ukiwa ndani ya bus linaloenda, halafu ukaruka juu unadhani utatua wapi? You will land at same spot you launched from as long as the bus is moving with un accelerated velocity, its Newton's first law of motion or inertia
 
yap nakubali nitatua pale pale ila basi litaniacha litakuwa mbele si sawa?

dunia inajizungusha kwenye orbit kwa kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa, ina maana kama nimepanda hellcopter nikasimama juu angani kwa sekunde 10 basi dunia ingeniacha kilomita 300, je kwanini hainiachi?

na hawa nasa wanapotuma vifaa nje ya dunia vikirudi haviji sehemu ile ile vilipotokea? maana dunia inakuwa imeshamove pale ipo eneo jengine. au ni changa la macho tu tunapigwa
 
mfano nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?

halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?

satelite.jpg

kuhusu hilo la kuwa juu ya gari then ukaruka hata kama gari linatembea utatua palepale gari lilipofika so halitakuacha otherwise uwe uliruka kiupande (hiyo ipo proved kwenye physics). kuhusu satellite ni kwamba zipo juu sana ndio maana hutuzigongi.

kila satellite ina speed yake katika kuzunguka dunia na kumbuka kuwa kuna nguvu ya uvutano kati ya dunia(ni kwa sayari zote) na jua sasa satellite huwa zinawekwa pale katikati ambapo nguvu ya uvutano ya dunia na ya jua zinapokutania hivyo haziwezi kuvutwa na jua wala dunia, position pia huwa inategemea na spidi ya satellite husika.

na ndege mara zote husafiri ngani ya anga ambamo inakuwa ni kama inavutwa na dunia vile, sasa kwa mfano helicopter isimame angani kwa siku nyingi haiwezi kuachwa na dunia licha ya kwamba dunia inazunguka jua, dunia huwa anahama na kila kitu kilicho ndani ya eneo ambamo nguvu yake ya uvutano imeenea (earth's attraction force) labda ikotee hiyo helicopter imevuka hili eneo ndio itaachwa na tutabaki kusema ndege imepotelea angani.

Spidi ya dunia kuzunguka jua ni kubwa(kilometa 30 kwa sekunde) na mzunguko mmoja wa dunia kwenye obiti kuzunguka jua ni zaidi ya kilometa milioni 940, hivyo licha ya spidi kubwa dunia inachukua zaidi ya siku 365 kuzunguka jua mzunguko mmoja.
 
yap nakubali nitatua pale pale ila basi litaniacha litakuwa mbele si sawa?

dunia inajizungusha kwenye orbit kwa kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa, ina maana kama nimepanda hellcopter nikasimama juu angani kwa sekunde 10 basi dunia ingeniacha kilomita 300, je kwanini hainiachi?

na hawa nasa wanapotuma vifaa nje ya dunia vikirudi haviji sehemu ile ile vilipotokea? maana dunia inakuwa imeshamove pale ipo eneo jengine. au ni changa la macho tu tunapigwa

Hebu soma vzr ulichoandika.

Rotational speed = 30km/h

After 10 seconds

Distance covered ???

Pia kuna tofauti ya rotational and translational motions.

Wanna be the philosopher? Welcome to my world.
 
Danny Job,

Sure it make sense kwenye nguvu ya uvutano, je kwa nasa, china na urusi ambao wanatuma vyombo kwenye anga za juu wakirudi hawaikuti dunia pale walipoiacha? inakuwa imesogea kwengine?

na zile picha za toka anga ya juu mbona sjawahi kuona hata moja ikionesha dunia yetu ikizunguka kwa speed?
 
Last edited by a moderator:
Hivyo vyombo/ space craft ambazo zinaenda anga za juu huwa zinakuwa controlled na watu walioko chini(duniani) hivyo katika kutua huwa wanavi'direct wanakotaka wao hivyo vitaland hapahapa duniani..
 
limetumbuka,

Mfano nipo juu ya gari then nikaruka juu basi gari litaniacha na mimi nitadondoka chini, iweje ndege imeruka ipo juu uniambie ipo duniani bado?

halafu na satelite (man made sio sayari) si zipo juu ya dunia why hatuzigongi?

satelite.jpg

Satelite hazitugongi kwa maana zinafuata kanuni za Kepler na Gravitation nazo pia zinaingia kwenye njia yake (orbit) hivyo kama ilivyo Sayari yetu ya Dunia nazo satelite pia zina njia yake na hakuna kugongana kama ukijaribu kuderive kanuni za Kepler ukachanganya na Kanuni ya nguvu za Uvutano (gravitational) utapata jibu!

Kumbuka kwanza hata Mwezi bado uko ndani ya Sayari ya Dunia ambapo ni kama kilometa 400 000 (laki nne) ktk kwenye Sayari yetu ya Dunia, hivyo maadamu hiyo Ndege iko ndani ya Sayari ya Dunia bado itabaki kuwa Duniani na Dunia haiwezi kuiacha ndege kwa maana Dunia inazungunguka kwenye Muhimili wake na haihami sema wewe ndiyo unaweza ukaicha Dunia na kwenda Sayari nyingine au hata kwenye Nyota ya jua kama ukiweza!
 
Back
Top Bottom