Je, ni kweli Bush kanunua kiwanja Kigamboni?..

Mkuu Mkandara,

Kweli Bush ataenda Tanzania bila ya media yoyote ya Tanzania kujua?

Inawezekana amenunua ardhi lakini sidhani kama ameenda TZ kimya kimya.

Pia kama ni kweli amenunua ardhi TZ ni jambo zuri. Hata kama simpendi Bush lakini jambo lolote ambalo linaweza kuwaongezea mlo Watanzania wenzangu hata kama ni wachache mimi nitaliunga mkono.

Kitendo cha mtu kama Bush kukaaa TZ hata kwa wiki moja tayari kuna Watanzania kibao wanaweza kufaidika.

So far what I know, hizi media zetu bado ni waoga, na wanatishwa sana tu, kuna ishu nyingi saan ambazo hawawezi wakaziandika, waulize wenyewe.

Bush ni mmoja wa wamiliki wa BARRICK GOLD COMPANIES, na TRA hawanusi pua kule!!! waliowahi kunusa pua walikiona cha moto, nchi ishauzwa hii, muulize Kikwete risiti!
 
So far what I know, hizi media zetu bado ni waoga, na wanatishwa sana tu, kuna ishu nyingi saan ambazo hawawezi wakaziandika, waulize wenyewe.

Bush ni mmoja wa wamiliki wa BARRICK GOLD COMPANIES, na TRA hawanusi pua kule!!! waliowahi kunusa pua walikiona cha moto, nchi ishauzwa hii, muulize Kikwete risiti!

Mkuu,
1. It is very possible sana kwamba Bush alikuja TZ bila hata knowledge ya media. Nakumbuka clinton alishakuja Arusha kimya kimya akashukia hoteli moja ambapo my sister was working there. So sishangai kwani hawa watu tukumbuke pia wana private life yao mbali na being popular.

2. Yap, I know barrick gold very well, Bush is one of the shareholder of the parent company which is based in Toronto Kanada. This guys have so many subsidiaries all over the world. Like you and me we can as well be owners of barrick through buying shares in the stock exchange so to me by bush being the owner is not really a big deal.

3. Unavyosema "TRA hawanusi pua kule" nakataa nakataa nakataa kabisa na nina evidence. TRA wako vizuri sana na they are tacxing those guys kama kawaida. I know tena kwanza TRA wamechukua more than what they were supposed to take from them and there several tax appeals by the company taking as whole in tanzania as they own several mines. So kusema TRA hawaendi huko Bro hapa umekuwa so unprofessional. I am very sure about it. Remember that is the multinational compan existing in many countries, so hawawezi kuwa na issue za tax disputes.

4. Sasa the problem iliyopo juu ya barrick sio barrick it is our government. Ile mikataba tulioingia nao ndo ina matatizo makubwa to the extent watanzania hatufaidiki kama nchi nyingine. Nimebahatika kuiona baadhi ambayo you could see kwamba jamaa ndo walio draft sie (tz) tukasign tu bila kuangalia vipengele vinasemaje. So it is us not them, they did it because of our loose management. Unaweza kuona tu the AG was Andrew Chenge so you can draw your conclusion.

Naomba kuwakilisha.
 
Mtanzania,
Mkuu kwanza heshima mbele..
Hizi ni habari za tetesi nilizozipata toka kijiweni hapa na ndio maana nimetaka kuuliza wana JF kama wana taarifa hizi..
Kuhusuiana na kuja kwa Bush kimya kimya mkuu wangu hilo linawezekana kwani hata Jimmy Carter alipomaliza urais wake alikuja TZ kimya kimya na ardhi ambayo alijishughulisha na kilimo cha ngano.. hadi leo hii navyozungumza sijui eneo alochukua wala huo mradi umemsaidia nini Tanzania!..Mbali na tetesi nyingine kuwa Carter alikuwa na foundation iliyohusiana na Utalii wa kupanda milima..
Miaka imekwenda, Tanzania kubwa na siwezi kufuatilia habari kama hizi kama vile ndio maisha yangu..kuhusiana na Barricks mkuu wangu mbali na viongozi wetu hawa jamaa wanafahamika dunia nzima kwa Unyonyaji...Makosa yameanza pale tu tulipowakaribisha wao tukifikiria kwamba ni Wawekezaji..Hili neno wawekezaji, linatumika vibaya sana kwani tunaishi kama dangulo ambalo fedha ndio inapewa thamani kuliko utu wetu..
Sasa nachotaka mimi kuelewa hapo Kigamboni kuna kitu gani ambacho Bush anaweza kuwekeza kiasi kwamba wananchi waporwe ardhi na kumpa Bush ambaye kiutaalam hana expertise nje ya Urais wake... hana elimu zaidi ya kushinda mtihani akiwa mwanachama wa Skull..Hata kusimamia visima vya mafuta vya baba yake vilimshinda..Nakuomba tazama sinema inayoitwa W...Utamfahamu vizuri Bush.. ni Kabuntas!..

Mkuu Mkandara,
Safari zote za Carter kwenda TZ na hiyo foundation yake ya kupanda mlima Kilimanjaro zilikuwa zinajulikana. Labda kama ulikuwa hufuatilii habari za TZ. Sio rahisi rais wa zamani wa USA aende TZ na kurudi bila hiyo habari kujulikana. Safari kama hizo zinaongozana na ulinzi mkubwa hivyo mwishoni habari hujulikana hata kama ni baada ya kiongozi huyo kuondoka. Kila Carter anavyopanda mlima Kilamanjaro, kuna watanzania wanafaidika. Hata kama ni kumi au 20 bado ni Watanzania. Cha kuangalia ni je madhara ni makubwa kuliko faida? Kama faida ni kubwa mimi nitaunga mkono. Kama Bush amenunua ardhi kwa bei halali, kwanini sisi wengine tuone ni issue? Nitaona kuna issue kama wananchi watanyang'anywa ardhi rao bila malipo.

Mimi sina matatizo kabisa na kukaribisha investors, matatizo makubwa yako kwa viongozi wetu ambao wametoa our natural resources kwa bei za kutupwa. Biashara yoyote ni negotiations. Kila mtu anataka kupata faida kubwa kuliko mwingine, ukilala, unaliwa. Hata umlete nani, kama hujui kutetea maslahi ya taifa, nchi italiwa tu.

Bush kuwa kilaza haina maana hawezi kufungua investment ya maana. Biashara kama hizo sio biashara za duka za kwamba lazima usimamie mwenyewe. Hata hivyo Bush sio mjinga kama mnavyotaka kujidanganya. Mimi simpendi Bush lakini pia nitakuwa very naive nikiamini Bush ni mjinga kama wanavyotaka tuamini kwenye hizo sinema. Mtu aliyesimama jukwaani zaidi ya mara tatu hawezi kuwa mjinga hivyo.

Naona kama tunaanza kuwa anti investors. Kama hatutaki wageni, basi sisi Watanzania tuchangamkie hizo opportunities zilizopo badala ya kupiga kelele tu. Pia tuwawajibishe viongozi ambao wanauza mali zetu kwa bei za chini na huku wao wakichukua rushwa.
 
Mimi nia kiwanja kigamboni lakini sijaambiwa kitu na last time went there watu wanaendelea na ujenzi kama kawaida, mimi nipo tuangoma perhaps ni somewhere else lakini nafikiri si habari za uhakika

Tuwangoma haipo ktk Hili...Mradi mpya hauhusu viwanja 20,000 vya Tuwangoma na Kibada. Unapojadili tetesi hizi ni vema tukaelewa hilo
 
Mtanzania,
Mkuu wangu, nitakubaliana na wewe tu ikiwa wewe una present upande wa pili wa shilingi na sio kwamba unaamini kabisa kuwa kuna jema linalotegemewa toka kwa Bush..
Kwenye swala la Dowans ungetupeleka kubaya sasa kama yungekusikia wewe, sasa umeanza na hili la Bush!..Inaonyesha wazi unashindwa kutazama nyuma ya pazia..

Mkuu sio kweli kabisa rais mstaafu wa Marekani huwa na walinzi mkubwa kama unavyodai..Carter alikuja hapa kuuza kitabu chake na watu tulikwenda kupata signature yake, pembeni mwake kulikuwa na mtu mmoja tu tena hatukufanyiwa search kabla hujamsogelea jambo ambalo lisingewezekana kabisa kama angekuwa rais bado..
Ningeweza kabisa kumchapa kibao kama ningekuwa mkereketwa...haya umeambiwa hata Clinton kisha tinga Bongo bila safari yake kuwa kichwa cha taarifa..Hii ndiyo tofauti kati yetu na hawa jamaa...na nina hakika huwezi kunambia carter mara ya mwisho ametinga lini Bongo iwe kupanda mlima au kuendelea na shughuli zake za biashara..
Kweli kabisa nakubaliana na wewe unaposemna tatizo ni viongozi wetu lakini mbali na wao kuna hawa vishawishi.. serikali yetu ni sawa na Malaya mtaani ambaye sidhani kama unaweza kumlaumu kwa kuuza mwili wake wakati kuna wanunuzi wa ngono ambao wameacha wake zao nyumbani...
Hawa wawekezaji kina Bush wanachokuja fanya ni kutumaliza tu, wametufanya mMalaya hawaji kwa nia ya kufunga ndoa ila kututumia hadi siku mwili utakapo choka..besides hivi kweli tunamhitaji Bush kuja fungua biashara ambayo hawezi kuifungua Marekani?..Foundation my....hawa wezi tu.
 
Tusipokuwa makini kuna hatari kuwa hata Ikulu itauzwa. Kama ni kweli it is a shame. Yaani niwatese wananchi walionipigia kura kwa kishindo cha sunami kwa ajili ya kujikomba kwa foreigner???? Tungekuwa na upendo wa kweli among ourselves (Tanzanians) leo usingekuta wahindi wanatuona choo ndani ya nchi yetu, mafisadi kila kona na mengine ya kunuka kama hayo. Sorry to say hatuna solidarity. Je mimi au wewe naweza kwenda kufanya kazi au kuwekeza India then nikapewa privilidges kama wapewavyo wahindi hapa??? Naweza kupata ardhi India??? Naweza kupata ardhi hapo Kenya tu??? Yaani watanzania tuamke. In 20 years to come we will have settlers Makaburu na Bepari wengi sana, watanzania tukakuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu!!!

Mungu ailaze pema peponi roho ya mpiganaji Julius Kambarage Nyerere aliyetuhangaikia
tukapata uhuru na amani ambavyo tunaviuza kwa sasa, aliyetuwekea rasilimali ambazo tumeshamaliza kuziuza na tuko mbioni kuuza rasilimali ya nishati ya mafuta!!!! Tungekuwa wote tuna lugha moja i.e lugha za asili basi ningeandika neno la kilugha ambalo kwa kishwahili halina tafsiri nzuri kama ilivyo kwa kilugha ili wote tupate kuamka katika usingizi wa pono tuliolala.
 
Mtanzania,
Mkuu wangu, nitakubaliana na wewe tu ikiwa wewe una present upande wa pili wa shilingi na sio kwamba unaamini kabisa kuwa kuna jema linalotegemewa toka kwa Bush..
Kwenye swala la Dowans ungetupeleka kubaya sasa kama yungekusikia wewe, sasa umeanza na hili la Bush!..Inaonyesha wazi unashindwa kutazama nyuma ya pazia..

Mkuu sio kweli kabisa rais mstaafu wa Marekani huwa na walinzi mkubwa kama unavyodai..Carter alikuja hapa kuuza kitabu chake na watu tulikwenda kupata signature yake, pembeni mwake kulikuwa na mtu mmoja tu tena hatukufanyiwa search kabla hujamsogelea jambo ambalo lisingewezekana kabisa kama angekuwa rais bado..
Ningeweza kabisa kumchapa kibao kama ningekuwa mkereketwa...haya umeambiwa hata Clinton kisha tinga Bongo bila safari yake kuwa kichwa cha taarifa..Hii ndiyo tofauti kati yetu na hawa jamaa...na nina hakika huwezi kunambia carter mara ya mwisho ametinga lini Bongo iwe kupanda mlima au kuendelea na shughuli zake za biashara..
Kweli kabisa nakubaliana na wewe unaposemna tatizo ni viongozi wetu lakini mbali na wao kuna hawa vishawishi.. serikali yetu ni sawa na Malaya mtaani ambaye sidhani kama unaweza kumlaumu kwa kuuza mwili wake wakati kuna wanunuzi wa ngono ambao wameacha wake zao nyumbani...
Hawa wawekezaji kina Bush wanachokuja fanya ni kutumaliza tu, wametufanya mMalaya hawaji kwa nia ya kufunga ndoa ila kututumia hadi siku mwili utakapo choka..besides hivi kweli tunamhitaji Bush kuja fungua biashara ambayo hawezi kuifungua Marekani?..Foundation my....hawa wezi tu.

Mkuu Mkandara,

Mimi msimamo wangu kuhusu DOWANS haujabadilika, kama ningeona ni value for money ningenunua na kuwajabika kama kungelikuwa na matatizo. Huo ndio uongozi, si huu wa kufuata upepo. Do nothing mentality haitatusaidia Tanzania. Kama katika kuchunguza ningegundua madudu mengine hapo nisingenunua. Ila siwezi kufanya jambo ninaloona litawafaa wengi kwa kigezo cha mbaya wangu atafaidika.

Wewe mlizi wa Carter unafikiri ni yule tu ambaye alikuwa amekaa pembeni kwake? Hapo kulikuwa na wengine wananua vitabu kama wewe, wengine ni kutoka polisi wenu hapo hapo. Niliposema wengi haina maana kama wale wanaomlinda Obama, ina maana kuna watu wengi inabidi wajue kwamba mtu kama huyo anakuja ili watoe ulinzi.

Hilo la Clinton sio sawa kabisa, maana safari zote za Clinton TZ zilikuwa zinajulikana. Labda anayesema hivyo hakufuatilia habari za TZ kwa wiki husika. Kuna siku moja hapa Clinton alitoka kwenye mkutano wa Labour, kumbe vyakula kule hakupenda na wakati wanaondoka akaomba wapitie McDonald. Watu tulidhani waliamua tu na kuchepuka, baadaye kuja kumhoji mwenye McDonald, kumbe alipigiwa simu na kuambiwa ajiandae na jamaa wasiovaa magwanda wakawahi pale kama na wenyewe ni wateja. Rais mstaafu wa USA ana ulinzi mkubwa tu maana kukitokea kupigwa risasi itakuwa balaa kwa nchi mwenyeji na kwa USA wenyewe.

Mwekezaji yeyote ni mwizi bila kujali ni wa ndani au nje. Ndio maana hata kwenye biblia imeandikwa ni ngumu kwa tajiri kwenda mbinguni. Uwizi wa mwekezaji yeyote unapunguzwa na sheria za nchi. Wenye nchi mkilala mnaibiwa hasa.

Nafikiri mawazo yako na yangu viko 180 degrees. Tukubali kutokukubaliana.
 
hii ni hofu ya waislam wenye hofu na kutokujiamini, acheni soga za kiswahili na kitoto. kama bush anakuja kuwekeza, mimi napendekeza angepewa eneo kubwa zaidi. ni sawa tu na kama wakija waarabu ambao sio marafiki wetu sisi baadhi ya wakristo, lakini tunawakubali tu kuja kuwekeza hapa. bush akija kuwekeza ni kosa gani?

ninyi ndio watu ambao akili zenu ni fupi sana. the kind of people like watu hawa wenye uoga, ni sawa na wale wenye akili ndogo ya kuweza kufundishwa hata kujilipua wafe(wakati waalimu wanaowafundisha wanaendelea kudunda na wanaogopa kifo). hivyo mnaweza kudanganywa chochote hata leo hii mkakubali kwasababu akili zenu fupi. nendeni shule mkasome kuondoa ujinga. hapo ndo mtakuwa na uwezo kupambanua ukweli na uongo.
 
Pointi yako ssielewi hapa.
Itakuwa ngumu kuielewa kama umeshindwa kuelewa na kujibu mada halisi#
ciao

Eeer..what exactly are you talking about? Hivi tupo ukarasa mmoja kweli au ndo wikiendi imeanza?

Mkuu hapa mjini, kama hujui ni vyema ukauliza njia, vinginevyo unaweza ukajikuta unaibukia kwenye choo cha kike, halafu wamama wakakupigia kelele za mwizi, halafu ukaishia kuzungushiwa tairi..

Elewa unacho-reply..
 
mi nashangaa jambo, moja. kwani kuna ulazima gani wa yeye kununua eneo hilo ambalo watu tayari wanaishi, tz si kubwa tu, kwanini wasingempa maeneo mengine, kuliko kuhamisha watu then kuwapeleka mbali zaidi. hakuna mji unaojengwa, mji huwa unakuwa wenyewe taratibu. hizi haraka za serikali tu, kutaka nchi iwe ki ulaya ulaya wakati sisi ni wa bongobongo. Hatukatai bush kupewa eneo. ila kwani hakuna maeneo mengine ambayo hakuna wakazi apewe badala ya kuhamisha watu?????
 
Ndugu wana Jamii,
Kuna habari huku majuu zinasambaa sana kwamba Bush (Kichaka) amenunua sehemu kubwa sana Kigambioni na anataka kuwekesha (uwekezaji) sijui kitu gani..Ndio maana ziara yake Bongo ilichukua muda mrefu sana na inasemekana kisha kuja tena Bongo baada ya kukabidhi madaraka kwa Obama ktk kumalizia malizia taratibu za umiliki..
Je, maneno haya kweli?!? au ndio yale ya kambi ya kijeshi ya Marekani baada ya Kenya kuwatolea nje!
Kale ka - nzi kako wapi?..

Ule mji wa Kigamboni satellite city sijui smart city uliishia wapi?
 
Back
Top Bottom