Je ni kwanini mheshimiwa rais haandiki jina wala saini anapotoa salamu binafsi?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Wakulu heshima mbele.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia salamu za raisi wetu mheshimiwa Jakaya Kikwete ambazo ni ama za kupongeza, au kutoa rambirambi au kutoa pole.

Mara nyingi mheshimiwa rais wetu amekuwa anaitumia kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kuandika na kutoa salamu hizo kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Kwahio kinachotokea hapo ni uchapaji wa barua hizo na mwisho inasemwa alieandika ni kurugenzi ya mawasiliano.

Mifano ipo mingi kwa kuangalia salamu nyingi tu ambazo mheshimiwa rais ametuma katika siku za hivi karibuni na akawaachia watu wengine wamalizie.

Je ni kwa sababu zipi mheshimiwa rais amekuwa hatii saini mwisho wa salamu zake, je anahofia nini au haoni kwamba jambo hilo sio sahihi kiitifaki?

Naomba kuwasilisha hoja.
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ipo kwaajili hiyo, na wanaandika alichoagiza...Mkuu, unataka kuwanyang'anya jamaa ulaji nini?
 
Back
Top Bottom