Je ni kutimia kwa usemi '' wamevaa ngozi yz kondoo kumbe ni mbwa mwitu?!''

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
252
Nimekua nikifatilia mambo yanayo endelea nchini ikiwemo kitendo cha sintofahamu katikati ya jamii yetu kwanza kabisa ni vuguvugu la kisiasa lililopo hapa nchini kwa sasa!
Kumekuwepo kesi nyingi zakupinga matokeo ya wabunge n.k pia kumekuwepo swala la makundi katika vyama hasa hasa ccm. Mathani kuna makundi ambayo yamesha anza kampeni kwa ajili ya 2015
chukulia mafano mh ''el'' huyu jaama imefikia mahali sasa ameanza kuwa mchungaji sijui niseme baba parokoo!!! Yeye ni kuhudhuria matamasha ya kidini,harambee za kidini,na matukio mbali mbali ya kidini ambayo ni aghalabu kusiwepo umati wa watu. Katika sehemu hizi amekuwa akitoa michango mingi na kupiga vijembe na kujisafisha pia. Si nia yangu kumhukumu bali nataka watazania tujiulize nyuma ya pazia kunani? Je ni kweli kwamba anawapenda watanzania sanaa? Je pesa zote za kuchangia tanzania yote anapata wapi? Je watu wakama hawa nyerere hakutuonya? Je sisi watanzania ni vipofu hivyoo? '' alisema tuogope watu wanaokimbilia ikulu....tena akasema tuwaogope kama ukoma''' i maneno ya mwalimu. Lakini tukija upande wa dini nayo inatukataza...nanukuu '''' tazameni naondoka kwenda kwa baba lakini nawaonya mbele.....tazameni watakuja watu wamevaa mavazi ya kondoo kumbe kwa ndani ni mbwa mwitu wakaliiiiii''' ''jihadharini nao'''
je ndungu zangu tuendelee kuziba masikio tuuu

tafakari chukua hatua
 
Back
Top Bottom