Je ni kutahiriwa au kukeketwa?

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Katika jukwaa la JF Doctor kuna thread inayoendelea kujadiliwa yanye kichwa cha habari ''Swala la kutahiriwa kwa wanawake mnasemaje?''. Ningependa wadau wa lugha tujajiliani juu ya lipi neno sahihi, kati ya kutahiriwa na kukeketwa, linaloeleza kitendo cha mwanamke kukatwa kinembe chake. Uwanja ni wenu
 
Inategemea na muktadha. Nionavyo mimi, neno 'kukeketa' linatumika zaidi katika muktadha unaoashiria kupinga (au kutokubaliana na kitendo chenyewe)- ni tafsiri ya 'female genital mutilation(FGM)' ambayo kwa tafsiri ya neno kwa neno ingekuwa 'kuharibu sehemu za siri za mwanamke'. Nimeona pia neno 'male genital mutilation(MGM)' limeanza kutumika kwa wale wanaopinga tohara kwa wanaume!

Lakini katika muktadha wa kukubali kitendo chenyewe au usioegemea upande wowote, watu wengi hutumia neno 'kutahiri' (- kufanyia tohara). Kwa baadhi ya mila/tamaduni, tohara ni sehemu tu katika mchakato mzima wa jando au unyago.

Neno kutahiri linaweza kutumika kwa jinsia zote mbili kama lilivyo neno la kiingereza 'circumcision'.
 
Back
Top Bottom