Je, ni Kupaza aliyemuua Mwivano? Upande wa pili wa Shilingi

Uswahilini tuna msemo usemao "Mkamatwa na Ngozi ndiye mwizi".
Hapa kwa ushahidi wa kimazingira unamwonesha moja kwa moja Kupaza kuwa ndie mhusika, lakini kuna kitu/vitu vyengine hapa vinanuka ambavyo vinaweza kumfanya Kupaza asiwe mhusika, lakini kutoka na haya mazingira yalivyosukwa, iwe ni kweli au la...Kupaza kanaswa.
Mnakumbuka kisa cha Ijumaa iliyopita ambapo Asha Mkwizu alimuua Mwanahamisi Happiness?
Tukio kama hili la Mkwizu vs Happiness ndilo linalozoeleka kutokea, na sio baina ya wananwake tu bali hata baina ya wanaume, kuwa yule "anayekuibia mpenzi wako" ndie mkosa na ndiye anayestahiki adhabu, na kumwacha upande mwizi wa kweli. Katika kesi ya Mkwizi na Happiness, mkosa alikuwa Dr Hauli lakini Mkwizu akamuua Happiness? Je hakuna uwezekano katika kesi hii kuwa Bi Shari alimwua Mwivano kama kulipiza kisasi kwa
a) Kunyang'anywa mume. b) Uchungu wa fadhila za punda za Kupaza na Mwivano.

Hakuna uwezekano pia mtu Mzungu aliyekuweko mtoni alikuwa msaidizi wa Bi Shari? Polisi wakati wowote walilifikiria hili? Tusisahau pia kuwa kuna mamia ya maelfu ya kesi Marekani ambapo mara nyingi "mtu mweusi ndiye "mbaya/adui" katika filamu?

Nilikuwa nasubiri mtu anisaidie kudadavua kama ulivyofanya..............Ahsante sana, kwani sikutaka kuwa na kiherehere cha kusherehesha mkasa huu mara tu baada ya kumaliza kuufasiri, nilitaka wasomaji wadadavue na kuweka mawazo yao humu kwa uhuru kabisa...............

Hebu tujiulize wote...........

1. Mama Shari Goss alikuja nchini kama mmishenari na kukutana na Peter Kupaza

2. Waliamua kuoana na kwenda kuishi wote Ughaibuni (Ikumbukwe kwamba kwa Mbongo hiyo ni bahati sana kupata mzungu na tiketi ya kuishi ughaibuni, lakini kwa Mzungu pia ni bahati maana sarakasi za mapenzi ya wao kwa wao zimewashinda na kupata Mbongo ni faraja na tulizo la moyo......Kumbukeni tunayo sifa ya ukarimu kwa wenzetu)

3. Kupaza kamwita dada yake binamu kwenda kuungana naye huko Majuu ili kujifunza kiingereza kabla ya kujiunga na chuo cha uuguzi

4. kashfa ya ujauzito wa kaka binamu unasambatisha ndoa ya Kupaza na mkewe Shari Goss......(Kumbukeni huyu Bwana alipata bahati hiyo ya kuishi na kufanya kazi ughaibuni kwa sababu ya ndoa yake na Shari Goss)

5. Kupaza akahamia kwenye eneo lingine na kuishi peke yake huku dada yake Mwivano akiishi Hostel na marafiki zake
aliokuwa akisoma nao.................

6. Si kwamba Kupaza aliona ni busara kumweka dada yake mbali na yeye ili kuepuka kuchomewa utambi kwa Polisi na Shari Goss baada ya Viza ya dada yake ya kuishi nchini humo kuisha muda wake?

7. Je Shari Goss anaweza kuishi kwa amani kweli, hasa baada ya ndoa yake kusambaratishwa na dada binamu wa mumewe?

8.Kwa nini Shari Goss awe wa Kwanza kuitambua sura ya Mwivano na kuripoti Polisi

9. Je ni visa vingapi vinavyofanana na hiki vinavyowapata Waafrika kutoka Afrika wanapotengana na wake zao au waume zao Wazungu?

10. Kisa cha mzungu kule mtoni nacho kinaacha maswali bila majibu.....................

Nimewaza kwa sauti tu..................................
 
[/QUOTE]

8.Kwa nini Shari Goss awe wa Kwanza kuitambua sura ya Mwivano na kuripoti Polisi
[/QUOTE]

Hii ndio hata mimi imenishangaza yaani huyo Mama utafikiri alikuwa amekaa sehemu anasubiri hilo tukio!!
Ila kuna nukta nyingine ya kuunganisha...
Ipo hivi, yule mzungu kule mtoni alikuwa anafuatilia hatima ya ile mifuko siku itakapokutwa na raia wa kawaida....
Hivyo siku alipoona kweli katokea mtu kaiona akapeleka taarifa kwa Shari, naye Shari akawa-standby kusubiri move ya polisi ili atoe ushirikiano wa kutosha kumshikisha adabu X-hubby wake....

Hapo vipi Mtambuzi na wanabodi.. nukta hizo haziunganishiki??
 
Nimekisoma Hiki kisa pamoja na hukumu yake
Labda niseme kuwa mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Criminal Investigation channel na nimeona kesi nyingi zenye kusumbua ,

Lakini ukiangalia kiundani hii kesi huyo Mama wa kizungu (Goss) ameinfluence kwa kiasi kikubwa Upelelezi na hata hukumu ya hiyo kesi,
Huo ushahidi wa mbwa hauna mshiko kabisa na wala huo ushahidi wa hiyo mifuko pia hauna mshiko,

1) Kwa asilimia kubwa mimi ninaamini kuwa huyo mama wa kizungu (Goss) kacheza mchezo mzima na nadhani hata Kupaza analijua ama alilishuhudia hilo tukio

b) kesi ingeanzia kwa yule mama aliyeona maiti na yule Mzungu aliyekimbia

3) ni ajabu kabisa kwa polisi kuchukua ushahidi wa huyo mama kuhusu hiyo mifuko ya Rambo, huo sio ushahidi kabisa wa kumfunga mtu, kama huyo mama Goss analijua hilo alishindwa vipi kumset Peter kUPAZA

4) Mahakama inakubali vipi ushahidi wa kuambiwa kuwa jamaa ni mtaalamu wa kukata Nyama, mahakama ilijilizishaje na hilo?, huo pia sio ushahidi wa kumtia mtu hatiani

5) INAWEZEKANA KABISA KUWA PETER KUPAZA NDIO MUUAJI, LAKINI KULIKUWA HAKUNA USHAHIDI UNAOMUWEKA HATIANI
 
Nimekisoma Hiki kisa pamoja na hukumu yake
Labda niseme kuwa mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Criminal Investigation channel na nimeona kesi nyingi zenye kusumbua ,"

salute mkuu, lakini swali mimi ninalojiuliza ni kwanini kupaza hakurepoti kupotelewa na ndugu muda wote huo?

- kumbuka mwivano ndio ndugu aliemuweka kama next of kin which means walikuwa wanajuana na wanafahamiana

- kwa nini alidanganya kuhusu kuongea na wazazi wa mwivano? ina maana wazazi nao waliconspire na huyu mama wa kizungu???

- for me i think kupaza ana kesi ya kujibu hapa.
 
Huyu ni Dr. Madeleke (Doctor wa vichaa) na Marehemu mkewe alikua anaitwa Sheila Sagara. Watoto wa huyu mama sasa hivi wanaishi Guyana kwa mjomba wao, Edward nadhani anaitwa, ambaye ni kaka wa marehemu Sheila anafanya kazi katika serikali ya Guyana. Aliamua kuchukua watoto wa dada yake maana shemeji alihukumiwa kufungwa maisha nadhani japo aligunduliwa akili kuvurugika. sikumbuki vizuri story pia. Ila ukituwekea itakua vizuri sana.

Nimejitahidi kuitafuta hiyo kesi Mtandaoni lakini sikupata taarifa zilizoshiba au niseme zenye mashiko...............kama unazo details zaidi nimegee, na mimi nitaiweka hapa kwa kadiri muda utakavyoruhusu..............
 
Uswahilini tuna msemo usemao "Mkamatwa na Ngozi ndiye mwizi".
Je hakuna uwezekano katika kesi hii kuwa Bi Shari alimwua Mwivano kama kulipiza kisasi kwa
a) Kunyang'anywa mume. b) Uchungu wa fadhila za punda za Kupaza na Mwivano?

Hakuna uwezekano pia mtu Mzungu aliyekuweko mtoni alikuwa msaidizi wa Bi Shari? Polisi wakati wowote walilifikiria hili? Tusisahau pia kuwa kuna mamia ya maelfu ya kesi Marekani ambapo mara nyingi "mtu mweusi ndiye "mbaya/adui" katika filamu.
Naamini Peter Kupaza alimuua dada yake. Kwa nini?

  1. Alidanganya kuwa Mwivano amesafiri kurudi Tanzania
  2. Alidaganya kuwa alisafiri na Shadrack Msengi (Ambaye yeye Peter hana details zozote kuhusu Shadrack)
  3. Alidanganya kuwa Mwivano alishafika Tanzania na hizo taarifa ameambiwa na wazazi wake
  4. Hakutoa taarifa polisi kuhusiana na kupotea kwa Mwivano
  5. Hata picha ziliposambazwa hakujitokeza kuwapa polisi ushirikiano wa kumtambua dada yake
  6. Hata polisi walipofika kwakwe na kumwonesha picha alikana kuwa zile picha hazifanani na sura ya dada yake
  7. MENGINE TU........................ Naamini anahusika.
 
Heko Mtambuzi kwa kutuletea visa vya kuhuzunisha na kufikirisha. OMBI: Hebu tutafutie kisa cha mtanzania mwanaume aliyekuwa akiishi Botswana na mkewe na baadaye mapenzi yao yakavurugika na kuishia kwa mume huyu kumwuua mkewe. Mimi nilikisikia juujuu sana ila nina uhakika unakifahamu hiki kisa.

Au unamaanisha Dokta Mtanzania aliyekuwa Swaziland akamuua mkewe kwa sababu ya mpenzi wa pembeni?
 
umenirudisha mbali sana mkuu, nakumbuka hi kesi kwenye vyombo vya habari hapa nyumbani, asante, nimekukubali
 
Mi naamin shari goss na peter wanajua kila kitu kilichotokea,huyu mama anahusika kabisa na yule mzungu kule mtoni alikuwa standby kujua hatima ya ule mfuko,lakin naye peter maelezo yake yanaonesha anahusika kwa asilimia zote kama shari..kuna siri wanaijua hawa wawili yaani shari na peter.
Thanks kwa thread nzur ila nakuomba usithubutu kusummarize haitakuwa vzuri
 
Kupaza kamuua mwivano,nawaamini sana wazungu ktk investigation.
Dah hii story inanisikitisha saaana maana nawajua sana wahuska wengi ukianza na mwivano mwenyewe na hao mashahid faith mmanywa na shadrack msengi,all are my school mates at Lutheran Junior Seminary, RIP dada Mwivano!
 
Nimekisoma Hiki kisa pamoja na hukumu yake
Labda niseme kuwa mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Criminal Investigation channel na nimeona kesi nyingi zenye kusumbua ,"

salute mkuu, lakini swali mimi ninalojiuliza ni kwanini kupaza hakurepoti kupotelewa na ndugu muda wote huo?

- kumbuka mwivano ndio ndugu aliemuweka kama next of kin which means walikuwa wanajuana na wanafahamiana

- kwa nini alidanganya kuhusu kuongea na wazazi wa mwivano? ina maana wazazi nao waliconspire na huyu mama wa kizungu???

- for me i think kupaza ana kesi ya kujibu hapa.

Kweli kuna walakini wa maelezo ya Peter Kupaza kuhusu wapi alipo dadake na uongo mwingi tu aliotoa, lakini ukiangalia kwenye tukio lenyewe la uuaji, sioni ushahidi wa moja kwa moja unaomuunganisha Peter, hapo upo ushahidi wa Kimazingira tu na wakuhisia tu ambao kwa kiasi kikubwa umetengenezwa na Goss
 
Waswahili wanasema uwongo huwa unazaa uwongo mwingine..................
-Kupaza alilazimika kudanganya kuhusu alipo dada yake kwa sababu Viza ya dada yake ya kuishi nchini Marekani iliisha muda wake, kwa kuuliziwa na Polisi, kulikuwa na maana kwamba ameshachomewa na Shari Goss na sasa inabidi am-protect, na kosa hilo ndilo lililomgharimu ikabidi aendelee kudanganya kumbe ndio anajitia kitanzi........
-Shari Goss alikuwa anajua mchezo mzima, ile kuwahifadhi wazazi wa Mwivano kwa kipindi chote wakati kesi inaunguruma, ni katika ku-cover up alichokifanya, lakini wote wawili wanajua what happened.

Bado kuna maswali mengi yanahitaji majibu ili kuthibitisha kweli Kupaza alimuua dada yake................
 
Nilikuwa nasubiri mtu anisaidie kudadavua kama ulivyofanya..............Ahsante sana, kwani sikutaka kuwa na kiherehere cha kusherehesha mkasa huu mara tu baada ya kumaliza kuufasiri, nilitaka wasomaji wadadavue na kuweka mawazo yao humu kwa uhuru kabisa...............

Hebu tujiulize wote...........

1. Mama Shari Goss alikuja nchini kama mmishenari na kukutana na Peter Kupaza

2. Waliamua kuoana na kwenda kuishi wote Ughaibuni (Ikumbukwe kwamba kwa Mbongo hiyo ni bahati sana kupata mzungu na tiketi ya kuishi ughaibuni, lakini kwa Mzungu pia ni bahati maana sarakasi za mapenzi ya wao kwa wao zimewashinda na kupata Mbongo ni faraja na tulizo la moyo......Kumbukeni tunayo sifa ya ukarimu kwa wenzetu)

3. Kupaza kamwita dada yake binamu kwenda kuungana naye huko Majuu ili kujifunza kiingereza kabla ya kujiunga na chuo cha uuguzi

4. kashfa ya ujauzito wa kaka binamu unasambatisha ndoa ya Kupaza na mkewe Shari Goss......(Kumbukeni huyu Bwana alipata bahati hiyo ya kuishi na kufanya kazi ughaibuni kwa sababu ya ndoa yake na Shari Goss)

5. Kupaza akahamia kwenye eneo lingine na kuishi peke yake huku dada yake Mwivano akiishi Hostel na marafiki zake
aliokuwa akisoma nao.................

6. Si kwamba Kupaza aliona ni busara kumweka dada yake mbali na yeye ili kuepuka kuchomewa utambi kwa Polisi na Shari Goss baada ya Viza ya dada yake ya kuishi nchini humo kuisha muda wake?

7. Je Shari Goss anaweza kuishi kwa amani kweli, hasa baada ya ndoa yake kusambaratishwa na dada binamu wa mumewe?

8.Kwa nini Shari Goss awe wa Kwanza kuitambua sura ya Mwivano na kuripoti Polisi

9. Je ni visa vingapi vinavyofanana na hiki vinavyowapata Waafrika kutoka Afrika wanapotengana na wake zao au waume zao Wazungu?

10. Kisa cha mzungu kule mtoni nacho kinaacha maswali bila majibu.....................

Nimewaza kwa sauti tu..................................

Kwanza Mtambuzi nashukuru kwa kutukumbusha stori hii..
Iliuza sana magazeti ya Tanzania kipindi kile...

Sasa kwenye kesi hiyo loose ends zipo lakini si nyingi,ndiyo maana hata rufaa zake zilitupiliwa mbali mara mbili..

1.Kwamba,vipande vya mwili vilifikaje mtoni?
2.Kwamba,wanafunzi wenzake/marafiki wa Mwivano hawakuhusishwa katika eneo hata moja la kesi hiyo..
3.Kushindwa kujitokeza,ama kupatikana yule jamaa wa kizungu pale mtoni..kwani kwa kuelezwa aina na rangi ya gari,walitakiwa wamtafute na kufuatilia nyendo za waliotumia magari ya aina,na rangi iliyotajwa..
Ila,

-Kwa no 7 yako... Ukumbuke dada binamu alibakwa,hata kupata ujauzito,na kupelekea ushauri wa kufanya "abortion"..

-Kwa no 8,kumbuka wanaishi kwenye ki-county hapo Wisconsin.. Na kwa miaka hiyo naweza kusuggest mazingira ya majengo machache,umbali wa nyumba moja hadi nyingine, hivyo mtu kutambua majirani kiukamilifu ni labda kuwa na mazoea ya kutembeleana,au kuonana mara kwa mara.

-No 9,visa kama hivi ni hadi viwe vimeripotiwa,si katika kesi tu,hata ndugu na jamaa. Kidogo sana labda Urusi..mwanamke wa Kirusi usimuahidi kumuoa na ukamuacha.. Utafia tu kwenu kwa ugonjwa usiojulikana!

-Kwa no 10,haikuelezwa kama wataalamu wa "forencic" waliweza kutumika kujua Mwivano aliuwawa lini..
Kwa Peter Kupaza kama muuaji,asingependa mabaki ya Mwivano yaonekane.. Na kwa Shari Goss(mtalaka wa Peter),labda alimplant mtu aone mabaki,na kuripoti Polisi,lakini hatimaye situation ikawa nyepesi kwake kwa kutokea mwanamama aliyeenda picnic na wanawe..hivyo akamshauri akatoe taarifa polisi,na yeye kutokomea..
 
Niliwahi kuisikia hii kesi, lakini haikuwa detailed namna hii. Asante Mtambuzi!

Mwaka 2000 ulikuwa wapi mkuu... Gazeti lililoifuatilia kwa sana nadhani ilikuwa Nipashe.. Tena ilikuwa front page.. Na kulikuwa na mwendelezo wa karibu kila siku kulingana na kesi ilivyoenda..

Waliuza sana gazeti kipindi kile..
 
Waswahili wanasema uwongo huwa unazaa uwongo mwingine..................
-Kupaza alilazimika kudanganya kuhusu alipo dada yake kwa sababu Viza ya dada yake ya kuishi nchini Marekani iliisha muda wake, kwa kuuliziwa na Polisi, kulikuwa na maana kwamba ameshachomewa na Shari Goss na sasa inabidi am-protect, na kosa hilo ndilo lililomgharimu ikabidi aendelee kudanganya kumbe ndio anajitia kitanzi........
-Shari Goss alikuwa anajua mchezo mzima, ile kuwahifadhi wazazi wa Mwivano kwa kipindi chote wakati kesi inaunguruma, ni katika ku-cover up alichokifanya, lakini wote wawili wanajua what happened.

Bado kuna maswali mengi yanahitaji majibu ili kuthibitisha kweli Kupaza alimuua dada yake................

Hata kama Shari Goss alijua Peter angefanya mauaji,lakini hakupenda yatokee..

Hata wakati yanatekelezwa,yeye tayari alishatengana na mumewe huyo.. Sasa mnahusisha vipi kuwa walishirikiana?

Au mnahisi alitekeleza mauaji hayo ili mapenzi ya Shari yarudi na aamue kumrudia mumewe Peter?

Siipati picha yenu mnayonipa..
 
mpendwa,

kweli wewe ni mtambuzi! nakupa heko kwa uandishi mzuri, tangu kisa cha Asha mkwizu hauli, siachi kusoma mada zako.

mimi sio mpelelzi ila inaonekana kupaza ndiye alioyemuuwa mwivano na sababu ya kumuua inatokana na tendo la kumbaka hasa ikizingatiwa kuwa ni dada yake na kama habari ile ilikuwa haijajulikana tanzania, basi alimuua ili kuondoa kabisa uwezekano wa kujulikana aibu hiyo ya kumbaka dada yake! pia nahisi alipata ujauzito mwingine na kupaza alijaribu kumshawishi autoe naye akakataa na ndipo alipoona kuwa akishajulikana ana mtoto, siri yao ya kumbaka itajulikana na jamaa zake tanzania.

pia inaonekana siri yao hiyo aliijua pia mmanywa kwa sababu wanazozijua wao na huyo mmanywa inaonekana alikuwa mwandani wake kwa mambo mengi tu mengine!

nionavyo mimi, hata kumfanyia mipango ya kumpeleka marekani ililenga kumtimizia matamanio yake kwa dada yake alioyokuwa nayo siku nyingi hata kabla hajahamia marekani.

inasikitisha sana jamani.

RIP mwivano

mbarikiwe wapendwa na weekend njema,

Glory to God!

Nahisi Peter alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Faith,wakiwa Tanzania.. Ama kama si hivyo,alikuwa anamtaka Faith walipokutana ama walipoanza kuwasiliana wakiwa Marekani..

Mimi sijawahi kutembea na mwanadada wa Kizungu hata siku moja.. Ila nimeona Waafrika wengi,waliowahi kuoa Wazungu(mzazi wangu ni mmojawapo),angalieni Madaktari wa zamani,na wasomi wengi wa zamani..
Lazima,walikuja ,walau kuzaa,na ama kuoa kabisa wanawake wa Kiafrika baadaye..

Sijui ni kwa nini kwa kweli!
 
Back
Top Bottom