Josephine
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 786
- 812
Kwa hakika nimeshtuka sana,kuona walinzi wa jadi kuwa ni watu ambao wanajibainisha kama wana CCM.
Wana JF,
Wengi wetu tunapenda mabadiliko ya sera ili kuirudisha Tanganyika yetu katika mfumo ambao ilikuwa ni ndoto ya Mwl. Nyerere na waasisi wa enzi hizo.
Lakini kwa yale niliyosikia toka kwa mwenyekiti,ni kweli Nyenzo wanazo,rasilimali watu wanayo,na hivyo wanajipanga kuendeleza ukoloni mweusi.
napozungumzia rasilimali watu,sizungumzi wananchi kama wananchi,bali ninaongelea Jeshi la polisi,maafisa wa serikali,maafisa usalama,Jeshi la wananchi,walinzi wa jadi na wafanyabihashara wakubwa na wadogo.
Kundi hili la watu limekuwa ni tishio,kwani linatumia nguvu,ubabe,mabavu na pesa katikakutekeleza adhima zao.Niukweli uliodhahiri kwamba kama sisi wananchi ambao tunapenda mabadiliko kwa manufaa ya kizazi chetu,ni lazima tujipange kwa hoja nzito na si kuendekeza ushabiki katika mijadala mingi.kwani mabishano na kiburi havijengi bali hubomoa na kuleta kushindwa.
kwa maana hiyo ni vema tukubali kubadili kufikiri kwetu na kutenda kwetu kwa pamoja kama kundi linalotaka mabadiliko na si kutegemea nguvu ya vyama pekee,Wote tunatambua chama pia kinapata ushindi kupitia sisi wananchi na wakereketwa.
Tuamke ndugu zangu kusambaza propaganda kwa ndugu zetu,marafiki na wote tunaowajua ambao leo bado fikira na mawazo yao yako kifungoni.
Kazi hii tuifanye mimi na wewe ili mabadiliko yatokane na sisi wenyewe.