Je, ni halali kwa daktari kuanzisha mahusiano na mgonjwa wake?

Kwa mujibu wa maadili ya jobs(kazi) haitakiwi na sio nidhamu za kazi na jengne nakubali kwamba mt2 yeyote hula kazini kwake lakini nat2mai sio kula hii iliyokusudiwa ktk kaziiiiiiiiii!!! Doctor upoooo!! Fikiri kwanza !!!

Mi nimeona rafiki yangu alienda kuchek malaria dispensari moja akakutana na nesi mmoja, akamwomba namba ya simu na kilichofuata alimlamba na ukawa ndo mchezo. Kw hyo hata mgonjwa anaweza kumfanyizia daktari wake
 
Nadhani si mbaya kwa daktari kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mgonjwa kwan ktk mapenz haijalishi ni wap na nan mapenzi hujengwa. Mapenzi yapo popote na kwa watu wowote mbaya hapa ni pale daktari atakapo lazimisha mapenz kwa mgonjwa wake ama pale daktari anapogeuza ofisi yake kama guest house.
Wakiendana poa tu ngoma inogile
 
Mi sioni tatizo! Kibaya probably kama Doctor atam'baka mgonjwa.
Otherwise mgonjwa anai'submit mwenyewe na hakuna mazingira ya Rushwangono sioni tatizo.
 
Polisi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na aliyemkamata au mlalamikaji ni sahihi? Vipi kuhusu hakimu na mshtakiwa? Nimewahi kusikia toka kwa rafiki yangu hakimu wa kike ambaye baada ya kumkuta mshtakiwa hana hatia alijikuta anawindwa kama aliyepotea njia. Dada akikuwa ameolewa na polisi. Ilibidi amuambie mumewe ndio former mshtakiwa alipoweka manyanga chini.
 
Sasa kama mie ni dr halafu nikamhudumia mgonjwa, nakamzoea na kumdondokea katika mapenzi sio mbaya ili mradi kwamba kila mtu amemkubali mwenzake hapo ndio nitakuwa nimekutana na mwenzi wangu wa maisha kama sijaoa ila kama umeshaoa sio halali(dhambi) wala sio kuchoma sindano ya ucngizi halafu u-do nae
 
Napata picha kama mtuhumiwa alikuwa na kesi ya kubaka! Duh, kazi kweli!
Nimewahi kusikia toka kwa rafiki yangu hakimu wa kike ambaye baada ya kumkuta mshtakiwa hana hatia alijikuta anawindwa kama aliyepotea njia. Dada akikuwa ameolewa na polisi. Ilibidi amuambie mumewe ndio former mshtakiwa alipoweka manyanga chini.
 
Sehemu nyingi za kazi zina code of conduct ya jinsi ya kuhandle mahusiano ya kimapenzi mahali palipo na conflict of interest. Ukiwa mgonjwa unakuwa vulnerable na emotions zako. Uko desperate kupona, whether kwa njia halali ama zisizo halali na kuna issue ya medical bills. Daktari akiruhusiwa anaweza kumtumia mgonjwa atakavyo na kuanza kumu-abuse. Inapashwa aruhusiwe kwa sharti kuwa aka-declare interest immediately na aache kumuhudumia mgonjwa. Mfano tu, kuna prof muhimbili alimfanyia operation mke wa rafiki yake (against ethics). Nurses walimuambia mgonjwa alikula kiazi a few hrs ago tena bila maji. Jamaa kwa sababu ni mke wa rafiki, thieter ina nafasi na anataka amsaidie rafikiye kufupisha adha ya kuja hosp kila saa, akaamua kuendelea na operation. Mama akafariki. Sasa dr kakosea, anachukuliwa hatua za kisheria na bodi. Umepata picha maisha yake binafsi na familia pia? Inabidi ahame hadi bar, mama ahame saluni etc. Pata picha sasa ni gf/bf wako amekupa dawa halafu ina-backfire? Ni wachache wataweza kuhandle that rationally.
My take: as soon as dr anadevelop feelings ama kuwa na uhusiano na mteja wake, anapaswa ku-declare interest na kuacha kumtibu mgonjwa immediately.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Professional ethics katika taaluma yoyote ile duniani ni muhimu sana kuheshimiwa. Kama Wataalamu hawataziheshimu professional ethics zao na kila mtu kucheza kivyake vyake basi taaluma zote zitakuwa kama uwanja wa fisi na hivyo Wataalamu kupoteza heshima (kama bado ipo) waliyonayo katika jamii.
 
Kama ndo hivyo basi madaktari wa magonjwa akina mama watawamaliza wengi
 
kTIK MAADILI ya udaktari/utabibu inakatazwa na pia ukienda katika sheria za makosa ya kujamiana haina tofauti na ubakaji. Endapo huyo mgonjwa amepona kabisa na akawa anaishi mtaani jamaa kamtafuta kumuoa itakuwa sual jingine.

jiulize je benki/afisa wa benki anaruhusiwa kuwa na mahusiano na mteja wake, wakati gani
 
Ni vizur sana kila mtu kujua kwa nini yupo duniani na nadhani kila mtu akijua ni kwa nini yupo lazima uwe na ETHICS za kazi yake 'madakitari ni watu muhimu sana' vitu kama hivyo vikiruhusiwa ni hatari sana ktk maisha ya watu na mwisho wake ni mbaya sana !
 
Kwa mujibu wa kipima joto cha jarida la Pulse watumishi wengi wa afya nchini Uingereza wanapenda kulegeza maadili makali ya kutoruhusiwa kujenga mahusiano ya kingono na wale wanaowapa huduma za kiafya.

Daktari asiye bingwa Tony Grewal wa jijini London, anasema: "Kuzuiwa kabisa kuwa na mahusiano na wagonjwa au wagonjwa wa zamani ni zuio lisilo la sahihi katika haki za kutafuta furaha kwa madaktari na wagonjwa pia."


"Tunahitaji upya, mwongozo wa kijamii wenye mamlaka ambao utakubali kuwa mabadiriko katika miaka 20 iliyopita, yanadumisha umuhimu wa kulinda makundi yasiyo na uwezo wakufanya maamuzi dhidi ya unyonyaji au kulazimishwa kutenda kitu kwa nguvu,lakini ukitoa nafasi kwa hao wenye nia ya kuanzisha mahusiano sahihi."


Mwongozo wa sasa wa baraza la kitabibu Uingereza unasema: "Ili kudumisha mipaka ya kitaaluma, na imani ya wagonjwa na jamii, ni lazima usianzishe au kuwinda kuanzisha mahusiano ya kimapenzi au hisia zisizo sahihi na mgonjwa."


Madaktari pia hawaruhusiwi kutumia nafasi ya kutembelea wagonjwa majumbani kama njia yakuonana na ndugu za wagonjwa, na wanaruhusiwa kuanzisha mahusiano na wagonjwa wao wa zamani baada ya kuonana nao kijamii. Na ikiwa mgonjwa wa zamani alikuwa asiyeweza kufanya maamuzi kwa sababu ya matatizo ya afya ya akili ya "kukosa ukomavu," hapo wanazuiwa kuanzishwa mahusiano ya aina yoyote.


Ingawa kuna sheria hizo, mwaka 2009 madaktari wengi waliondolewa katika rejesta ya kitabibu ya nchini Uingereza kwa sababu ya kuwa na mahusiano yasiyo sahihi na wagonjwa wao kuliko sababu nyingine za kitabibu, ikihusisha matukio 15 kati ya matukio 83.


Chanjo: Gazeti la The Sun na The Telegraph

It sounds like doctors are extremely powerful to the extent that many privileges goes onto their advantage. Seriously!
 
Back
Top Bottom