Je, ni halali kwa daktari kuanzisha mahusiano na mgonjwa wake?

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
feet.jpg
Kwa mujibu wa kipima joto cha jarida la Pulse watumishi wengi wa afya nchini Uingereza wanapenda kulegeza maadili makali ya kutoruhusiwa kujenga mahusiano ya kingono na wale wanaowapa huduma za kiafya.

Daktari asiye bingwa Tony Grewal wa jijini London, anasema: "Kuzuiwa kabisa kuwa na mahusiano na wagonjwa au wagonjwa wa zamani ni zuio lisilo la sahihi katika haki za kutafuta furaha kwa madaktari na wagonjwa pia."

"Tunahitaji upya, mwongozo wa kijamii wenye mamlaka ambao utakubali kuwa mabadiriko katika miaka 20 iliyopita, yanadumisha umuhimu wa kulinda makundi yasiyo na uwezo wakufanya maamuzi dhidi ya unyonyaji au kulazimishwa kutenda kitu kwa nguvu,lakini ukitoa nafasi kwa hao wenye nia ya kuanzisha mahusiano sahihi."

Mwongozo wa sasa wa baraza la kitabibu Uingereza unasema: "Ili kudumisha mipaka ya kitaaluma, na imani ya wagonjwa na jamii, ni lazima usianzishe au kuwinda kuanzisha mahusiano ya kimapenzi au hisia zisizo sahihi na mgonjwa."

Madaktari pia hawaruhusiwi kutumia nafasi ya kutembelea wagonjwa majumbani kama njia yakuonana na ndugu za wagonjwa, na wanaruhusiwa kuanzisha mahusiano na wagonjwa wao wa zamani baada ya kuonana nao kijamii. Na ikiwa mgonjwa wa zamani alikuwa asiyeweza kufanya maamuzi kwa sababu ya matatizo ya afya ya akili ya "kukosa ukomavu," hapo wanazuiwa kuanzishwa mahusiano ya aina yoyote.

Ingawa kuna sheria hizo, mwaka 2009 madaktari wengi waliondolewa katika rejesta ya kitabibu ya nchini Uingereza kwa sababu ya kuwa na mahusiano yasiyo sahihi na wagonjwa wao kuliko sababu nyingine za kitabibu, ikihusisha matukio 15 kati ya matukio 83.

Chanjo: Gazeti la The Sun na The Telegraph
 
Sio sahihi kwani daktari pia ni binadamu hivyo anashikwa na hisia km mtu wa kawaida.hivyo kumzua asimpende mtu kwa sababu ni mgonjwa wake ni kuingilia uhuru wa mapenzi.
 
Madaktari wakiruhusiwa itakuwa ni full kuenjoy ,Tanzania hiyo ikoje?
 
Nadhani si mbaya kwa daktari kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mgonjwa kwan ktk mapenz haijalishi ni wap na nan mapenzi hujengwa. Mapenzi yapo popote na kwa watu wowote mbaya hapa ni pale daktari atakapo lazimisha mapenz kwa mgonjwa wake ama pale daktari anapogeuza ofisi yake kama guest house.
 
hii sio nzuri kabisa maana watashindwa kuwaudumia vizuri kutokana na kuleteana malovee wakati wa kazi.

kwa hili mi siungi mkono kabisa..
 
Mimi naona nisahihi unataka kuniambia dereva taxi haruhusiwi kuwa na mahusiano na mteja wake?
 
Madaktari wakiruhusiwa itakuwa ni full kuenjoy ,Tanzania hiyo ikoje?
'Whatever houses I may visit, I will come for the benefit of the sick, remaining free of all intentional injustice, of all mischief and in particular of sexual relations with both female and male persons, be they free or slaves'.

Hii ni sehemu ya Hippocratic oath ambayo madaktari wote ulimwenguni wanaapa kuifuata, so Tanzania katazo ni lile lile.
 
ni minume na ethics za kazi yake kama ni muda wa kazi lakin....................kinyume na hapo ni anachezea kipande cha muhogo tu
 
kwani kambaka? mbona nyie walimu mnakula ma-dent? choir master na kwaya member! padri kwa ccta! we km domo zege umba tafu! utaishia kula kwa macho!
 
kwani kambaka? mbona nyie walimu mnakula ma-dent? choir master na kwaya member! padri kwa ccta! we km domo zege umba tafu! utaishia kula kwa macho!
<br />
<br />

mmmmhhh..hatari hii..
 
'Whatever houses I may visit, I will come for the benefit of the sick, remaining free of all intentional injustice, of all mischief and in particular of sexual relations with both female and male persons, be they free or slaves'.

Hii ni sehemu ya Hippocratic oath ambayo madaktari wote ulimwenguni wanaapa kuifuata, so Tanzania katazo ni lile lile.

Kusema kweli mapenzi hata kwa mila na desturi za kiafrika mapenzi hayaendekezwi kizembezembe tu.

Kuachia hii kitu iwe free kutaichafua kabisa hii prefession.

Ni vizuri Daktari akajiheshimu kwanza kama Dr. na baadaye kama mwanajamii wa kawaida.

Mapenzi katika maana yake haswa ni kitu kizuri sana,lakini binadamu akitawaliwa na hisia ndipo huwa shida.
 
make ur patient to bcome ur lover but dont change ur patient to be ur lover. Teh,teh!
 
Hii inaweza saidia kutupunguzia stress maanake baada ya kupiga vitabu vikubwavikubwa miaka 6, hasa kwa akina dada wanaosema doctor doctor doctor I love uuuuuu!
 
Nadhani si mbaya kwa daktari kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mgonjwa kwan ktk mapenz haijalishi ni wap na nan mapenzi hujengwa. Mapenzi yapo popote na kwa watu wowote mbaya hapa ni pale daktari atakapo lazimisha mapenz kwa mgonjwa wake ama pale daktari anapogeuza ofisi yake kama guest house.
<br />
<br />
Hivi Guest house si nyumba ya kulala wageni, awe mchungaji, sheikhe, padre, nabii, maalim, papa (pope), n.k. au?
 
ni kuvunja maadili ya kazi, haitakiwi itaonekana kama ulimforce ili umpe huduma
 
Kwani Mchungaji huruhusiwi kuoa muumini? au Mhadhiri wa chuo kuoa mwanafunzi wa chuo hairuhusiwi? kama inaruhusiwa basi ni fair.
 
hapa hakuna tatizo cha muhimu iwe baada ya mgonjwa kupona na daktari awe ana mpango wa kumuoa na siyo kumuharibia maisha vinginevyo hafai kuwa daktari.
 
Kwa mujibu wa maadili ya jobs(kazi) haitakiwi na sio nidhamu za kazi na jengne nakubali kwamba mt2 yeyote hula kazini kwake lakini nat2mai sio kula hii iliyokusudiwa ktk kaziiiiiiiiii!!! Doctor upoooo!! Fikiri kwanza !!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom