Je ni haki ya mfanyakazi kupewa likizo bila malipo

Jun 18, 2012
5
0
Wadau naomba kuuliza je ni haki ya mfanyakazi kupewa likizo bila malipo kwa muda wa miaka mitatu? Wadau mnaoijua sheria naomba msaada.
 
Kisheria mfanyakazi anastahili likizo yenye malipo isiyopungua siku 28 kila baada ya miaka miwili. Hii ina maana ukiajiriwa mwaka wa kwanza utapata likizo isiyo na malipo. Mwaka wa pili utapata yenye malipo. Mwaka wa tau aina malipo, n.k. Kwa sheria ya sasa mwajiri atakiwi kumpa pesa mwajiriwa kama mbadala wa likizo. Hivyo kama umepata likizo kwa miaka 3 bila malipo ina maana umepunjwa malipo yako ya likizo yako ya mwaka mmoja
 
Kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini no.6 ya 2004, mfanyakazi atatakiwa kwenda likizo ya mwaka (annua leave) kila baada ya miezi 12 kazini. Kumbuka likizo zote ni za malipo. Mfanyakazi atakuwa na haki ya kulipwa Leave allowance kila baada ya miaka miwili na mwajiri wake.
 
na je hii leave allowance inalipwa kwa kiasi gani?, mfano nina mke na watoto, nitalipwa masurufu pamoja na familia yangu kwenda likizo?, how much?
 
Kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini no.6 ya 2004, mfanyakazi atatakiwa kwenda likizo ya mwaka (annua leave) kila baada ya miezi 12 kazini. Kumbuka likizo zote ni za malipo. Mfanyakazi atakuwa na haki ya kulipwa Leave allowance kila baada ya miaka miwili na mwajiri wake.
Na hii leave allowance inalipwaje kimahesabu!!
 
Nahisi mdau hujaeleweka au mimi ndo sijaelewa:-

Unamaanisha likizo ya bila malipo ya miaka 3?

Au likizo ya kawaida baada ya kukaa miaka 3 kazini?
 
Kisheria mfanyakazi anastahili likizo yenye malipo isiyopungua siku 28 kila baada ya miaka miwili. Hii ina maana ukiajiriwa mwaka wa kwanza utapata likizo isiyo na malipo. Mwaka wa pili utapata yenye malipo. Mwaka wa tau aina malipo, n.k. Kwa sheria ya sasa mwajiri atakiwi kumpa pesa mwajiriwa kama mbadala wa likizo. Hivyo kama umepata likizo kwa miaka 3 bila malipo ina maana umepunjwa malipo yako ya likizo yako ya mwaka mmoja
What if ulihama kutoka taasisi ingine na ulimaliza kule likizo isokua na malipo..je mwajiri mpya anapaswa kukulipa likizo inayofuata?
 
Manyanyaso, umemechisha ID na content ya thread. Kampuni binafsi ndivyo zilivyo... Zoea au uanzishe zengwe!
 
Wadau naomba kuuliza je ni haki ya mfanyakazi kupewa likizo bila malipo kwa muda wa miaka mitatu? Wadau mnaoijua sheria naomba msaada.
Wadau napenda kuungana na manyanyaso2012 kwenye hoja yake hii ingawa ningependa kuiweka sawa kama ataridhia.
Nadhani hoja/swali lake hapa ni Je mwajiri anaweza mlazimisha mwajiriwa aende likizo bila malipo?
Je sheria na kanuni za kazi zinaruhusu?
 
Back
Top Bottom