Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,461
- 12,216
Wakuu wa JF amani kwenu!
Kuna jambo nimelifikiri kwa muda sasa, nami nikaona ni vema kulileta hapa jukwaani ili tulijadili.Jambo lenyewe ni kuhusu kuipa CHADEMA kura kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2020.Ingawa 2020 inaonekana ni mbali lakini ni miaka minne tu kutoka sasa, hivyo kitu kizuri kinahitaji maandalizi na mikakati ya muda mrefu.
Litakuwa jambo la ajabu kwangu kudhani kwamba kuna chama kingine cha siasa kitakachoweza kuiondoa CCM madarakani tofauti na CHADEMA. CHADEMA ndicho chama kikuu cha upinzani kwa sasa, kimevipita vyama vingine vya upinzani kwa kuwa na mtaji mkubwa wa rasilimali watu hadi fedha.Hivyo nimeona niizungumzie CHADEMA kama possible successor wa CCM kwenye kushika dola kwa mwelekeo wa wakati huu.
HISTORIA YA CHADEMA KATIKA CHAGUZI KUU:
Kwa mbio za urais CHADEMA kimeshiriki chaguzi kuu tatu, yaani chaguzi za 2005, 2010 na 2015.Kwenye chaguzi za 1995 na 2000 CHADEMA kilinga mkono vyama vya NCCR Mageuzi na CUF, kwenye ngazi ya urais.Hawakusimamisha mgombea wa urais kwenye chaguzi tajwa(unaweza kunisahihisha kama nipo kinyume).Kwa maana hiyo mbio za kusaka mlango wa Ikulu kwa CHADEMA zilianza 2005.
CHADEMA NA UCHAGUZI MKUU 2005:
Hapa alisimama F.Mbowe kama mgombea wa kiti cha urais kwa CHADEMA.Kwa mtazamo wangu walijitahidi sana, Mbowe alipata kura 668000 na kitu sawa na 5% na kujinyakulia nafasi ya tatu.Kwenye uchaguzi wa kwanza wa chama kama hiki mbele ya miamba ya siasa kama CCM na CUF ukijumlisha na mitazamo ya watanzania kwa wakati huo, CHADEMA walijitahidi kwa kupata walau zaidi ya kura nusu milioni.Huwezi kuwalaumu hata kidogo zaidi ya kuwapongeza.
CHADEMA NA UCHAGUZI MKUU 2010:
Hapa alisimamishwa Dr.Slaa kama mgombea wa urais.2010 CHADEMA kilishakuwa maarufu karibu maeneo yote ya nchi.Kilishajiimarisha kifedha pamoja na idadi ya wanachama, ushahidi upo kwani Dr.Slaa alipata zaidi ya kura 2000,000.Kutoka kura laki 6 hadi kura milioni 2 na zaidi ilikuwa hatua kubwa ya maendeleo ya kichama.Hata hivyo CHADEMA kilitoa manung'uniko ya kuibiwa kura na CCM.
Dr.Slaa alilalamika sana akidai alipata kura zaidi ya zilizotangazwa na kutaka zoezi la kuhesabu kura lirudiwe.Sii haba kwani wabunge wa CHADEMA waliongezeka maradufu kulinganisha na chaguzi za nyuma.Morali iliyotokana na matokeo ya 2010 ukijumlisha na kuongezeka kwa wabunge, kuliipa CHADEMA nguvu ya kufanya operesheni mbalimbali zilizokitangaza chama nchi nzima.Hata hivyo gear ya kushindwa uchaguzi ilikuwa kuibiwa kwa kura zao na Dr.Slaa hakusaini matokeo ya urais wala kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mshindi wa urais.
CHADEMA NA UCHAGUZI MKUU 2015:
Huu ndio ulikuwa uchaguzi wa kihistoria tangu tuanze kupiga kura.Hapa alisimamishwa mtu mzima, Edward Lowasa.Ukweli usiopingika watu waliamini CCM ilikuwa hoi sana, hasa kutokana na kashfa za ufisadi zilizopamba sura ya CCM, wachache sana walikuwa na imani nacho.Kuwepo kwa UKAWA,idadi kubwa ya wafuasi wa CDM, nguvu ya Lowasa kisiasa, kulisababisha watu waamini mambo mawili, yaani mwisho wa CCM na mwanzo wa CHADEMA kwenye dola au CCM warudi tena kwa mkono wa chuma.
Mchuwano ulikuwa mkali, watu waliamini EL ndiye rais wa JMT, hata baadhi ya wafuasi wa CCM waliamini hivyo.Ile hofu ya kuibwa kwa kura haikuwepo kwani EL aliwataka watu wampigie kura na kuwaaminisha kuwa hakuna hata kura moja itakayo ibwa.Siku hazigandi mara 25 Oct. ikafika na watu kupanga foleni vituoni kupiga kura.Matokeo ya uchaguzi yanafahamika kwa kila mtu, madiwani, wabunge wa kutosha na kura milioni sita, sii haba kwani hata ushindi wa JK 2010 haukuwa wa kura 6M.
Lakini ukichunguza kwa umakini utagundua kwamba CDM waliangukia pua kwenye uchaguzi wa 2015 kuliko chaguzi zilizopita.Nguvu iliyotumika na matokeo yaliyopatikana haviendani, hawakushinda urais, wabunge wakuchaguliwa hawakufika walau 100 wala mikoa mingine hawakupata wabunge na kupoteza wabunge makini bungeni.Hili jambo lilikatisha watu tamaa juu ya CDM...CDM wamekuwa wakijifariji na vitu kama kupata meya wa JJ la Dar na kuongeza idadi ya wabunge tufauti na ile ya 2010.
Kama ilivyo kwa mbaazi kukauka kisha kusingizia jua, CDM hawakuishiwa na lawama.Walilalamikia tume yenyewe, vyombo vya dola, pamoja na katiba kwa kutokuruhusu kupingwa kwa matokeo ya urais mahakamani.Walifika mbali zaidi na kudai kura ziliibwa na wengine wakadai ''pengine'' EL alishinda kwa 62%.Hizi lawama zimekuwa zikitolewa na CDM mara baada ya kushindwa kwenye uchaguzi, hata 2010 nilizisikia pia.
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020:
Itakapofika 2020 CDM watapanda majukwaani tena kuomba kura huku wakiwaaminisha wananchi kwamba wanakwenda kutwaa dola.Kwa mazingira yale yale ya 2010 na 2015, Tume ile ile, na katiba ile ile au watakayoona mbovu zidi(katiba pendekezwa), CDM wata wajaza wananchi matumaini ya kutwaa dola lakini baada ya uchaguzi kupita wanakuja na gear ya lawama
SASA NAULIZA:
Hivi kuelekea 2020 CDM wanafanya maandalizi yapi kutatua lawama zao?
Wana mpango gani kuhakikisha wanapata katiba mpya na tume huru itakayoleta uchaguzi huru?
Watafanya nini kurudisha matumaini na imani ya wananchi juu ya chama na hatimaye kupata kura?
Je kama hali itakuwa kama ilivyo ifikapo 2020, nikiipa CDM kura yangu nitakuwa tofauti na mtu anaye piga pedo baiskeli isiyo na mnyororo huku akiwa na matumaini ya kupanda kilima? au mtu anayejaribu kumpa mimba mwanamke asiye na kizazi kwa matarajio ya kupata mtoto?
NAWASILISHA HOJA KARIBUNI KWA MAJADILIANO.