Je, Nape Nnauye anapinga kila kitu cha Chadema?

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Siasa za nchi nyingi duniani, Tanzania ikiwemo, ni za milengo au vyama tofauti, lakini pamoja na utofauti huu yapo mambo ambayo huwa yanafanana na si jambo la ajabu kukuta mtu wa upande mmoja akikubaliana hadharani na mambo fulani ya upande mwingine.
Tumemsikia Nape mara nyingi akikemea mambo kama rushwa na uongozi mbaya usio na manufaa kwa wananchi. Haya ni baadhi ya mambo ambayo Chadema pia mara zote inayakemea.
Swali ni kwamba je, Nape yuko tayari kutamka hadharani kwamba anakubaliana na Chadema katika kusisitiza ubaya wa rushwa na maovu mengineyo ambayo yanaliumiza taifa na kuahidi kushirikiana nao kuyatokomeza?
 
Dmatemu,
kweli hayuko tayari maana ndiyo yeye aliwahi kusema NCHI KWANZA CHAMA BAADAE KWA MAMBO YA NCHI LAZIMA KUVUKA MIPAKA YA ITIKADI WAKATI MWINGINE.

kiongozi nape mbona kuna mambo ya msingi yainzishwa kwenye thread unapotea. bila kutoa maoni yako....... Nchi kwanza

Rejea hapa kwnee comment hii no #68 za wadau wengine tpue maoni yako mkuu au hata uziptoa maoni jaribu kutafuta namna huko.

Hivi chama chenu kina sera gani na kinasemaje juu ya Teknohama kwenye sekta mbali mbali.

Kama ni nchi kwanza mara moja moja jena utaduni wa utembela na kuomba hoja za wadau . Njoo kwenye Jukwaa la Teknolojia tukupe maoni . Msihisie tu kwenye SIASA. siasa na wansiasa ni chanzo cha matatzio mengi lakini siasa sio suluisho la hata 25% ya matatizo tuliyonayo. ....
 
Dmatemu,
kweli hayuko tayari maana ndiyo yeye aliwahi kusema NCHI KWANZA CHAMA BAADAE KWA MAMBO YA NCHI LAZIMA KUVUKA MIPAKA YA ITIKADI WAKATI MWINGINE.
Kila mtu anaweza kusema hivyo kwenye utekelezaji ndipo shida inapoanzia.
 
Back
Top Bottom