Dalili za ugonjwa wa UTI kwa wanaume

fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,984
1,026
Uti wamgongo unatokana na namna ya kubeba vitu...au kazi unazo fanya...kitanda unacho lalia na mambo mengi tu.

Sidhani kama sex inahusika na uti wa mgongo...kukujibu swali lako, yeap unaweza kupata uti wa mgongo bila kufanya sex.
 
Ni UTI na sio uti wa mgogo. Na hii thread ungeipeleka kwenye jukwaa lake la jf doctor. Au kwa sababu umeweka neno KUSEX
 
Ni UTI na sio uti wa mgogo. Na hii thread ungeipeleka kwenye jukwaa lake la jf doctor. Au kwa sababu umeweka neno KUSEX
Duuu mimi nilidhani anaongela utu wa mgongo...Thanks.
 
No idea ila najua watoto wengi huwa unawapelekesha sana. Watu wazima sijui inakuwaje...labda kina mama
 
A urinary tract infection (UTI) is a bacterial infection that affects part of the urinary tract. When it affects the lower urinary tract it is known as a simple cystitis (a bladder infection) and when it affects the upper urinary tract it is known as pyelonephritis (a kidney infection). Symptoms from a lower urinary tract include painful urination and either frequent urination or urge to urinate (or both), while those of pyelonephritis include fever and flank pain in addition to the symptoms of a lower UTI. In the elderly and the very young, symptoms may be vague. The main causal agent of both types is Escherichia coli, however other bacteria, viruses or fungi may rarely be the cause.

Urinary tract infections occur more commonly in women than men, with half of women having at least one infection at some point in their lives. Recurrences are common. Risk factors include female anatomy, sexual intercourse and family history. Pyelonephritis, if it occurs, usually follows a bladder infection but may also result from a blood borne infection. Diagnosis in young healthy women can be based on symptoms alone. In those with vague symptoms, diagnosis can be difficult because bacteria may be present without there being an infection. In complicated cases or if treatment has failed, a urine culture may be useful. In those with frequent infections, low dose antibiotics may be taken as a preventative measure.
In uncomplicated cases, urinary tract infections are easily treated with a short course of antibiotics, although resistance to many of the antibiotics used to treat this condition is increasing. In complicated cases, longer course or intravenous antibiotics may be needed, and if symptoms have not improved in two or three days, further diagnostic testing is needed. In women, urinary tract infections are the most common form of bacterial infection with 10% developing urinary tract infections yearly.

In young sexually active women, sexual activity is the cause of 75–90% of bladder infections, with the risk of infection related to the frequency of sex.[SUP][/SUP] The term "honeymoon cystitis" has been applied to this phenomenon of frequent UTIs during early marriage. In post-menopausal women, sexual activity does not affect the risk of developing a UTI. Spermicide use, independent of sexual frequency, increases the risk of UTIs.[SUP]
[/SUP]

Women are more prone to UTIs than men because, in females, the urethra is much shorter and closer to the anus.[SUP][/SUP]As a women's estrogen levels decrease with menopause, her risk of urinary tract infections increases due to the loss of protective vaginal flora.
 
Mimi ninavyofahamu ugonjwa huu wa UTI huwapata sana pia watoto wadogo na wachanga vile vile ambao hata sex hawajui ni kitu gani.
 
Habari zenu wakuu,

Naomba kupata msaada wa kujua dalili za ugonjwa wa Urinary Track Infection (UTI) kwa wanaume na nini madhara yake.

Nashukuru sana in advance
 
UTI ni nini ?

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.
Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata

tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.
Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.
Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.
Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI

UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.

Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.
Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi (cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.
Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.
Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika

Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.

Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.@Pafyum
 
UTI ni nini ?

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea
(bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.

Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata

tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.
Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.

Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI

UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.

Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.

Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi
(risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi
(cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.

Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.
Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika

Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.

Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati
.@
Pafyum

Nashukuru sna kaka Mzizimkavu, kwakwel nimejifunza mengi kuhusu ugonjwa huu maana nilikuwa naskiaga tu mtu anaumwa UTI but nilikuwa sijui ni nn hasa! Mungu akubariki sna
 
Kinga kushuka inasababishwa na nini. Mimi nimekuwa nikitumia antibiotics mara kwa mara na nilipokwenda kupima full blood picture niliambiwa white blood cells count ipo 3.74 wakati minimum ni 4.0. Je, inaweza kuwa sababu ni hiyo ya kutumia mara kwa mara dawa? Je, ioi white blood cells ziongezeke nahitaji kufanya nini mbali ya kujiepusha na matukizi ya mara kwa mara ya dawa?
 
ndugu wa humu naombeni msaada njia zinazopelekea mwanaume kupata huu ugonjwa wa U.T.I maana kuna mdogo wangu amepima leo urine kaambiwa ana huoo ugonjwa. Je mwanaume anawezaje pata U.T.I .? Karibuni nyoteee kwa michango yenu.
 
kufanya ngono na mtu mwenye vimelea vy u.t.i....matumizi ya choo hasa kile kichafu
 
U.T.I ni urinary Track Infection

so urethral sijui ndo iko infected au epididymis sikumbuki vizuri biology yenyewe ya division 5

it is either through sharing toilet , choo hakisafishwi vizuri ( dettol na harpic is effective)
 
Inawezekana sana kwa mwanaume kupata UTI:-
•kujamiina na mwanamke mwenye UTI bila kinga.
•Vyoo vichafu hasa vya umma
•Kuvaa chupi chafu kwa muda mrefu
au ku-share hizi underpants na aliepata hai bacteri.
 
ndugu wa humu naombeni msaada njia zinazopelekea mwanaume kupata huu ugonjwa wa U.T.I maana kuna mdogo wangu amepima leo urine kaambiwa ana huoo ugonjwa. Je mwanaume anawezaje pata U.T.I .? Karibuni nyoteee kwa michango yenu.

Hata masturbation inachangia U.T.I
 
Back
Top Bottom