Je, Mwakyembe kujiuzulu Ubunge?!

Mwanafalsafa wa Kijeruman Arthur Schopenhauer aliyeishi kati ya miaka ya 1788-1860 aliwahi kusema.
"Ukweli Wowote hupitia Ngazi tatu.

Kwanza ngazi ya kukejeliwa.
Pili,ngazi ya Kupingwa na hata ikibidi damu kumwagika .
Tatu, ni Ngazi ya Kukubalika ,kwa kuwa ukweli hujisimamia wenyewe"

Richmond ,Lowassa , na Mafisadi sasa wapo hatua ya ngapi?

Mkuu angalia wasije kusema umesema DAMU IMWAGIKE!
WATA KU JMUSHI..BE WARE!
UCHUNGU WAKE HAUUFAHAMU.
 
Mwanafalsafa wa Kijeruman Arthur Schopenhauer aliyeishi kati ya miaka ya 1788-1860 aliwahi kusema.
"Ukweli Wowote hupitia Ngazi tatu.

Kwanza ngazi ya kukejeliwa.
Pili,ngazi ya Kupingwa na hata ikibidi damu kumwagika .
Tatu, ni Ngazi ya Kukubalika ,kwa kuwa ukweli hujisimamia wenyewe"


Richmond ,Lowassa , na Mafisadi sasa wapo hatua ya ngapi?

Unaongelea ukweli unaopingana na mafisadi au mafisadi wenyewe?

This can be interpreted both ways, with opposing results.
 
hivi haya majadiliano ya bunge yanakwenda kwa mpangilio gani?
manake tulitegemea kuwa siku moja ifike aje waziri atoe ripoti imetekeleza vipi mapendekezo ya kamati ya bunge hivi ile siku imepita au bado?
au ndio amehisi wanataka kuiua hoja?
sitashangaa, manake hawa watu mafisadi wana pesa za kutosha, halafu walivyo wajinga wanapeana moyo kwa mambo ya kijinga kama haya.
sijui daktari wetu yuko wapi atutibu watanzania.
mimi huwa napenda sana bunge la baadhi ya states za USA yani historia ya kila mbunge ya choices katika kura zake inajulikana, hakuna kura ya siri.



Haika sasa unaweza kuelewa kwa nini am calling for Vodacom boycott.
 
Niliwaambia waikatae bajeti wakagoma.
Baada ya hapo nikaazisha thread ya ccm bai bai..!
Kuna anayebisha sasa?
Ama kuna anaye bisha lolote?
 
I reserve opining much about the details.

I find the "nitajiuzulu" comment outrageous. He was elected to work for the people, despite majungu and all.Sasa huku ku whine "nitajiuzulu" kunatoka wapi?

Pundit,
Mimi nilivyoelewa kauli ya Dr Mwakyembe ni kuwa ana uhakika na kilichofanywa na kamati na ushahidi upo..kwahiyo kama akina Lowassa wata-prove kuwa kamati ilikosea yuko tayari kujiuzulu ubunge. Na kama (akina Lowassa et al.) wakishindwa ku-prove kuwa kamati ilisema uongo basi na wao wajiuzulu pia hata ubunge walio nao sasa. I would think this could be a brillliant idea. Wouldn't you?
 
Pundit,
Mimi nilivyoelewa kauli ya Dr Mwakyembe ni kuwa ana uhakika na kilichofanywa na kamati na ushahidi upo..kwahiyo kama akina Lowassa wata-prove kuwa kamati ilikosea yuko tayari kujiuzulu ubunge. Na kama (akina Lowassa et al.) wakishindwa ku-prove kuwa kamati ilisema uongo basi na wao wajiuzulu pia hata ubunge walio nao sasa. I would think this could be a brillliant idea. Wouldn't you?

Post ya kwanza imesema,

Mbunge wa Kyela Dr,Mwakeyembe amelitaka bunge kutengua kanuni ili kuurudisha upya majadala wa Richmond Bungeni na wao kama kamati waruhusiwe kusema yote na ikibainika kuwa kuna mtu walimwonea yeye pamoja na wajumbe wa kamati yake wako tayari kujuuzulu ubunge wao.

Sioni sehemu ilipoandikwa kwamba kama Lowassa naye ikibidi, kwa kufuata logic hiyo hiyo ya kuprove / kushindwa kuprove uongo wa kamati, ajiuzulu.

Kuongelea kujiuzulu kwa mwanamapinduzi aliye vitani ni dhambi kubwa sana.
 
Baada ya matukio haya naamini kwamba JK na hata Spika ni part ya wizi wa mali zetu na Rais pia .Haya si mambo yanaweza kufanywa na watu wenye uchungu na Nchi .Sitta ni mnafiki sana na nia yao sasa inawaumbua .Mwakyembe sina hakika kama atafika kokote .Kilango hii ngoma haiwezi maana amesha anza kulewa support za Watanzania na kusema CCM ndiyo wenyewe lakini issue ya kutimiza ama kutenda wanashindwa .
 
Ataungwa mkono soon na mjumbe mmojawapo wa kamati ambaye inategemewa atapata nafasi ya kuzungumza jioni hii ,waliopo karibu na TV zao fuatilieni kujua na msikie wenyewe .

Tupo ngazi ya pili ya ukweli.......
 
Ataungwa mkono soon na mjumbe mmojawapo wa kamati ambaye inategemewa atapata nafasi ya kuzungumza jioni hii ,waliopo karibu na TV zao fuatilieni kujua na msikie wenyewe .

Tupo ngazi ya pili ya ukweli.......

Hii ngazi ni hatari watanzania waendelee na MAOMBI.
 
Unaongelea ukweli unaopingana na mafisadi au mafisadi wenyewe?

This can be interpreted both ways, with opposing results.

Ninaongelea,
Naomba kunukuu, Lowassa alisema kuwa ,nimedhalilishwa sana, nimeumizwa sana, nimekejeliwa sana, ..........najua kuwa watu wanachotaka ni huu uwaziri mkuu wangu ............

Ngazi ya kwanza ya ukweli kulingana na huyu bwana ni kukejeliwa, Lowassa alikejeli kamati ya Richmond.

Hili ndio nilikuwa nalizungumzia .
 
Nilishawahi kusema kuwa KIKWETE NI FISADI COMPLETELY na nalisema tena kama mnanifungia sawa, angalia anafanya nini sasa hivi kwenye madini yetu kama sio kuifisadi nchi
Pili anawashikilia mafisadi na kutotoa msimamo huku akikimbilia mambo ya zimbabwe wakati na sisi ndio tunaelekea huko, baada ya kutoa solution anakimbilia ya watu

Sasa hakuna ya kudoubt kama Mr President is not a member of this Mafisadi Group

Sidhani kama kuna mtu atakufungia ukisema kuwa Kikwete ni fisadi.... kama ni hivyo kuna wengi sana wataafungiwa hapa.
 
Patently. It is self-evident that stifled you from even expressing freely what exactly they stifled you from expressing.

I was finding myself relegated to second guessing creative tendencies, hesitating from even mentioning my favorite psalms relevant to the subject and arrived at not due to religious fanaticism, but from my love of poetry, analogies, similes and metaphors.

Tusitake kuweka mitego ya panya itakayowakuta waliokusudiwa na wasiokusudiwa.Kama kuna watu wanaleta religious fanaticism inayoondoa amani washughulikiwe.Siyo kusema mtu hawezi kuweka Zaburi zake, hadith zake au stanza zake za Lotus Tree.
 
Rostama Azizi keshavunja katiba ya jamuhuri ya muungano kwa kuwa raia wa IRAN kinyume na taratibu za nchi!
Huyu ana maslahi ya nani huko bungeni?
Ameruhusiwa vipi kuwa muamuzi wa TAIFA LETU?
ANARUHUSIWA VIPI KUWA BUNGENI KAMA ALIKIUKA CONSTITUTION YETU KWA KUWA NA DUAL CITIZENSHIP?
 
Hii ishu ingekuwa imeisha kama JK angekuwa na maamuzi ya busara ya kutoogopa wenzake, lakini kwa jinsi inavyokwenda inatoa "circumstancial evidence" kuwa na yeye ni aidha muhusika au mshirika.

Lowasa alipewa mda wa kujieleza bungeni, hiyo ndio ilikuwa nafasi yake ya kusema ukweli na kukana yote ambayo hakuhusika nayo, alichokifanya ni "kuanchia ngazi" yuko bungeni siku zote kwa nini asijipe nafasi ya pili basi ajitee tena kama kuna majungu au mtu anasema uongo basi amuumbue.

Dr Mwakyembe kwa taarifa yake anawashangaa hawa watetezi ambao wanaropoka inaonekana hawakuipitia report vizuri swali ni kwamba walipitisha yapi katika azimio la bunge kama sasa wanaonekana hawakumbuki waliyoyapitisha?
 
Ninaongelea,
Naomba kunukuu, Lowassa alisema kuwa ,nimedhalilishwa sana, nimeumizwa sana, nimekejeliwa sana, ..........najua kuwa watu wanachotaka ni huu uwaziri mkuu wangu ............

Ngazi ya kwanza ya ukweli kulingana na huyu bwana ni kukejeliwa, Lowassa alikejeli kamati ya Richmond.

Hili ndio nilikuwa nalizungumzia .

Got you,

Ingeweza pia kueleweka kama "Lowassa alikejeliwa" na sasa ndiyo watu wanamuelewa which is so incosistent with your record hapa.

Ndiyo maana nikataka clarification.

Ahsante.
 
Ndio maana kuna mtu alishauri kuwa majukwaa yote yaunganishwe na jukwaa la siasa, inawezekana alijenga kwenye hii argument yako kuwa kila kitu ni sawa tu as longer as kina balance.. ndio hivyo?

Sio hivyo.

Mwnkjj kasema dini sio mahala pake hapa. Na kwamba mapambio yale yameegemea upande mmoja. Wataonekana jamvi lao la dini moja.

Mi nikamuuliza basi tukiwahimiza wa dini nyingine wachomekee maudhui yao ili muwe fifte fifte itatatua concern yako, akasema hapana, mapambio pambio yakizidi sio poa. Dini sio mahala pake.

Ndio nikamwambia basi swadakta. Usilete habari ya kwamba JF itaonekana inamilikiwa Wakristo.

Hakutakiwa kusema hivyo. Hilo -kama unasoma katikati ya mistari - ni dongo kwa Waislamu. Kwamba wataleta kompleini!

Yale yale mambo ya ku qualify, ku modify na ku clarify public statements.

Nitamalizia kwa kunukuu msemo wa Mgiriki mmoja wa Kike:

"Get it?"
 
Tusitake kuweka mitego ya panya itakayowakuta waliokusudiwa na wasiokusudiwa.Kama kuna watu wanaleta religious fanaticism inayoondoa amani washughulikiwe.Siyo kusema mtu hawezi kuweka Zaburi zake, hadith zake au stanza zake za Lotus Tree.

Umekurupuka.

Mwjkjj hakusema usiimbe nyimbo za Zaburi hapa kabisa kabisa. Kasema mapambio ya hapa na pale ni sawa ila yasizidi.

Alipokosea - kwa mawazo yangu - ni pale alipoongezea kusema kwamba tatizo ni kwamba jamvi litaonekana linamilikiwa na Wakristo kwa sababu kulikuwa na mapambio tu, hakukuwa na maudhui ya dini nyingine. Lakini hapo hapo akakataa kwamba ukileta aya za Korani itatatua concern yake. Nikamwonyesha kwamba haleti mantiki.

Alikosea kusema wataambiwa jamvi linamilikiwa na Wakristo. Ndani ya hiyo hoja kuna tasnifa kwamba Waislamu wataleta kompleini. Ni dongo la kidini hilo. Hapo ndipo nilipo m call out. Lakini unaweza kutuletea tungo za Zaburi.
 
Date::6/25/2008
Mwakyembe apigilia msumari wa mwisho Richmond
*Asema wasioridhika na maamuzi waombe mjadala uanze upya
*Adai ikibainika waliwaonea waliotajwa na kamati watajiuzulu ubunge

Na Kizitto Noya, Dodoma
Mwananchi

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge iliyochunguza Zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopewa Kampuni ya Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, ameibuka bungeni mjini Dodoma na kutishia kuwa, kama kuna wabunge wasioridhika na maazimio ya Bunge, waombe kazi hiyo ifanyike upya ili yasemwe yote, hata yaliyoachwa ili kulinda heshima ya serikali.

Akizungumza kwa kujiamini bungeni jana, Dk Mwakyembe alisema katika hatua hiyo, ikithibitika kuwa kamati yake ilimwonea mtu katika uchunguzi na mapendekezo yake, yeye na wajumbe wake wako tayari kujiuzulu ubunge na kwamba ikithibitika kuwa ilitenda haki, watuhumiwa wajitoe kwenye nyadhifa zao serikalini.

Pamoja na pendekezo hilo, Mwakyembe alibainisha kuwa kitendo cha baadhi ya wabunge kuzungumzia suala hilo, kinakiuka kanuni za 53 na 54 za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazomzuia mbunge kukumbushia mambo ya Bunge yaliyojadiliwa na kutolewa maamuzi.

Pendekezo: Kama wapo wasioridhika na maamuzi ya Richmond tutengue kanuni hizo ili tuendeshe mjadala mwingine kusudi watu waseme na sisi (kamati) tuseme yote hata ambayo hatukuyasema kwa heshima ya serikali, alisema Mwakyembe.

Dk Mwakyembe alikuwa anatoa mchango wake katika mjadala wa kuchangia Bajeti ya Waziri Mkuu, akiwakumbusha wabunge kuwa kamati yake iliundwa kwa uamuzi wa Bunge, hivyo kitendo cha baadhi ya wabunge kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond ni kulidhalilisha Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kero moja, ambayo ni michango ya baadhi ya wabunge kukosoa maamuzi ya kamati kuhusu Richmond. Badala ya kuzungumzia mambo ya msingi watu wako 'busy kusafishana'. Unamsafisha nani?� alihoji Mwakyembe.

Alisema baadhi ya wabunge wanadhani kuwa uamuzi wa Richmond ni wake (Mwakyembe) na hivyo wako huru kuukosoa na kusahau ukweli kwamba Bunge linaulinda kwa kanuni.

Tukikutwa tulimwonea mtu, tuko tayari kujiuzulu ubunge, lakini ikithibitika tulikuwa kweli, wahusika wajitoe kwenye nyadhifa zao serikalini, alisema.

Wakati Mwakyembe akitoa msimamo huo, wabunge walionekana kuwa makini zaidi kusikiliza hoja zake tofauti na mwanzoni alipokuwa akijitambulisha rasmi kwamba amerudi bungeni na afya yake inaendelea vizuri.

Nawashukuru watu walioniombea pamoja na homa yangu kutiwa chumvi sana ambapo wengine walisema nimefariki, lakini namshukuru Mungu afya yangu inaendelea vizuri, alisema Dk Mwakyembe kabla ya kuanza kutoa mchango wake.

Katika mchango wake Dk Mwakyembe pia aliishauri Serikali kuhamisha Kitengo cha maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ili kuongeza ufanisi.

Aliema kitengo hicho kihamishwe na kiajiri wastaafu wa JWTZ ambao watafanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko ukiritimba unaofanywa na Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimwa Mwenyekiti kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kimejaa ukirimba wa kiraia. Kazi waliofanya wanajeshi kujenga daraja mkoani Mbeya kwa siku nne, ingefanywa kwa hata miezi minne na kitengo cha maafa, alisema.

Sakata la Richmond lilibadili hali ya siasa ya nchi kufuatia maamuzi ya mazito ya Mkutano wa Mumi wa Bunge, na kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, alijiuzulu baadha ya kutajwa kwenye ripoti ya kamati hiyo.

Katika uchunguzi uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge chini ya Dk Mwakyembe, ulibaini nafasi ya waziri mkuu ilishindwa kuwajibika kuzuia ufisadi huo.

Baada ya kujiuzulu Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamgi na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki Dk Ibrahim Msabaha awali alikuwa Waziri wa Nishati na Padini, pia walijiuzulu.

Maamuzi hayo yalisababisha yalimfanya Rais Jakaya Kikwete avunje Baraza la Mawaziri.

Baada ya Rais kuvunja baraza, Cunge lilitoa mapendekezo 23 kwa serikali ambayo yalipaswa kufanyiwa kazi ambayo baadhi ni kutaka wahusika wote wa mkataba wa Richmond, wachukuliwe hatua na kwamba malipo dhidi ya kampuni hiyo yasitishwe.

Hata hivyo, tangu maamuzi ya bunge katika mkutano huo wa 10 kumekuwa na juhudi mbalimbali za kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond akiwemo Lowassa.
 
Back
Top Bottom